Alinialika tuishi wote nimsitiri, sasa anadai nichangie kodi ya nyumba

Ulichemka ulipokubali kuhamia Kwa mwanamke. Siku zote mwanamke huhamia Kwa Mwanaume na ikitokea tofauti ni Kama imebidi napo iwe Kwa siku chache tu.
Kama mwanamke, huyo alihitaji MTU wa kumsaidia mahitaji ila alikosea kutokukuweka wazi.
Tafuta Chumba uhame au lipia kodi ya watu. Vya bure hakuna siku hizi.
 
Mjini hapa hakuna vya bure. Hukuvutwa kwenda kwake leo unamchambua kwamba humpendi mala chakula kama kuna msiba, kijana jitambue
Alafu kama unatunga vile hiyo yako nyumba unaijenga na mawe?! Maana unasema ulipumzika kazi.
Jamani mtu wa elfu unaforce kwa malaki lazima upwelepwetwe. Mjini hapa kila nyumba ina namba. Ukijua kupokea jua na kutoa. Hakuna cha bure.

Teh teh duuuh nimejikuta naguna kwa sauti mkuuu... Nina hakika utakuwa unaishi zenji au tanga,, na kama upo dar basi una undugu wa kuchora na isha mashauzi...
 
Ww nae ni dume? au yaani akili za kuishi kwa mwanamke na huo umri wako mjomba mbna kama aibu?
 
Kama mlikubaliana hakuna kuchangia chochote wewe komaa tu dadeki...Mwanaume msimamo bwana.
 
Ulidhani umepata mteremko????

Baada ya kutakiwa kutoa 200,000 ( ambazo kwa mwaka ni 2.4m) ndio ukajua kuwa hukuwa unampenda?
Ndio ukajua nyumba haikauki ndugu?
Ndio ukajua chakula kikipokwa ni kama msiba ( halafu mwanaume umejuaje mambo ya chakula? Mambo ya jikoni????)

Anyway....mwanaume sio kufunga mkanda.... mwanaume ni majukumu...pambana
 
Teh teh duuuh nimejikuta naguna kwa sauti mkuuu... Nina hakika utakuwa unaishi zenji au tanga,, na kama upo dar basi una undugu wa kuchora na isha mashauzi...

Mkuu hawa watu wanaudhi sana. Dume zima linakaa kwa mwanamke alafu anaomba ushauri. Wa moja havai mbili
 
Kama unalalamika kwenye pesa ndogo tu kama laki4, wewe kutoa laki2 tu hiyo nyumba yako unayojenga itaishia lini. Alafu usione vyaelea ujue vimeundwa, nadhani ulikuwa unajua hayo yote ila umeingia kichwa kichwa mwenyewe tu, kwa kupenda vya mtelemko. Nilidhani kwenye ulaghai ni wanawake tu peke yao ndiyo huingia kingi, kumbe hata wanaume pia.
 
Back
Top Bottom