Alinialika tuishi wote nimsitiri, sasa anadai nichangie kodi ya nyumba

Yaani hapo ulipofikia unataka ushauri tena?Hama haraka iwezekanavyo maana huyo mwanamke alikutegeshea mtego na wewe umeingia kichwa kichwa
 
You are a pathetic excuse of a man (pardon my french).
Mwanaume unatakiwa uwe unafanya maamuzi yenye uzito na faida kwa jamii. Hapo ndipo unaonekana we kweli ni mwanaume na si mvulana.
Ukifanya maamuzi lazima yageuke msaada kwa jamii;
We umeharibu
1) Umedisturb maisha ya mdogo wako (wewe kama kaka ni jukumu lako pia)
2) Umedisturb maisha ya ndugu yako uliyempelekea mdogo wako (angekuwa na akili zako mdogo wenu angeishi wapi?)

Kiufupi kuhoji tabia yako;
a) wanaume wenzio huwapangia nyumba wasichana wa kupass nao time bila kwenda kuishi nao, we mtu humpendi. Why on earth would you go live at her house?
b) Na unategemeaje mtu akulipie kodi? We ulivyotoka kwenu si uliaga unakwenda jitegemea?
c) Kwa hiyo hata hiyo kodi yako umeshindwa kuiongeza hata kidogo ukampa? Mwenye nyumba wako angeongeza kodi ungeenda ishi kwa kakako?

Dude get the hell out of her house!
 
Kwa muda mrefu sasa, nimekua nikisumbuliwa na mambo ya mapenzi hasa kazini, nikaamua nifuate ushauri wenu niachane na mapenzi ya sehemu za kazi, nikafanya hivyo

Hapo katikati nikakutana na Dada mmoja wa makamo na mwenye watoto wawili wa 9 na 12 yrs yeye ana 36 yrs mimi nina 32 yrs tukawa tuna date, kwa kweli anajiweka vizuri sana huwezi jua kama ana watoto au ana 36 yrs.

Akaniomba niamie kwake tuishi wote maana amepanga nyumba nzima na wanawe wote wapo boarding, nikaona poa tu sio mbaya, nilikua nakaa na mdogo wangu wa kike ambae yupo tu home alipata matatizo kazini, nikamuomba akaishi kwa kaka yetu mkubwa ili niepukane na kodi kwa kuhamia kwa mwanamke wangu.

Tangu nimehamia kwa mwanamke wangu ni miezi miwili, sasa juzi nashangaa ananiambia eti kodi imeisha tunatakiwa kulipia nyingine hivyo tuchangie nusu kwa nusu, wakati mwanzo akiniomba tukae wote alisema yeye ana uwezo wa kulipa kodi mwenyewe kama siku zote, sasa nashangaa kanigeuka hiyo ni haki kweli?

Mimi nilikokua nimepanga mwanzo nilikua nalipa kodi ya 60,000/= per month, hapa tulipo sasa ni 400,000/= sasa anataka nichangie 200,000/= na land lord anataka kwa mwaka mi ntaweza wapi hiyo kodi?
Si bora nirudi kule kwa mwanzo

Yeye alidai anataka kuishi na mwanaume amechoka upweke hivyo nimsitiri atagharamia kila kitu nashangaa sasa anakuja na lugha mpya.Kwanza mimi sikua nampenda nilimsaidia tu, sipendi kuchukua mwanamke mwenye watoto, hapa nilipanga nijibanze kwake hadi hapo baadae, sasa najikuta naingia kwenge budget nisiyotarajia.

Nyumba yenyewe ndugu kila siku wanapishana humu, chakula kikipikwa utadhani kuna msiba, mi nilishazoea gharama ndogo kabisa, kwanza huwa nakula town nikirudi ni kulala tu.

Nashangaa yeye ananifosi nicha gie gharama za uendeshaji nyumba kinyume na makubaliano, kwa hali hii nyumba yangu itaisha kweli?Sikutaka kuoa ili nikamilishe hiyo nyumba, bora nisepe tu.

Wadau mna mawazo gani juu ya hill?

ivi na wewe ni mwanaume una mbupu mbili?unakula bure, unalala bure unambato bure, still u cant pay 200000? Shameless man! What kind of a person a u???

Ila na nyie wanawake mnatutia aibu utakalibishaje jitu kama hili kwako kisa kuliwazwa??? Kwann mnajifanya cheap? Mwanammenakupeleke hotel dats all. Unless kakuoa.

Aisee kwangu sikaribishi mwanaume hata kutembea siweziiiiiii tutakutana hotelin na si kuniletea mikos kwangu.
 
wow...kwahiyo unataka huyo dada akuhudumie kila kitu bure? huoni aibu, ni mamako uyo? you should better yourself!
 
Duuuu!!utaweza kuwa na familia kweli wewe na ndugu wakakutembelea wakala na kulala kwa jinsi ulivozoea vya vbure wanaumewengine bhana ,unawadhalilisha wanaume wenzio
 
Inawezekana mie ndo nimesoma vibaya, huyo bro aliyealikwa ana miaka 32 ama 12..!? huh
 
Kwa muda mrefu sasa, nimekua nikisumbuliwa na mambo ya mapenzi hasa kazini, nikaamua nifuate ushauri wenu niachane na mapenzi ya sehemu za kazi, nikafanya hivyo

Hapo katikati nikakutana na Dada mmoja wa makamo na mwenye watoto wawili wa 9 na 12 yrs yeye ana 36 yrs mimi nina 32 yrs tukawa tuna date, kwa kweli anajiweka vizuri sana huwezi jua kama ana watoto au ana 36 yrs.

Akaniomba niamie kwake tuishi wote maana amepanga nyumba nzima na wanawe wote wapo boarding, nikaona poa tu sio mbaya, nilikua nakaa na mdogo wangu wa kike ambae yupo tu home alipata matatizo kazini, nikamuomba akaishi kwa kaka yetu mkubwa ili niepukane na kodi kwa kuhamia kwa mwanamke wangu.

Tangu nimehamia kwa mwanamke wangu ni miezi miwili, sasa juzi nashangaa ananiambia eti kodi imeisha tunatakiwa kulipia nyingine hivyo tuchangie nusu kwa nusu, wakati mwanzo akiniomba tukae wote alisema yeye ana uwezo wa kulipa kodi mwenyewe kama siku zote, sasa nashangaa kanigeuka hiyo ni haki kweli?

Mimi nilikokua nimepanga mwanzo nilikua nalipa kodi ya 60,000/= per month, hapa tulipo sasa ni 400,000/= sasa anataka nichangie 200,000/= na land lord anataka kwa mwaka mi ntaweza wapi hiyo kodi?
Si bora nirudi kule kwa mwanzo

Yeye alidai anataka kuishi na mwanaume amechoka upweke hivyo nimsitiri atagharamia kila kitu nashangaa sasa anakuja na lugha mpya.Kwanza mimi sikua nampenda nilimsaidia tu, sipendi kuchukua mwanamke mwenye watoto, hapa nilipanga nijibanze kwake hadi hapo baadae, sasa najikuta naingia kwenge budget nisiyotarajia.

Nyumba yenyewe ndugu kila siku wanapishana humu, chakula kikipikwa utadhani kuna msiba, mi nilishazoea gharama ndogo kabisa, kwanza huwa nakula town nikirudi ni kulala tu.

Nashangaa yeye ananifosi nicha gie gharama za uendeshaji nyumba kinyume na makubaliano, kwa hali hii nyumba yangu itaisha kweli?Sikutaka kuoa ili nikamilishe hiyo nyumba, bora nisepe tu.

Wadau mna mawazo gani juu ya hill?

Jamani hivi hawa ndio wanaume wa leo! Kazi kweli kweli lakini na nyinyi wanawake mkome kupenda kusitiriwa na watoto wenu (32 V 36)
 
sasa si uondoke au kakufunga kamba

Jitambue kijana hauna hata aibu kuhama kwako na kwenda kuolewa kwa mwanamke mwenye watoto 2 ukijidanganya kuwa una save ili umalizie ujenzi wa nyumba yako, hakina dezo ktk dunia ya leo tena ndani ya jiji la Dar, nakupa pole na ushauri wa bure beba kilicho chako rudi kwako.
 
Kizazi cha wanaume werevu ndo kinaishia hivyo huko mbeleni sipati picha tutakuwa na wanaume wa namna gani iwapo wewe ndo baba wa hicho kizazi kijacho
 
Haujaweza kufanya vzr kazi uliyoitiwa.
Achia wanaume waje. Halafu unatudhalilisha sie wanaume
 
Umeeleza upande mmoja,je kilichokuleta hapo unakimudu?
au ameona unamtia hasara akaona akufukuze kiaina?
 
Back
Top Bottom