Alinialika tuishi wote nimsitiri, sasa anadai nichangie kodi ya nyumba

jean phillipe beyun

Senior Member
May 18, 2015
142
225
Kwa muda mrefu sasa, nimekua nikisumbuliwa na mambo ya mapenzi hasa kazini, nikaamua nifuate ushauri wenu niachane na mapenzi ya sehemu za kazi, nikafanya hivyo

Hapo katikati nikakutana na Dada mmoja wa makamo na mwenye watoto wawili wa 9 na 12 yrs yeye ana 36 yrs mimi nina 32 yrs tukawa tuna date, kwa kweli anajiweka vizuri sana huwezi jua kama ana watoto au ana 36 yrs.

Akaniomba niamie kwake tuishi wote maana amepanga nyumba nzima na wanawe wote wapo boarding, nikaona poa tu sio mbaya, nilikua nakaa na mdogo wangu wa kike ambae yupo tu home alipata matatizo kazini, nikamuomba akaishi kwa kaka yetu mkubwa ili niepukane na kodi kwa kuhamia kwa mwanamke wangu.

Tangu nimehamia kwa mwanamke wangu ni miezi miwili, sasa juzi nashangaa ananiambia eti kodi imeisha tunatakiwa kulipia nyingine hivyo tuchangie nusu kwa nusu, wakati mwanzo akiniomba tukae wote alisema yeye ana uwezo wa kulipa kodi mwenyewe kama siku zote, sasa nashangaa kanigeuka hiyo ni haki kweli?

Mimi nilikokua nimepanga mwanzo nilikua nalipa kodi ya 60,000/= per month, hapa tulipo sasa ni 400,000/= sasa anataka nichangie 200,000/= na land lord anataka kwa mwaka mi ntaweza wapi hiyo kodi?
Si bora nirudi kule kwa mwanzo

Yeye alidai anataka kuishi na mwanaume amechoka upweke hivyo nimsitiri atagharamia kila kitu nashangaa sasa anakuja na lugha mpya.Kwanza mimi sikua nampenda nilimsaidia tu, sipendi kuchukua mwanamke mwenye watoto, hapa nilipanga nijibanze kwake hadi hapo baadae, sasa najikuta naingia kwenge budget nisiyotarajia.

Nyumba yenyewe ndugu kila siku wanapishana humu, chakula kikipikwa utadhani kuna msiba, mi nilishazoea gharama ndogo kabisa, kwanza huwa nakula town nikirudi ni kulala tu.

Nashangaa yeye ananifosi nicha gie gharama za uendeshaji nyumba kinyume na makubaliano, kwa hali hii nyumba yangu itaisha kweli?Sikutaka kuoa ili nikamilishe hiyo nyumba, bora nisepe tu.

Wadau mna mawazo gani juu ya hill?
 

housegirl

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
3,127
2,000
Mtu anaweza kufikiri ana upweke kumbe ukame tu unamsumbua. Haya ukame umeisha sasa back to reality. hahaaaa. lipa bills bro akae akulipie kila kitu kwa lipi??? hahaaa
 

Clueless14

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,994
2,000
Aisee wanaume bwana! Kwa hiyo ulitaka vya bure ili umalizie nyumba yako wewe halafu umwache yeye kwenye mataa?? Hivi km huna mpango na mtu kwa nini mnampotezea muda?
 

cutte bee

Member
Feb 8, 2015
97
125
Mjini hapa hakuna vya bure. Hukuvutwa kwenda kwake leo unamchambua kwamba humpendi mala chakula kama kuna msiba, kijana jitambue
Alafu kama unatunga vile hiyo yako nyumba unaijenga na mawe?! Maana unasema ulipumzika kazi.
Jamani mtu wa elfu unaforce kwa malaki lazima upwelepwetwe. Mjini hapa kila nyumba ina namba. Ukijua kupokea jua na kutoa. Hakuna cha bure.
 

bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,387
2,000
Ikiwa huna mkataba nae basi funga virago pole pole uondoke hakuna cha bure brother.

Na kila ukikaa na kuwaza waza kibahili ndiyo utashindwa kuondoka na utaishia kuoa na kubeba familia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom