Aliniahidi kupokea utajiri kwa panda mbegu ya utajiri (pesa). Mwaka wa tano sasa napigwa. Je, nawezaje kumfungulia mashtaka tapeli huyu?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,427
154,274
Mwaka 2016 nilienguliwa ofisini pale hazina kwa kuwa na vyeti feki. Sio kwamba vyeti vyangu vilikuwa feki, ila matokeo yangu ya form 4 hayakuwa mazuri Sana, nikachonga cheti na kwenda high school ambako nilipata division 1 ya point 3 ya halali kabisa na kisha kwenda chuo, ambako niligraduate with a distinction.

Nikafanya Masters nje ya nchi na kuhitimu vizuri Sana. Bujibuji kichwa Sana, sema sometimes shit happens.
Nilipo ondolewa kazini nilikuwa na ka akiba kangu kadogo. Licha ya kwamba nilikuwa na kazi nzuri, sikuwa na utajiri wa mapesa kwani Mimi ndiye niliyekuwa nasomesha watoto wa ndugu zangu wote. Kwetu Ni Mimi peke yangu niliyesoma na kupata kazi nzuri. Kwa hiyo nilikuwa na jukumu kubwa Sana la kubadilisha hali ya ukoo wetu kifikra, kiuchumi na kimtazamo.

Na kweli kupitia Mimi familia iliyosemwa imelaaniwa, ikaanza kuonekana kuwa Ni familia yenye Baraka. Waliokuwa wanatutenga wakaanza kujipendekeza kwetu.

Ukiwa masikini unadharaulika sana, hata ukiwa ndani ya basi unaweza ukashangaa kunguru anaingia, anakunyea kisha anaondoka huku akikutazama kwa dharau.

Mwaka ule nilipoondolewa kazini, kuna siku nilienda Rudi's Farm kula kitimoto na pia nilikuwa ninaamini ntakutana na watu wapya maishani mwangu wenye mawazo mapya kwangu.

Nikiwa nimekaa nasubiri Masai aniletee portion ya ribs na chop nusu, akaja mezani kwangu jamaa mmoja mtanashati, akanisalimia, akakaa. Mhudumu alikuja na kumsikiliza mtu Yule, akaagiza fanta na maji.

Mezani nilikuwa nimelaza Konyagi kubwa GuDume a.k.a Faru Mshana Jr na chupa ya St. Anna.

Jamaa akawa busy kidogo na simu yake, Mimi nikawa busy na kutengeneza cocktail yangu ya St. Anna na Konyagi. Jamaa akamaliza simu Yake, Kisha akaniita kwa jina langu la nyumbani, kijijini kabisa hukoooo. Jamagege habari yako? Nikamuuliza umeniongelesha? Akajibu ndio Jamagege, nimekuongelesha.

Akajitambulisha, kabla sijataka kumuuliza kanifahamia wapi, akaendelea na kuniambia Mambo yangu mbalimbali, ikiwemo sehemu ilipo wallet yangu ambayo tangu siku kadhaa nyuma nilikuwa siioni. Na kwa kunithibishia maneno Yake, nikapiga simu home, nikamuuliza wife, umeiona ile wallet? Akajibu kuwa bado hajaiona, nikamwwlekeza sehemu ambayo nipo, naye alipoenda pale, akaikuta.

Aliniambia Mambo yangu mengi ya sirini, Siri za michepuko yangu, Siri zangu na mke wangu. Akanitisha zaidi alipoanza kunieleza mipango niliyonayo kichwani, ambayo sijaiandika Wala kumwambia mtu yoyote, akaniambia hadi idadi ya vifaranga nyumbani vilivyototolewa asubuhi.

Tukapiga story nyingi sana, akaniambia yeye ni mtumishi na ana kanisa lake, ambalo natakiwa niwe nasali ili mambo yangu yanyooke.
Mimi ni Mhasibu, ninayetambulika na bodi mbalimbali za uhasibu duniani. Akaniambia anaona kwenye ulimwengu wa roho, kuwa kuna asasi ya kigeni itanipigia simu ndani ya siku mbili nikafanye nao kazi, kazi itakuwa ya siku chache ila utalipwa 30 mil, nikaona huyu anaropoka tu.

Baada ya siku moja, kweli nilipigiwa simu, jamaa wakataka nifike ofisini kwao tuongee. Kesho yake mapema asubuhi, nikaenda Mirambo 50, nikaongea nao, tukakubaliana kufanya kazi. Wakanipa USD 1000 kama allowance yangu, na kazi tukapatana use 14500.

Duh, nikampigia simu Yule mtumishi, akasema niende akaniombee ili niendelee kupanda utukufu hadi utukufu. Nikafanya kazi na kuikamilisha kwa muda mfupi tofauti na matarajio yao. Wananipenda sana.

Mara kwa Mara waliniita na Mimi nikajiona mwenye bahati. Nikamnunulia mtumishi kiwanja ili ajenge kanisa kubwa, kwani alikuwa amekodiwa ukumbi Sinza.

I'll asasi ilikuwa inahusika na Mambo ya haki za binadamu na ilikuwa ikitetea mashoga, ilifukuzwa nchini na mh. Dili zikakata.
Nikakaa kitambo bila kazi, kila biashara ninayojaribu inaanguka, sikuwa na ujuzi Wala uzoefu wa biashara. Mambo yakaanza kuwa magumu.

Mtumishi akawa anasisitiza kunifanyia maombi, ananiambia nipande mbegu ya utajiri, hiyo mbegu nampa yeye, hiyo mbegu ni fedha nyingi.

Kila Mara anasema pokea utajiri, pokea madola, pokea heshima, pokea kazi, sioni cha kazi wala utajiri. Mambo yakaendelea kudinya huku yeye akinona na kanisa lake likiongeza waumini.

Niliendelea kwenda kusali kwake, ila nikaanza kupoteza imani naye, nikaona sio msaada Tena kwangu. Kwa huyo mtumishi nimepoteza mamilioni mengi Sana, Tena Sana, je nawezaje kumshitaki ili anirudishie pesa zangu?

Hapoy nyuma kidogo alikuwa akinidharau na kunibeza, Sasa nimepata kazi kwenye Taasisi moja ya nje, wamenipa na Prado TX ya 2018 natembelea, mtumishi kaanza Tena kujipendekeza.

Huyu kimburu nataka nikamfilisi mahakamani. Naombeni msaada wa mawaidha yenu
 
Kimsingi labda umhukumu wewe kama wewe,sina ninachojua kuhusu sheria lakini ninaona wazi kua atakushinda maana ni jambo la imani ambalo ulilibeba wewe mwenyewe. Cha kufanya hiyo ni darasa tu la kuja kufundisha wajukuu zako kuhusu matapeli, unaweza kumtafuta na kumchana wazi wazi kua asikuzoee tena na unaomba kwa heshima na usalama wa siku za usoni akurejeshee kiasi fulani.

Akikataa endelea na maisha mengine na utafanikiwa, kama kuna sheria ya kumpeleka mahakamani kwa maana ya kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu ninaona wazi atakushinda tu maana mahakama sidhani kama itamlazimisha huyu mchungaji feki kua ulicho mpa hakikua sadaka.

We pambana kivingine na maisha yataenda tu. Kama una mahala pa kulala, watoto wako wanakula na kwenda shuleni,nguo unafua na kuvaa zikiwa safi,kuna nini huku duniani unachotaka? Chapa mwendo mwingine Man.
 
Katika maisha bujibuji umepitia Mengi sna ila inatosha kusema Mungu wako anakupenda na Wew ni mtu mweny bahati sna.

Ila uyu mchungaji si alikutabiria kweli mwanzo?
Ni ikawa
Ulio itoa ni sadaka ya shukrani.

Kama upako umeisha nenda kwingine, ulilete battle na watumishi wa Mungu.

Alafu Mkuu kwa visa vyako vyote jifungie ndani usali wew mweny maana Mungu unae mtumikia hajawahi kukupungukia kbsa.
 
Mbegu sio sadaka. Sadaka Ni kafara, lazima ife. Mbegu Ni mbegu lazima iote na izae zaidi. Ndio maana nilikuwa namlipa kwa bank deposits na kwenye deposit slip nilikuwa naandika hii Ni mbegu ambayo iwapo itakufa nitaidai
Mkuu mi naona wafate wanasheria wabobezi ili upate kwanza msaada wa mawazo.
 
Mbegu sio sadaka. Sadaka Ni kafara, lazima ife. Mbegu Ni mbegu lazima iote na izae zaidi. Ndio maana nilikuwa namlipa kwa bank deposits na kwenye deposit slip nilikuwa naandika hii Ni mbegu ambayo iwapo itakufa nitaidai
Mkuu sina hakika kama mahakama inaamini hayo mambo ya mbegu na blah blah zingine. Cha muhimu umeshagundua huyu mtumishi ni mtu kunguni mnyonya damu wewe achana naye fanya mambo yako mengine ila watahadharishe na wengine wasiingie kwenye mtego wake.

Vitu vingine usikaze kichwa kutaka kuvifanya vikubwa potezea tu pengine ile mbegu uliyokua unapanda ndio hiyo imeota. Lakini pia kwa sisi wakulima tunatambua siyo kila mbegu utakayopanda itaota nyingine zinagoma. Nadhani umenielewa.
 
Hiv Bujibuji visa vyako ni kweli au unatulisha tango pori tu? Una visa vingi sana.

Na kama ni kweli, mtegemee Mungu sana maana anakupitisha kwenye mengi kukufundisha. Jitahidi sana kuwa karibu na Mungu.

Achana na wazo la kufanya vita na watumishi wa Mungu. Wanayemtumikia mwenyewe atawahukumu.

Endelea kumtegemea Mungu ataendelea kufanya maajabu yake kwako! Haya ndo maoni yangu.
 
Tengeneza bomu la petrol tukalipue kanisa lake, unafanya mashambulizi consecutively mpaka waumini wakimbie pawe sio mahali salama tena na mamlaka zitapafunga mbona simple tu mjomba.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom