Aliniahidi kupokea utajiri kwa panda mbegu ya utajiri (pesa). Mwaka wa tano sasa napigwa. Je, nawezaje kumfungulia mashtaka tapeli huyu?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,409
2,000
Huyu "kimburu"..
Kule kwetu kimburu ni kimbuzi kidogo dogo kile kilichokomaa/dumaa kinapigaga sana kelele zizini kama ni kidume ni ile vinavyoacha kula vinamsumbua mama yao kumdandia dandia ,nyapia nyapia
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,409
2,000
Huyu "kimburu"..
Kule kwetu kimburu ni kimbuzi kidogo dogo kile kilichokomaa/dumaa kinapigaga sana kelele zizini kama ni kidume ni ile vinavyoacha kula vinamsumbua mama yao kumdandia dandia ,nyapia nyapia
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,409
2,000
Huyu "kimburu"..
Kule kwetu kimburu ni kimbuzi kidogo dogo kile kilichokomaa/dumaa kinapigaga sana kelele zizini kama ni kidume ni ile vinavyoacha kula vinamsumbua mama yao kumdandia dandia ,nyapia nyapia
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,409
2,000
Huyu "kimburu"..
Kule kwetu kimburu ni kimbuzi kidogo dogo kile kilichokomaa/dumaa kinapigaga sana kelele zizini kama ni kidume ni ile vinavyoacha kula vinamsumbua mama yao kumdandia dandia ,nyapia nyapia
 

AgentX

JF-Expert Member
Mar 7, 2015
1,581
2,000
Alkasus mujarab kabisa kutoka kwa mtaalam buji buji. Ila hapo mwanzo jamaa alivyokuwa anakutabiria unabii nikadhani ulikutana na wazee wa kitengo. The vetting team.
 

Siku za ajabu

JF-Expert Member
Dec 23, 2012
1,238
2,000
Mwaka 2016 nilienguliwa ofisini pale hazina kwa kuwa na vyeti feki. Sio kwamba vyeti vyangu vilikuwa feki, ila matokeo yangu ya form 4 hayakuwa mazuri Sana, nikachonga cheti na kwenda high school ambako nilipata division 1 ya point 3 ya halali kabisa na kisha kwenda chuo, ambako niligraduate with a distinction.

Nikafanya Masters nje ya nchi na kuhitimu vizuri Sana. Bujibuji kichwa Sana, sema sometimes shit happens.
Nilipo ondolewa kazini nilikuwa na ka akiba kangu kadogo. Licha ya kwamba nilikuwa na kazi nzuri, sikuwa na utajiri wa mapesa kwani Mimi ndiye niliyekuwa nasomesha watoto wa ndugu zangu wote. Kwetu Ni Mimi peke yangu niliyesoma na kupata kazi nzuri. Kwa hiyo nilikuwa na jukumu kubwa Sana la kubadilisha hali ya ukoo wetu kifikra, kiuchumi na kimtazamo.

Na kweli kupitia Mimi familia iliyosemwa imelaaniwa, ikaanza kuonekana kuwa Ni familia yenye Baraka. Waliokuwa wanatutenga wakaanza kujipendekeza kwetu.

Ukiwa masikini unadharaulika sana, hata ukiwa ndani ya basi unaweza ukashangaa kunguru anaingia, anakunyea kisha anaondoka huku akikutazama kwa dharau.

Mwaka ule nilipoondolewa kazini, kuna siku nilienda Rudi's Farm kula kitimoto na pia nilikuwa ninaamini ntakutana na watu wapya maishani mwangu wenye mawazo mapya kwangu.

Nikiwa nimekaa nasubiri Masai aniletee portion ya ribs na chop nusu, akaja mezani kwangu jamaa mmoja mtanashati, akanisalimia, akakaa. Mhudumu alikuja na kumsikiliza mtu Yule, akaagiza fanta na maji.

Mezani nilikuwa nimelaza Konyagi kubwa GuDume a.k.a Faru Mshana Jr na chupa ya St. Anna.

Jamaa akawa busy kidogo na simu yake, Mimi nikawa busy na kutengeneza cocktail yangu ya St. Anna na Konyagi. Jamaa akamaliza simu Yake, Kisha akaniita kwa jina langu la nyumbani, kijijini kabisa hukoooo. Jamagege habari yako? Nikamuuliza umeniongelesha? Akajibu ndio Jamagege, nimekuongelesha.

Akajitambulisha, kabla sijataka kumuuliza kanifahamia wapi, akaendelea na kuniambia Mambo yangu mbalimbali, ikiwemo sehemu ilipo wallet yangu ambayo tangu siku kadhaa nyuma nilikuwa siioni. Na kwa kunithibishia maneno Yake, nikapiga simu home, nikamuuliza wife, umeiona ile wallet? Akajibu kuwa bado hajaiona, nikamwwlekeza sehemu ambayo nipo, naye alipoenda pale, akaikuta.

Aliniambia Mambo yangu mengi ya sirini, Siri za michepuko yangu, Siri zangu na mke wangu. Akanitisha zaidi alipoanza kunieleza mipango niliyonayo kichwani, ambayo sijaiandika Wala kumwambia mtu yoyote, akaniambia hadi idadi ya vifaranga nyumbani vilivyototolewa asubuhi.

Tukapiga story nyingi sana, akaniambia yeye ni mtumishi na ana kanisa lake, ambalo natakiwa niwe nasali ili mambo yangu yanyooke.
Mimi ni Mhasibu, ninayetambulika na bodi mbalimbali za uhasibu duniani. Akaniambia anaona kwenye ulimwengu wa roho, kuwa kuna asasi ya kigeni itanipigia simu ndani ya siku mbili nikafanye nao kazi, kazi itakuwa ya siku chache ila utalipwa 30 mil, nikaona huyu anaropoka tu.

Baada ya siku moja, kweli nilipigiwa simu, jamaa wakataka nifike ofisini kwao tuongee. Kesho yake mapema asubuhi, nikaenda Mirambo 50, nikaongea nao, tukakubaliana kufanya kazi. Wakanipa USD 1000 kama allowance yangu, na kazi tukapatana use 14500.

Duh, nikampigia simu Yule mtumishi, akasema niende akaniombee ili niendelee kupanda utukufu hadi utukufu. Nikafanya kazi na kuikamilisha kwa muda mfupi tofauti na matarajio yao. Wananipenda sana.

Mara kwa Mara waliniita na Mimi nikajiona mwenye bahati. Nikamnunulia mtumishi kiwanja ili ajenge kanisa kubwa, kwani alikuwa amekodiwa ukumbi Sinza.

I'll asasi ilikuwa inahusika na Mambo ya haki za binadamu na ilikuwa ikitetea mashoga, ilifukuzwa nchini na mh. Dili zikakata.
Nikakaa kitambo bila kazi, kila biashara ninayojaribu inaanguka, sikuwa na ujuzi Wala uzoefu wa biashara. Mambo yakaanza kuwa magumu.

Mtumishi akawa anasisitiza kunifanyia maombi, ananiambia nipande mbegu ya utajiri, hiyo mbegu nampa yeye, hiyo mbegu ni fedha nyingi.

Kila Mara anasema pokea utajiri, pokea madola, pokea heshima, pokea kazi, sioni cha kazi wala utajiri. Mambo yakaendelea kudinya huku yeye akinona na kanisa lake likiongeza waumini.

Niliendelea kwenda kusali kwake, ila nikaanza kupoteza imani naye, nikaona sio msaada Tena kwangu. Kwa huyo mtumishi nimepoteza mamilioni mengi Sana, Tena Sana, je nawezaje kumshitaki ili anirudishie pesa zangu?

Hapoy nyuma kidogo alikuwa akinidharau na kunibeza, Sasa nimepata kazi kwenye Taasisi moja ya nje, wamenipa na Prado TX ya 2018 natembelea, mtumishi kaanza Tena kujipendekeza.

Huyu kimburu nataka nikamfilisi mahakamani. Naombeni msaada wa mawaidha yenu
Ungesoma biblia mwenyewe watu kama hao wasingekutisha ni wezi na wachawi kama wachawi wengine wamejifunika tu kwa tiketi ya uchunaji tunawaita fake pastor hujiulizi hv Mungu akupe utabiri wa pochi yako iko sehem fulani ili iweje sasa utabiri sio simple kias hicho soma Bjblia hawatakudanganya hao fakepastor.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom