Alimpa magonjwa best wa mchumba sasa ameambiwa ndiyo best man siku ya harusi ana haha

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Story ni kuwa bibie ambae amekuwa kwenye mahusiano kwa miaka mitano sasa. Alipata bahati kwenda nje ya nchi kwa shahada ya uzamili.

Kuonyesha commitment yake , mchumba alikwenda mara mbili ughaibuni kumuona. Siku anarudi alifanyiwa surprise ya engagement nyumbani baada ya mapokezi.

Ndani ya miezi mitatu kazini baada ya kurudi alipandishwa cheo na kuhamishiwa Arusha. Kule alianza maisha, mapenzi yakiwa uanaendelea mchumba akiwa Dar.

Rafiki wa mchumba alipata safari ya kikazi kwenda Arusha. Jamaa alinunua vizawadi kwa mchumba. Kule Arusha kwa nia njema kabisa bi dada alimwabia shemeji lazima ufike nyumbani. Alipika chakula na wine ya kumezea. Baada ya chakula shemeji alisaidia kuondoa vyombo na story kibao.

To cut a story short walikulana. Wakiahidiana itakuwa siri na wasahau. Sasa kule jamaa amemuomba huyu huyu rafiki yake awe best man akiwa hajui chochote.

Bibi harusi BP iko juu.
 
Atasema kwamba anazaliwa upya kwenye ndoa, yaliyopita si ndwele, wagange yajayo.

Mi kuna bibie kanipigia simu leo kaniambia anaolewa, lakini kabla hajaolewa "anataka kukutana na mimi".

Nikasema makubwa haya.

Sasa mtu unaolewa mimi unataka tukutane iweje?
 
Mimi sipendi kuzoea marafiki wa mr hivyo, kama hayupo wasifike home wamsubiri akiwepo.
 
Mimi sipendinkuzoea marafiki wa mr hivyo, kama hayupo wasifike home wamsubiri akiwepo.
Old school that's how we roll.

Siku hizi tangu mna date siku ya kwanza bibie anataka umtoe yeye na kundi la rafiki zake, sasa hapo ashajenga ukaribu usio na mzurikwa afya njema ya mahusiano yao.

Kuna wawindaji wengine hawaridhiki.
 
Kiranga kwa heshima na taadhima inakualika kwenye hafla ya kurasimisha ndoa yangu mkuu. Endapi hautakua ughaibuni.
 
Kiranga kwa heshima na taadhima inakualika kwenye hafla ya kurasimisha ndoa yangu mkuu. Endapi hautakua ughaibuni.
Kwa sasa nipoughaibuni mpaka Baba Jesca aondoke madarakani.

Hata likizo naenda Jamaica na Turks and Caicos.

Naweza kuja kwenye harusi nikasema mbaya nikafungwa bure.

Niwie radhi, ila nitaomba picha nile harusi kwa macho.
 
Shukrani mkuu. Hilo ntalitekeleza. Licha ya kukuru kakara kwenye mambo mengine, weee ni miongoni mwa watu nnaowaheshimu na kutambua uwezo na vipaji vyao.

Tukirudi kwenye uzi, watu wanafikiri kuoa kunabadili tabia ya mtu, inaweza ikawa hivyo lakini sio mara zote. Watu wenye ndoa zao wanafanya ufuska unategemea nini?

Lakini siku huyo bwana harusi akija kugundua yaliyotokea, kesi yake itasuluhishwa The Hague.
 
Kwa sasa nipoughaibuni mpaka Baba Jesca aondoke madarakani.

Hata likizo naenda Jamaica na Turks and Caicos.

Naweza kuja kwenye harusi nikasema mbaya nikafungwa bure.

Niwie radhi, ila nitaomba picha nile harusi kwa macho.

Oh! Jambo moja nilisahau, mie narasimisha tu ndoa. Wajomba zako tayari wanapanda school Bus hahahahaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom