Alimeza dawa za kuzuia ujauzito (P2) nikimshuhudia lakini kapata ujauzito

elly2p

Member
May 27, 2015
89
364
Habari zenu wanajamvi,

Nina mpenzi ana miaka 23, tumekuwa katika mahusiano kwa miezi 7 sasa. Tunafanya mapenzi vizuri tu ila nilishamuambia mimi sihitaji mtoto na yeye so awe makini kucheki uwezekano wa kupata mimba kabla hatjafanya mapenzi.

Kuna tatizo limetokea wiki tatu zilizopita baada ya game akaniambia ile siku ni ya hatari anaweza akapata mimba, nilimpa hela akaenda kununua P2 na nilimshuhudia akimeza.

Baada ya wiki moja binti kaanza kulalamika anajisikia vibaya akahisi ana mimba nikamshauri baada ya wiki mbili nenda kanunue UPT tucheki akakubali akaja na kipimo tukapima kipimo kikaonesha ana mimba.

Swali ninalojiuliza ni hii kitu imekuwaje wakati alitumia P2 napata hisia mbaya pia kuna uwezekano mabaharia wamenizidi kete anataka kunishikisha.
 
Nina mtoto sasa hivi ana miaka mitatu mie na huyu wife wangu tulicheza sana huo mchezo wa P2

Siku vikagoma ndio vile tena sasa hivi baba na mama.

Nasikia hivyo vitu vipo feki so wazee wa dry kuweni makini msije ingia matatizoni makaja ua mtu kwa abortion ooh.
 
Pole Mkuu jiandae tu kisaikolojia kukubaliana na hali halisi, kama hutaki kuoa basi Lea mtoto ili hali mama awe single maza.

NB: mwanamke akikupenda na ukionesha huna future naye, hayo ndo matokeo yeye anayoyataka
 
elly2p, Mimi ilinitokea nilime, @ p2 na mimba nikapata kwasababu nilikuwa ndani ya ndoa niliamua kuiacha nimejifungua juzi tu japo mtoto nilomfatisha ni mdogo sana, hana hata mwaka nilijifungua mwaka huu mwezi wa kwanza mwanzoni tu nikapata mimba mwezi wa tatu mwanzoni tu mtoto akiwa mchanga kabisa ile siku ya kwanza na du baada ya kujifungua nikameza p2 hola nimejifungua juzi tarehe 21/11/2019 siku ya alhamis . huyu mkubwa akiwa na miezi 11 so watoto 2 nimewazaa mwaka mmoja.
 
Nawaona ma dokta mkitoa maoni ynu.

Mkuu mtoa mada hii ungeileta tu kule habar mchanganyiko au mmu
 
Back
Top Bottom