Alikuwa Milionea Kijana, Hivi Sasa Anakusanya Taka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alikuwa Milionea Kijana, Hivi Sasa Anakusanya Taka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 26, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Mamilioni yote yameisha Callie anafanya kazi ya kukusanya taka</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Thursday, August 27, 2009 2:21 PM
  Akiwa na miaka 16 alishinda bahati nasibu na kuwa milionea kijana lakini baada ya miaka sita tu hivi sasa amefilisika na ili kupata pesa za kuganga njaa anafanya kazi ya kukusanya takataka.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Akiwa na miaka 16 tu alifanikiwa kushinda bahati nasibu ya takribani paundi milioni 2 ( Zaidi ya Tsh. Bilioni 4) lakini hivi sasa ikiwa imepita miaka sita tu, pesa zote zimeisha na ili apate pesa za kuganga njaa imembidi afanye kazi ya kukusanya taka.

  Lakini kabla ya kuanza kazi hiyo kutokana na stress alizokuwa nazo alijaribu kujiua mara mbili bila mafanikio.

  Huyo si mwingine ni Callie Rogers mwanamke wa nchini Uingereza ambaye hivi sasa akiwa na umri wa miaka 22 anaishi na mama yake baada ya maisha ya kifahari ya miaka sita baada ya kushinda bahati nasibu ya paundi milioni 1.875.

  Callie hivi sasa kutokana na jinsi alivyochacha anahaha kutafuta kazi za kufanya usafi kwenye majumba ya watu hasa kipindi hiki ambacho uchumi wa Uingereza unatetereka.

  Callie huwaambia rafiki zake "Maisha yangu ni kama naishi chini ya ardhi, Pesa zilinifanya niwe mtu nisiyekuwa na furaha. Kushinda bahati nasibu kumeyateketeza maisha yangu".

  "Nilizitumia pesa kuwafurahisha watu waliokuwa wakinizunguka lakini jambo hili halikuniletea furaha zaidi ya watu kujaribu kuwa karibu nami kwaajili ya pesa zangu", alisema Callie.

  Callie hivi sasa anaendesha gari kuukuu lililotumika aina ya Volkswagen na nyumba yake aliyoinunua wakati huo yenye thamani ya paundi 180,000 anaipiga mnada ili kupata pesa za kujikimu.

  Mwezi wa saba mwaka 2003 aliposhinda bahati nasibu jina lake lilisikika sana kwenye magazeti akijulikana kama mtu wa pili mwenye umri mdogo kushinda bahati nasibu hiyo kubwa na ghafla maisha yake yalibadilika kuwa milionea kijana.

  Takribani paundi 450,000 alizitumbua kwenye kununua nguo na viatu vya wanamitindo maarufu pamoja na kufanya operesheni mbili za kurekebisha matiti yake.

  Alitumia paundi 255,000 kununua zawadi, magari ya kifahari na kutoa mikopo kwa watu wa familia yake.

  Callie alikuwa hana bahati pia kwenye mahusiano ya kimapenzi kwani mpenzi wake wa kwanza, Nicky Lawson, aliyempata wakati huo na kuzaa naye watoto wawili alitembea na rafiki yake wa karibu na kumfanya ajaribu kujiua bila ya mafanikio.

  Mpenzi wake wa pili Ryan Thompson, alikuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya na mwezi wa 12 mwaka jana alikamatwa akimiliki silaha kinyume cha sheria na kutupwa jela miaka miwili.

  Callie anasema marafiki zake walimkimbia baada ya pesa zake kuisha.

  "Nilijaribu kujiua kwasababu pesa nilizozipata baada ya kushinda bahati nasibu hazikuniletea furaha zaidi ya kuyaangamiza maisha yangu, natamani nisingeshinda bahati nasibu". alimalizia Callie.</td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; text-align: center; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2931526&&Cat=7

  </td></tr></tbody></table>
   
 2. K

  Kijamani Senior Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Muambieni anitafute nitamsaidia.
   
 3. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Aaah,maisha ndio hivyo tunatafuta ,tunapata,zinapotea au tunaziacha,so there is no time to regret in this so called life!!
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  MziziMkavu... huu ni ukumbi wa picha....
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  kibunango huioni hiyo picha ya kusikitisha?alikuwa tajiri kaamka masikini faida za kujirusha sana hizo teteteteteh
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Siyo lazima iwe starehe. kuna factors nyingi unabidi uangalie. Kwanza kama mtu haja wahi kushika kiasi cha pesa hicho ni vigumu kujua nini kuzifanyia. Unaziwekeza wapi wakati hauona experience hiyo? Pili lazima uconsider umri aliyo shindia hizo hela. Dogo wa miaka 16 una tegemea ata fanyia nini cha maana na pesa hizo? Tatu kwa sababu ya umri wake lazima utambue kuna watu lazima walikua wanamshauri kuhusu hizo pesa. Je alikua anapewa ushauri gani? Wewe fanye experiment hii ili niprove my point. Mchukue dogo wa miaka kumi unaemjua kisha mpe kiasi cha laki moja. Usimambie jinsi ya kuzitumia halafu baadae mfuate umuulize kazi tumiaje hizo pesa. Naku hakikishia chances are dogo katumia pesa kwenye vitu vya kijinga sana ambavyo wewe mtu mzima ungesema mtoto hana akili. Hela za ghafla haswa ambazo hauja zifanyia kazi ni vigumu sana kuzi tunza.
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Ndio tujifunze.....sio lazima bahati nasibu hata pesa zetu ndg ndg inabidi tujiheshimu na matumizi.....
   
 8. Keynez

  Keynez JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 640
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 80
  Deja Vu.....hii imewatokea wengi tu walioshinda bahati nasibu, wengine wametupwa jela, wengi wamesema they wish they never won in the first place. Ni rahisi kusema haya wewe yasingekutokea kwa kuwa ni mtu mzima, au umesoma, lakini there is something about free money that almost always end up being a curse. Namuonea huruma, lakini nadhani tu amekuwa frustrated/dissapointed. Kama hana madeni, chochote kilichobaki, ikiwemo nyumba hiyo akituliza akili anaweza kufanya vizuri tu.
   
 9. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Amefulia
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hiyo picha mbona kama anatoa taka nyumbani kwake? Utafanya kazi ya kukusanya taka bila kuvaa overalls na gloves? Magazeti ya udaku noma!
   
 11. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwa watanzania msiende mbaaali katika kutafakari suala hili kwani Ma miss wetu wengi unaweza kuwatumia kama kigezo cha pesa za kuokota, wengine unaoweza kuwatumia kama kigezi ni wale wote wanaorithi pesa ambazo haziko kwenye mifumo ya biashara. Kila binadamu ana nafasi yake ya kuwa limbukeni once,then ndio anaweza kujipanga upya. Bahati mbaya inakuwa 'golden chance never come twice'
   
 12. Mahmood

  Mahmood JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 7,851
  Likes Received: 1,336
  Trophy Points: 280
  Bahati nasibu ni kamari,

  Kamari haina baraka.

  Kucheza kamari ni miongoni mwa madhambi makubwa na ni kamba madhubuti ya Shetani.

  Pia ni ugonjwa wa hatari kama vile ulevi, na ukiota mizizi kwenye moyo wa mtu huwa taabu kuponeka.

  Nayo ni njia ya kupotezea wakati na mali, na humpelekea mcheza kamari kuwa bakhili na kufanya vitendo vilivyo haramu. Na ili kutimiza na kufanikisha lengo lake, mcheza kamari yuko tayari hata kuuwa ili apate fedha za kuchezea kamari au kuweka rehani nyumba yake au mkewe. Na kamari huleta uhasama na ugomvi baina ya watu. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Maida aya ya 90 na ya 91,

  "Bila shaka ulevi na kamari na kuabudiwa (kuombwa) asiekuwa Mwenyezi Mungu, na kutazamia kwa mishale ya kupigia ramli (na kwa vinginevyo); (yote haya) ni uchafu (ni) katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufaulu (kutengenekewa). Hakika Shetani anataka kukutilieni uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anataka kukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na (kukuzuilieni) kusali. Basi je, mtaacha (mabaya hayo)?"

  Na Mwenyezi Mungu S.W.T kasema kuwa fedha za mchezo wa kamari ni fedha za haramu, katika Suratil Baqarah aya ya 188,

  "Na wala msiliane mali zenu baina yenu kwa batili (dhuluma)..."

  Na Mtume S.A.W. katuhakikishia haya kasema kuwa mali ya kamari ni mali ya haramu na adhabu ya mtu yule anayekula mali ile ni Moto wa Jahannam katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari,

  "Hakika wanaume wameshughulika katika kupata mali ya Mwenyezi Mungu bila haki watakuwa Motoni siku ya Kiyama."

  Kwa jinsi ilivyokuwa kucheza kamari ni kitendo cha uovu imekuja katika Hadithi kukatazwa hata kusema tu, "Njoo tucheze kamari." Na atakayesema hivyo basi lazima atoe kafara ya sadaka. Mtume S.A.W. kasema katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari,

  "Atakaesema kwa rafiki yake "Njoo tucheze kamari," lazima atoe sadaka."
   
Loading...