Alikuwa Milionea, Hivi Sasa Anakusanya Taka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alikuwa Milionea, Hivi Sasa Anakusanya Taka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 16, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Alikuwa Milionea, Hivi Sasa Anakusanya Taka
  [HR][/HR][​IMG]
  Mamilioni yote yameisha Callie anafanya kazi ya kukusanya taka

  Akiwa na miaka 16 alishinda bahati nasibu (Kamari) na kuwa milionea kijana lakini baada ya miaka sita tu hivi sasa amefilisika na ili kupata pesa za kuganga njaa anafanya kazi ya kukusanya takataka! Akiwa na miaka 16 tu alifanikiwa kushinda bahati nasibu ya takribani paundi milioni 2 ( Zaidi ya Tsh. Bilioni 4) lakini hivi sasa ikiwa imepita miaka sita tu, pesa zote zimeisha na ili apate pesa za kuganga njaa imembidi afanye kazi ya kukusanya taka.

  Lakini kabla ya kuanza kazi hiyo kutokana na stress alizokuwa nazo alijaribu kujiua mara mbili bila mafanikio.

  Huyo si mwingine ni Callie Rogers mwanamke wa nchini Uingereza ambaye hivi sasa akiwa na umri wa miaka 22 anaishi na mama yake baada ya maisha ya kifahari ya miaka sita baada ya kushinda bahati nasibu ya paundi milioni 1.875.

  Callie hivi sasa kutokana na jinsi alivyochacha anahaha kutafuta kazi za kufanya usafi kwenye majumba ya watu hasa kipindi hiki ambacho uchumi wa Uingereza unatetereka.

  Callie huwaambia rafiki zake "Maisha yangu ni kama naishi chini ya ardhi, Pesa zilinifanya niwe mtu nisiyekuwa na furaha. Kushinda bahati nasibu kumeyateketeza maisha yangu".

  "Nilizitumia pesa kuwafurahisha watu waliokuwa wakinizunguka lakini jambo hili halikuniletea furaha zaidi ya watu kujaribu kuwa karibu nami kwaajili ya pesa zangu", alisema Callie.

  Callie hivi sasa anaendesha gari kuukuu lililotumika aina ya Volkswagen na nyumba yake aliyoinunua wakati huo yenye thamani ya paundi 180,000 anaipiga mnada ili kupata pesa za kujikimu.

  Mwezi wa saba mwaka 2003 aliposhinda bahati nasibu jina lake lilisikika sana kwenye magazeti akijulikana kama mtu wa pili mwenye umri mdogo kushinda bahati nasibu hiyo kubwa na ghafla maisha yake yalibadilika kuwa milionea kijana.

  Takribani paundi 450,000 alizitumbua kwenye kununua nguo na viatu vya wanamitindo maarufu pamoja na kufanya operesheni mbili za kurekebisha matiti yake.

  Alitumia paundi 255,000 kununua zawadi, magari ya kifahari na kutoa mikopo kwa watu wa familia yake.

  Callie alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi ya kiharamu na mpenzi wake wa kwanza, Nicky Lawson, aliyempata wakati huo na kuzaa naye watoto wawili lakini mpenzi wake huyo alitembea na rafiki yake wa karibu na kumfanya ajaribu kujiua bila ya mafanikio.

  Mpenzi wake wa pili Ryan Thompson, alikuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya na mwezi wa 12 mwaka jana alikamatwa akimiliki silaha kinyume cha sheria na kutupwa jela miaka miwili.

  Callie anasema marafiki zake walimkimbia baada ya pesa zake kuisha.

  "Nilijaribu kujiua kwasababu pesa nilizozipata baada ya kushinda bahati nasibu hazikuniletea furaha zaidi ya kuyaangamiza maisha yangu, natamani nisingeshinda bahati nasibu". alimalizia Callie.
   
 2. D

  Derimto JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  biblia inasema hivi kufanikiwa kwa mpumbavu kutamwangamiza na ndicho kilichomtokea huyu dada hajui marafiki wakoje na wanakupendaje ni hasa pale ukiwa nacho kila moja atakupamba
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,041
  Likes Received: 6,480
  Trophy Points: 280
  asante, tutajifunza.
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  ''More Money! More Problem!''
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,811
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  easy come easy go.
   
 6. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  always there is a lesson to be learnt
   
 7. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  atacheza kamari na kupata tena,...mwambie ajipe moyo tu.
   
 8. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Either she was too young to think wise, or maybe she was surrounded by wrong people, or she just didnt win the lottery fairly.. Something must be wrong somewhere!
   
 9. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,832
  Trophy Points: 280
  Hakutoa jasho kupata hizo pesa hivo hana haja ya kuzitolea machozi
   
 10. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Pesa mwanaharamu.
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Aje atoke na Wabongo anaweza akatoka tena.
   
 12. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Unapata bilioni halafu unafilisika? Kichekesho.
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Daaaa,fedha fedhehaaa
   
 14. K

  Karry JF-Expert Member

  #14
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 266
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ndo maisha hayo kuna kupanda na kushuka
   
 15. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #15
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,051
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu! Hasa kwa kuileta kwa kimatumbi.. Somo limegota panapo. Wengi humu huleta habari kama hii kwa kiingilishi, kiasi nalazimika kuwa na mabarafu au maji ya baridi ili kupoza rejeta ya kichwa! Khaa! Senkyu sana.
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  usicheke ndugu yangu. Dah! Hilo ni fundisho.
   
 17. President Elect

  President Elect JF-Expert Member

  #17
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 693
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Na hapa Tanzania kuna mdada alikuwa anakusanya taka maeneo ya o'bay, sasa hivi ni mbunge yuko mjengoni. Bahati haiji mara mbili.
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Aug 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  ni nani?
   
 19. M

  Mfwalamanyambi JF-Expert Member

  #19
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yalikukuta kama hayo???
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  hakuwahi kuwa milionaire.....thats why..
   
Loading...