Alikiba kutua Dar Jumanne hii, kula dinner na wadau muhimu

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
236
306
aada ya kufanya ziara yenye mafanikio nchini Afrika Kusini, Alikiba anatarajiwa kutua Dar es Salaam, Jumanne hii.

16906856_1822214474721420_6467752781024329728_n.jpg

Kiba na timu yake watatua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, saa nane mchana ambapo anatarajiwa kupata mapokezi makubwa.

Baada ya mapokezi hayo, Kiba atakula chakula cha usiku na wadau muhimu wakiwemo wanahabari kwenye hoteli ya Double Tree. Jumatano asubuhi atapaa tena hewani kuelekea Marekani kwa ziara yake ya huko kwenye majiji kadhaa.

Pamoja na ziara yake hiyo nchini Afrika Kusini, Alikiba alikabidhiwa tuzo yake ya MTV EMA pamoja na kupewa tuzo na label yake ya Sony Music baada ya wimbo wake Aje kufikisha views milioni 5 kwenye Youtube.

Pia alifanikiwa kumalizia kurekodi collabo yake na mwanamuziki mkongwe, Yvonne Chakachaka.
 
Nyie watu kuweni serious acheni mchezo. Alivyokua ana perform kwenye zile pubs that can't even accommodate 100 people ndo ilikua tour yenyewe ya South? Tuzo kwa kufika 5M views YouTube? Duh halaf akija apokelewe? Kwa lipi kubwa hadi wananchi wapoteze nauli kwenda airport kumsubiri? Wonders shall never end
 
Si anatuzo ya mtvema best African act
 
Nyie watu kuweni serious acheni mchezo. Alivyokua ana perform kwenye zile pubs that can't even accommodate 100 people ndo ilikua tour yenyewe ya South? Tuzo kwa kufika 5M views YouTube? Duh halaf akija apokelewe? Kwa lipi kubwa hadi wananchi wapoteze nauli kwenda airport kumsubiri? Wonders shall never end
Wenye wivu utawajua tu tayari mapov hayoo
 
Nyie watu kuweni serious acheni mchezo. Alivyokua ana perform kwenye zile pubs that can't even accommodate 100 people ndo ilikua tour yenyewe ya South? Tuzo kwa kufika 5M views YouTube? Duh halaf akija apokelewe? Kwa lipi kubwa hadi wananchi wapoteze nauli kwenda airport kumsubiri? Wonders shall never end
Acheni wivu wa ajabu ndio maana tunaendelea kuwa maskini,nonsense...mxiuuuu
 
Mimi nashauri kwenye interview zake awe anaenda na mkalimani. Ali Kiba atumie lugha ya kiswahili anayoimudu vyema na mkalimani awatafsirie wasiojua. Nimeangalia mahojiano yake na redio moja huko SA, anababaika sana, anatumia nguvu sana mpaka mishipa inamsimama, anaongea vitu havieleweki,maneno sentensi nyingine haziishi baada ya kukosa neno la muendelezo Yah yah Yes Yes no no nyingi sana.

Kutokujua kiingereza sio dhambi lakini kama huwezi kuzungumza basi usilazimishe. Kiswahili sasa hivi ni lugha ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom