Alikiba awapa onyo mashabiki wake wanaomtumia video apost kwa lengo la kukuza mziki wake,asema hatozipost waache

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,204
42,063


















Wasalaam wana jf..
Msanii namba moja na tajiri nchini Alikiba ijumaa wiki hii amewashangaza watu na mashabiki wake baada ya kuwapiga marufuku mashabiki wake wanao imba nyimbo zake au nyimbo za kundi lake na kujirekodi halafu wanamtumia wakitegemea atazipost wakiamini zitasaidia kusukuma nyimbo zake na kusema kamwe hatokuja kupost video hizo hivyo wasijisumbue na yeye si mtu wa namna hiyo kupost clip watu wakiimba nyimbo zake na hatoweza kufanya.

Msimamo huo uliwekwa wazi na msanii Alikiba ndani ya Times FM kwenye kipindi cha Playlist..... Msanii Alikiba alipo endelea kuulizwa kuna ubaya gani mashabiki wako ukiwapost wakiimba nyimbo zako....? Msanii Alikiba alijibu kwa kiumanyema akisema ni wapost kwa what?........'''

Mtangazaji wa Kipindi aliendelea kumuuliza kama kuna account maalum ya mashabiki kutuma clip wakisupport nyimbo zako...... Alikiba alijibu kimanyema akisema yaaaah kuna account ziko blended kwaajili ya hicho kitu........ mtangazaji alitabasamu....

Mtanagzaji alijatibu kumuelewesha Kiba umuhimu wa mashabiki kushiriki kwa njia hiyo lakini Alikiba alisisitiza kuwa yeye si wa aina hiyo na hawezi fanya hivyo........vijana aliyokuwa amefatana nao walionekana kunyong'onyea sana baada ya kauli ya Alikiba dhidi ya mashabiki wake....

NB; Mashabi wa Kiba ni vyema mkawa waelewa msijipendekeze kutuma viclip kwa Kiba tafuteni kwa kuvituma.....yeye si wa namna hiyo haitaji promo.

Wasalaam
 
Mashabiki walishampoteza siku nyingi
Ukisikiliza nyimbo kama macmuga, ya Karim na mapenzi yana ran dunia hi ndio identity yake sio hizi nyimbo anazoimba sasa ili aweze kucheza
 
Back
Top Bottom