AliKiba amefunguka jinsi Dully Sykes alishiriki kutengeneza wimbo wake wa kwanza (2003)

Robidinyo

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
3,736
7,677
Jana kupitia Insta Live, King wa muziki wa Bongo Fleva AliKiba amefunguka namna ambavyo Dully Sykes alishiriki katika kumsaidia kutengeneza wimbo wake wa kwanza mwaka 2003.
.
Dully Sykes alimsikia Alikiba anaimba kwa Mjomba wake, akapenda sauti, akamchukua na kwenda studio kwa Enrico na wakarekodi wimbo wa Kuteseka Nimechoka. Baada ya hapo Dully Sykes akamtambulisha Alikiba kwa G Lover na kuanzia hapo Alikiba akaanza kufahamika.

Hata hivyo Kiba amewashukuru wale wote waliomshika mkono katika safari yake ya maisha wakiwemo, Mully B, Prof Jay, Sugu, Dj Venture, pamoja na Dj Majey aliyekuwa Dj wa kwanza kuchukua CD yake na kumpambania wimbo wake kupigwa.

King Kiba pia awamewataka mashabiki wake kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kwa kufuata maagizo ya mamlaka husika huku akiwataka kukaa mkao wa kula kwasababu Alhamis wiki hii anadodosha wimbo mpya.

Jana mida ya Saa mbili nilipandisha nyuzi hapa kuwapa taarifa wapenzi wa muziki wa bongo fleva kuchat na King wa muziki huu na pia nilitegemea tupeane update kupitia ule uzi kuhusu alichokisema King kwa mashabiki, NIMESIKITIKA BAADA YA KUKUTA UZI UMEFUTWA sijui shida nini kwa Mods kuendelea kufuta nyuzi nazoleta zinazowahusu kiba na Harmonize

Hata huu uzi sitoshangaa baada ya dk kadhaa ukafutwa
officialalikiba_20200407_1.jpg
 
HUYU NI FAILURE TU, ALISHAJIFIA KITAMBO KIMUZIKI LIMEBAKI JINA
Afu bifu mseleleko sasa hivi hakuna, atakufa njaa huyu
...................Mzee usimchukulie mtu aliye bado hai kwa kumuona kuwa ni failure huijui kesho yake.

Amini ktk kushindwa kwako usijiaminishe kwa unayemuhisi ameshindwa kila mtu ana goal lake la kulenga ni muda haujamfikia.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Hakuna msanii hapo... Mambo mengi, akiulizwa na mashabiki lini utaachia nyimbo? Anajibu sipangiwi kutoa nyimbo. Binafsi huyu jamaa anaboa na kwa ujio wa Konde Boy... Huyu jamaa anapotea mdogodogo labda ajiunge konde gang

Sent using Jamii Forums mobile app

Ashapotea tayari huyo!

Kwa nini uandike kuw atapotea? Una chuki nae?
 
...................Mzee usimchukulie mtu aliye bado hai kwa kumuona kuwa ni failure huijui kesho yake.

Amini ktk kushindwa kwako usijiaminishe kwa unayemuhisi ameshindwa kila mtu ana goal lake la kulenga ni muda haujamfikia.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
'Mzee usimchukulie mtu aliye bado hai kwa kumuona kuwa ni failure huijui kesho yake.'

Daah una busara sana mkuu.
 
HUYU NI FAILURE TU, ALISHAJIFIA KITAMBO KIMUZIKI LIMEBAKI JINA
Afu bifu mseleleko sasa hivi hakuna, atakufa njaa huyu
Pengine ungefafanua una maana gani ya kusema huyu ni failure? Jee amekuwa failure kwa sababu ya kushukuru waliomsaidia? Wivu na Chuki ni sumu kali kuliko 'cyanide' hebu punguza kidogo.
 
Back
Top Bottom