alijua ukweli lakini alificha kwa kuogopa atatengwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

alijua ukweli lakini alificha kwa kuogopa atatengwa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by elmagnifico, Feb 7, 2012.

 1. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  Habari ya asubuhi wadau
  Leo ningependa ku share nanyi kisa kilicho mkuta kaka yangu.
  Mnamo mwishon mwa mwaka jana kaka yangu aliugua. Na kipidi hicho mkewe na mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu walikuwa wamesafiri hivyo basi ndani ya nyumba akawa kabaki yeye na mtoto wake wa kwanza mwenye umri wa miaka saba.
  Kwa kawaida kaka yangu ni mlevi sana yeye ni engineer mkuu wa kiwanda flan na ela yake nyingi anamalizia kwenye pombe.
  basi aliugua na akakonda sana ikabidi familia ichukue jukumu la kumhudumia lakini pamoja na kumtaka ahamie nyumbani kwakuwa pale kwake zaidi ya huyo mwanaye hakuwa na mtu wa ziada, jamaa aligoma kata kata. Mkewe naye kipindi hicho ilikuwa ana kama miezi minne toka aondoke kurud kwao na alipopigiwa simu hakuwa tayari kuja kumhudumia mumewe.
  Basi kwa kumlazimisha akapelekwa hospital japo hakupenda maana kila mtu alikuwa na mashaka kama ataliona jua. Hospital walimwekea drip na hakuna msaada zaidi aliopatiwa.
  Siku mmoja asubuhi nesi alikuja kumwona mgonjwa na kaka yangu mwingine ndiye aliye kuwa naye hapo wodini nesi akamuuliza huyo kaka yangu aliyekuwa anamhudumia, file maalum la mgonjwa liko wapi?
  Kaakangu akamjibu file wauliza file gani, nesi akamjbu kumbe nawe hujui lolote toka nje uniache na mgonjwa.
  akatoka nje lakini akabaki anajiuliza kipi kinaendelea. Nesi alipotoka akmamfuata akampa elfu 5 akamhohi kwani nesi kuna nini na ulikuwa waongelea file gani. Nesi akamjibu kwani wewe hujui kama ndugu yenu ana UKIMWI.
  Kaka yangu akabaki anashangaa. Akamwambia usijifanye huji wakati yeye anajua na huu ni mwaka wa pili toka agundue ana UKIMWI.
  Basi ikabidi aje aieleze familia na jukumu likawa ni jinsi gani ataambiwa mgonjwa ili akubariane na hali yake maana alikuwa yuko katika hali ya kukata tamaa.
  Akaitwa nesi ambaye tuna ukoo naye naye akasema alidhan sisi kama famila tunajua ila hatutaki kusema ndiyo maana naye alikuwa haulizi na pale hospital walikuwa hawampi dawa yoyte zaidi ya kumwekea maji na glucosse kwakuwa yeye hataki kuanza dozi na cd4 zake zko chini sana kiasi kwamba hawezi tumia ARV mpaka zipande kwa kiwango flani. Akatushauri kwamba tusimwambie kama tunafahamu lolote yeye ataenda zyngumza naye.
  Na kweli alienda akazungumza naye na jamaa akamwambia alijua miaka miwili iliyopita na kuwa alishataka kujiua mara mbili ila kila alipokuwa akiwakumbuka watoto anaona huruma anaacha. Basi akapewa counselling ya maana na baada ya hapo hali yake ikaanza rudi taratibu.
  Leo hali yake iko poa ila ilibidi watoto wakapimwe na wakakutwa wote hawana mkewe yeye aligoma kupima.
  Nalotaka kusema ni kwamba UKIMWI si kufa lakini ndugu zangu play safe na msi wanynyapae
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Inshallah tutalizingatia hilo..
   
 3. m

  mkazamjomba Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we umenikumbusha mbali sana nimempoteza dada yangu kwa ajili ya mambo ya kuona haya mimi nashukuru niliwahi kumwambia kwa mapenzi mazito nilichogundua alikuwa anaogopa kupima kwa vile alikuwa bosi ofisini na hospital wanamfahamu alijua wangemtangaza vibaya kumbe angewahi angishi mpaka leo najua na bahati mbaya tuliishi mikoa tofauti yaani nalivyorudi tulikuwa tumechelewa anyway tusiogope kupima mungu amrehemu alikolala inaniuma sana
   
 4. Ndechumia

  Ndechumia JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 1,015
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  pole sana , ww ndo wa kwanza kumfariji
   
Loading...