Alijitolea hata kupoteza ndoa yake, kumfichia siri kaka yake!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alijitolea hata kupoteza ndoa yake, kumfichia siri kaka yake!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Tuko, Oct 14, 2011.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  This is too much...

  Hii inshu ilitokea miaka kadhaa iliyopita (miaka kama 18), maeneo ya Dodoma. Asubuhi na mapema dada mtu ambaye wakati huo alikuwa na miaka 3 na mtoto mmoja katika ndoa yake, alijiwa na mdogo wake wa kiume ambaye alikuwa amebeba mtoto mchanga. Waliongea pembeni kwa dakika ambazo hazikuzidi 10, then dada mtu akambeba yule mtoto akarudi nae ndani na mdogo mtu akaondoka. Mumewe yule dada akashangaa ile hali ikabidi amuulize mkewe, vipi mbona shemeji kaja gafla, mmeongea wenyewe na kakuachia mtoto, kuna nini. Hapo ndipo siri ilipoanzia... yule dada alikataa katakata kutoa details za yale mazungumzo au yule mtoto aliyeachiwa zaidi tu ya kusema mdogo wake amemuomba amlelee yule mtoto.

  Mume alikomaa kutaka kujua ni nini kinaendeela lakini hakuambiwa kitu na mkewe wala shemeji yake (baba mtoto). Alijaribu kushirikisha wakwe ambao nao walipomhoji binti yao aligoma kueleza chochote. Inshu ilikuwa kubwa ikafika mahali mume mtu akamwambia mkewe, kama hasemi kitu arudi kwao, na yule dada akakubali bora arudi kwao kuliko aseme ile siri, tena akamuacha mwanae wa pekee aliyekuwa na miaka 2 tu kwa mumewe! Vikao vya familia upande wa mwanamke vilikaa na kuwashurutisha mtu na dada yake waeleze yanayomhusu yule mtoto, mama yake ni nani, lakini waligoma mwanzo mwisho, zaidi baba mtoto alipobanwa sana na maswali alikuwa analia...

  Yule mtoto alikua na shangazi yake ambaye aliikacha ndoa yake, akimwacha mumewe kulazimika kuoa mwanamke mwingine miaka minne baadae. Alipofika darasa la tano, yule mtoto alianza tabia ya uma.laya, akawa gumzo mtaani, hata walipopiga, na kuadhibu kwa namna yoyote, kesi za kukutwa na waume za hazikupungua kila kukicha pale kwa bibi yake alipokuwa analelewa na shangazi na bibi (Bagamoyo). Tabia mbovu ya yule mtoto ilisababisha ahamishwe shule mara kwa mara, na mara ya mwisho alikuja kuishia Dar kwa ndugu lakini alitoroka shule akiwa la saba, akatoroka home, akaingia mtaani na hajulikani anaishi wapi, wala anafanya kazi gani, japo mara kwa mara anaonekana kwa baba wakubwa, au kwa bibi yake, hasa wakati wa matukio kama ya msiba, lakini hasemi anakaa wapi wala anakula nini mtoto wa kike mwenye miaka 18 sasa, na haya maisha ameyaanza tangia akiwa na miaka 13!

  Cha kushangaza zaidi, hadi leo baba na shangazi yake yule mtoto hawajawahi kutoa details za yule mtoto...
   
 2. k

  kisukari JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,754
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  hii topic kwa kweli sijaielewa madhumini yake ni nini.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  tumieni condoms ,hamsikiii
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Madhumuni yake ni kustorisha... hahahah...
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Lakini Boss unadhani ni kitu gani kinaweza kufanya mtu na dada yake wafiche siri hivyo, kiasi cha dada kusacrifice ndoa?
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kubakwa na baba mzazi hivi
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  No, no... mtoto ni wa kaka mtu ambaye hajulikani wala hataki kusema alizaa na nani...

  Yani sawa na wewe Boss umzalishe mwanamke, then ukachukue kachanga ukapeleke kwa dada yako alafu wewe na dada hamtaki kutoa details za huyo mtoto kiasi kwamba dada anakuwa tayari kuiacha ndoa yake, kuliko akusemee siri yako... Umenipata?
   
 8. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh hata kama ni siri hyo imepitiliza
   
 9. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #9
  Oct 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndo maana nikasema ni too much... Watu walidhani labda huyo jamaa alizaa na ndugu akaona aibu, lakini ukoo mzima hakukuwa na historia ya kuwepo ndugu aliyekuwa na mimba wakati huo...
   
 10. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tunasubiri part 2 na labda 3.
   
 11. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Isidingo the need!!
   
 12. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  nimetoka mweupe,sijaelewa kitu hapa,hebu labda iwasilishwe kwa kanumba anaweza kuwa na la kuchangia.
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mtoa mada naomba uweke part two hadithi yako haijakaa sawa,fanua utafiti mwone yule dada
  akueleze kwa kina namtafute na huyo binti pia kisha uje utujuze yanayojiri
   
 14. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii story ya vitabu vya bulicheka uende ukamalizie mwenyewe jinsi unavyojua wewe...Au inamuhusu muhusika atuoneshe dada yake alivyokuwa jasiri na msiri.
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  so what!!! hadithi haina mashiko stahili and I dont know lengo la mleta hoja
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  ikifika kwa kanumba hii anafyatua movie yenye part 1 hadi 4, tena kila baada ya wiki 3.
   
 17. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  ndo tatizo la utajiri wa kiganga. Walidhani huyo mtoto atawaletea utajiri, ngoja sasa awaletee wajukuu
   
 18. VeronicaAmadu

  VeronicaAmadu Senior Member

  #18
  Oct 15, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  Labda kaka mtu alibaka kichaa.
   
 19. Raimundo

  Raimundo JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 13,552
  Likes Received: 10,940
  Trophy Points: 280
  Kuna thread nimeiona inazungumzia siri ambazo mtu kaahidi kufa nazo, huu ni mfano wake hivyo iunganishwe pamoja.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  heri ningeangalia kamba nyingine tu!
   
Loading...