Alietudanganya kuwa CHADEMA ni nguvu ya umma yuko wapi?

Pamoja na yote yanayotokea kwa mwenyekiti na chama kwa ujumla, lakini maisha mtaani yanaendelea kama kawa hakuna dalili ya kuyumbishwa. Nguvu ya umma yuko nayo Zuma tu peke yake.
Hapa Tz, kwani kuna binadamu?au misukule!!kiumbe hata kesho kiambiwe bei ya unga kilo moja ni 3000!!hakina habari??kinamuachia Mungu tu!!leo anakwenda hospital hata panadol hakuna lakini anafurahia kuambiwa kuwa kuanzia sasa muhimbili itakuwa hospital ya kwanza kumfanyia mgonjwa wa moyo bila upasuaji kwa nchi za Afrika Mashariki!!anashangiliiaaa!!sembuse kwenye mambo mazito kama hayo?
 
Utafiti ambao umefanyika ni watanzania wachache sana wanaofatilia siasa wengi wanafatilia wkt wa kampeni tu na jambo la kisiasa halina hisia sana kwa watanzania

Kitu pekee ambacho Serikali ya Tanzania ambacho siku wakijichanganya na ambacho kinaweza kuleta maandamano na hatari ya usalama kwa Tanzania ni mambo ya DINI au imani pekee si kitu kingine chochote
 
7+m wa wapi wewe..unafikiri kwa nini hawataki katiba mpya plus ACT na CUF mnan'goka usubuhi tu😂😁😂😁
Kwanza swala la katiba halipo kwenye ilani ya CCM, pili katiba iliyopo haina tatizo isipokuwa wanaotakiwa kufuata katiba ndio sometimes huwa na tatizo. Kama ww unaona katiba iliyopo ina tatizo basi tuwekee vifungu vitano hapa vyenye tatizo tuvisome na kuvichambua na pamoja, ili kila atakaesoma hapa mathalani wale wasiojua hayo matatizo ya katiba iliyopo wayaone kupitia comment yako, maana watanzania wa sasa sio wale wa mwaka 2008 ambapo walidanganywa kuwa Lowasa ni fisadi kwa lengo la kujenga chama, afu mwaka 2015 wakamtumia tena huyo huyo Lowasa kukibomoa chama. Nashauri swala la katiba liwekeni katika ilani yenu ya uchaguzi wa mwaka 2025 ili hao wananchi mnaosema wanataka katiba waweze kuwachagua sababu ya katiba mpya.
 
Utafiti ambao umefanyika ni watanzania wachache sana wanaofatilia siasa wengi wanafatilia wkt wa kampeni tu na jambo la kisiasa halina hisia sana kwa watanzania

Kitu pekee ambacho Serikali ya Tanzania ambacho siku wakijichanganya na ambacho kinaweza kuleta maandamano na hatari ya usalama kwa Tanzania ni mambo ya DINI au imani pekee si kitu kingine chochote
Kwa wanao amini dini, dini ni imani, dini ni roho na dini ni uhai. Hauwezi kufananisha dini na huu upuuzi unaoitwa siasa ambapo mtu mmoja anatumia ujinga wa wanachama wake kujinufaisha yey na familia yake.
 
Pamoja na yote yanayotokea kwa mwenyekiti na chama kwa ujumla, lakini maisha mtaani yanaendelea kama kawa hakuna dalili ya kuyumbishwa. Nguvu ya umma yuko nayo Zuma tu peke yake.
Kama siyo nguvu ya umma Mr Dudumizi . Mbona Ccm inawaogopa kwenye sanduku la kura mpaka wanaamua kupora mchakato wote ?!

Kama haina nguvu ya umma hofu ya Dola ni nini ?!
 
Kama siyo nguvu ya umma Mr Dudumizi . Mbona Ccm inawaogopa kwenye sanduku la kura mpaka wanaamua kupora mchakato wote ?!

Kama haina nguvu ya umma hofu ya Dola ni nini ?!
Una uhakika gani kama wameporwa mkuu? Au na ww umri wote huo umekubali kumezeshwa matango pori na hawa wachumia tumbo, waongo na wanafiki. Hivi mwamba viongozi vigeu geu na waongo wa aina hii kuna haja gani ya kuwaamini tena kwa lolote watakalosema?

images (7).jpeg

images (12).jpeg

images (10).jpeg
 
Ni muda mrefu sasa nimekuwa nikiwasoma CHADEMA...

Nimegundua kuwa NGUVU WANAYODAI KUWA NAYO haipo....haipo kabisaaa.....

Huku mitaani vijana wanaendelea KUBETI.....
Huku mitaani vijana tunaendelea kusebenza kutafuta CHAPAA ya dona la Kila siku......

Kiufupi WATU WAKO BIZE NA MAMBO YAO....

#TunaImaniNaSSH
#KaziInaendelea
 
Back
Top Bottom