Aliebuni wazo la vijana wa BAVICHA kwenda Dodoma Mungu ampe maisha marefu

Ya ccm waachie ccm wenyewe, hayakuhusu. Iwe 2016 au '17 ni mapenzi yao. Polisi hawawezi zuia mkutano wa uchaguzi iwe ccm, cuf, cdm nk. Mbona mnashindwa kuelewa jambo dogo kama hili? Hakika naunga mkono hatua zitakazochukuliwa na polisi.
Tatizo ni kwamba ni mkutano wa kisiasa, kwenye lile agizo la raisi hakuna kipengele kinachosema kwamba mikutano ya ndan ya kufanya uchaguz wa viongozi iliruhusiwa. Kwahiyo ni mikutano yote ilimradi tu ni ya kisiasa
 
is it unlawful for ccm to have a party chairman?
Having a chairman is not an issue here but convening unlawful meeting is. If they can have him without that unlawful meeting then it is okay or they should wait until those orders being terminated or they can challenge those decrees in the court but not to pretend as if they are bound with them.
 
Usijinyime raha kwa chuki zako za hovyo ambazo haziwezi hata kukuletea chakula mezani.Ushabiki wako wa kisiasa unaokupelekea kuwaona wenzako kama ni watu wa daraja la pili hauwezi kuwa na maana yoyote kwako zaidi ya kuiua dhamiri yako na kwa kuifanya ishindwe kuhisi uonevu wanaofanyiwa wanadamu wenzako.

Zaidi ya mara nne jeshi la polisi lilipiga marufuku mikusanyiko ya ndani iliyoandaliwa na vyama vya upinzani kwa malengo mbalimbali.Polisi walianza kuzuia kongamano la ndani lililokuwa limeandaliwa na Mh.Zitto Kabwe lililokuwa na lengo la kuijadili Bajeti ya 2016/2017.Kongamano hilo lilikuwa lifanyike katika ukumbi wa hotel moja hapa DSM,lakini policcm walizuia kufanyika kwa kongamano hilo.

Policcm pia walivamia na kuzuia mahafali ya CHASO kule Dodoma yaliyokuwa yameandaliwa katika ukumbi wa hotel.Polisi haohao walizuia kongamano la mbunge wa CHADEMA na vijana huko Bariadi lililopangwa kufanyika katika ukumbi wa kanisa LA KKKT Bariadi mjini,lengo likiwa ni kujadili changamoto za maendeleo yao,polisi kwa sababu ileile iliyozoeleka,walilizuia kongamano hilo.

Unaposema eti mkutano wa ccm ni mkutano wa ndani na haupaswi kuzuiliwa,hiyo "ndani" ni ndani gani?Ni ndani ya makaburi ya mlingotini kule Bagamoyo au ndani ya nini?Mbona wengine walipojaribu kufanya kile wanachotaka kukifanya ccm walisambaratishwa kwa Maji ya kuwasha,mabomu ya machozi na virungu?

Usifikiri tuliojipanga kwenda Dodoma kuzuia uvunjwaji wa kauli halali ya serikali ya ccm tunafanya hivyo kwa mizuka,tuna rejea za kutosha za namna jeshi la policcm lilivyotumika kutekeleza agizo ovu la kuzuia shughuli za kisiasa nchini,kwa kuwa mkutano wa ccm Dodoma ni shughuli ya kisiasa,tunaliomba jeshi la polisi liache Double standard,lisimamie maagizo ya serikali kwa kuwafurusha wanaCCM wote watakaoenda Dodoma,tena ikibidi wamvunje miguu au wamchomoe hata jicho Magufuli,hapo haendi kama Rais bali anaenda kama kada wa chama hivyo naye anapaswa atii bila shuruti agizo la Rais alilolitoa la kupiga marufuku mikutano ya kisiasa.

Polisi wakishindwa kumzuia Magufuli na genge lake lililojipanga kuikaidi amri ya mkuu wa nchi,ndipo BAVICHA tutakapoingilia kati kuudhibiti ukaidi wao dhidi ya mkuu wa nchi.
Hapo hamna hoja yenye mashiko ya kunishawishi.Mikutano yote uliyoitaja hapo juu haikuwa na nia njema kwa taarifa za kiintelejensia na ndio maana mikutani yenu yenye tija kama;Ule wa CHASSO karemjee na ule wa CHASSO iringa,polisi hawakushulika dhidi yao na badala yake waliimarisha ulinzi kama sheria ya kazi yao inavyowataka ili kuhakikisha mikutano inaisha salama.

Sasa unapokuja na hoja za mikutano yamakongamano skuelewi kabisa,na ccm hatufanyi mkutano wa kongamano bali tunafanya tu hivyo kwa mujibu wa katiba ya chama na c vinginevyo.
 
Ana akili sana sana.Hakuna maisha ya kutokuwepo kwa usawa na ukiukaji wa haki kiasi hiki.
 
Ile ya wapinzani ya ndani ya ukumbi ilikuwa ni disco sio mikutano ya chama yenye haki kisheria???
Ipi hiyo ww?Tunakutaka ututhibitishie uhalai wa mikutano hiyo na pia ni shiguli gani walipanga kufanya,ndipo ufananishe na huu wa ccm kama hutoona tofauti kubwa.

Siwakatazi kwenda dodoma,pengine labda mna makusudio ya kujitoa makafara kwa kuitafuta dola.Na hao viongozi waliojificha migongoni mwenu baadaye watajibu dhambi hiyo.

Polisi watafanya wajibu wao kama kawaida maana polisi wa nchi hii c wq chadema au chama chochote kile.
 
Wazo hili,bila kujali utekelezaji wake utakuwaje au nini kitatokea siku hiyo,ni wazo lililotoa funzo kubwa sana kwa wakubwa kuacha kujisahau na pia ni onyo kama sio ishara ya nini kinaweza kuja kutokea siku za usoni iwapo mambo haya yataendelea.

Nina amini asilimia mia moja kuwa wakubwa wenye dhama ya mambo fulani fulani katika nchi hii hawakutarajia kuwa kuna siku vijana wa Taifa hili wanaweza kufikia hatua ya kupanga au kuandaa movement ya aina hii kutokana na kauli zao.

Uliebuni wazo hili nakupongeza sana na mungu akupe maisha marefu maana naamini umewapa watu homework ya kutosha na huenda wakajifunza.

Hata hivyo,itakuwa ni busara zaidi kama wahusika wote watakaa pamoja katika meza ya mazungumzo kwa lengo kushauriani namna bora ya kumaliza jambo hili pasipo kuleta madhara yoyote na kila mtu akajiona ana haki na haki yake inalindwa.
Mungu yupi sasa? Maana ingekuwa wazo la kwenda nyumba za ibada hapo sawa
 
Having a chairman is not an issue here but convening unlawful meeting is. If they can have him without that unlawful meeting then it is okay or they should wait until those orders being terminated or they can challenge those decrees in the court but not to pretend as if they are bound with them.
contradictory..
 
Polisi jamii ...wanakwenda kuisaidia polisi na serikali kwa gharama zao wenyewe. Wapiga siasa kwenye professional wajue sasa kuwa siku zao zinaanza kuisha, ndio hapo mtu akijifanya mpuuzi nawe unakuwa mpuuzi zaidi yake!
 
inciting a crime is an offence punishable under our laws. you must be punished.
racism which ccm excises publicly is worse than inciting crime! it is my hope that multitudes and multitudes of Tanzanians will travel to Dodoma to show love to their country.
 
Back
Top Bottom