Alichosema Karugendo kwenye Raia Mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichosema Karugendo kwenye Raia Mwema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALEX PETER, Jun 15, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Baada ya vurugu za kuchoma makanisa kule Zanzibar, watu wengi wamekuwa wakiniomba niandike kitu juu ya matukio hayo. Jibu langu ni kwamba tumeandika mengi juu ya hatari ya kutanguliza udini. Tumeonya mara nyingi juu ya kuzikumbatia hizi dini za kigeni na kuweka pembeni umoja wetu wa kitaifa.

  Ninachokifanya kwenye makala hii, ni kuwakumbusha Watanzania kwamba yanayotokea sasa hivi tuliyatabiri na tunaendelea kuyatabiri. Kama tunataka amani ni lazima na ni muhimu kumtambua adui wetu wa umoja wa kitaifa.

  Hakuna taifa linaloweza kusimama bila ya kuwa na umoja wa kitaifa. Tanzania imesimama imara hadi leo hii kwa sababu ya umoja wa kitaifa uliojengwa na waasisi wake.

  Tunasifiwa kwa utulivu na amani. Sifa hizi ni za kweli na kilichotukifisha hapo ni umoja. Na hili halikunyesha tu kama mvua, ni jambo lilofanyiwa kazi usiku na mchana. Waasisi wa Taifa walijitahidi kujenga umoja.

  Kuna mengi yaliyowasaidia kujenga umoja huu: Tulikuwa na chama kimoja cha siasa. Chama kilitunga sera na kutoa visheni. Hivyo chama kilikuwa ni chombo kimojawapo cha kuujenga umoja wa taifa letu. Ingawa kulikuwa na watu wachache walioupinga mfumo wa chama kimoja, hawakuwa tishio la kuuvunja umoja wetu. Walikuwa wapinzani wenye kulenga kujenga umoja wa kitaifa.

  Waasisi hawakutanguliza dini zao, jambo la kuabudu lilibakia kuwa la mtu binafsi. Watanzania walikuwa na dini, lakini Tanzania, haikuwa na dini – haikutawaliwa kidini. Jambo hili lilionekana wazi katika katiba ya nchi yetu. Mwalimu Nyerere, alikuwa mcha Mungu na Mkatoliki hodari, lakini hakuthubutu kujenga nyumba ya ibada ndani ya Ikulu. Na Abeid Karume naye hakufanya hivyo.

  Ukabila ulipigwa vita na utawala wa machifu ulifutiliwa mbali. Kiswahili kilipewa kipaumbele na kuwa chombo cha kuwaunganisha Watanzania wote. Nchi ambazo zinatumia lugha za kigeni kama lugha zao za kitaifa, hadi leo zinapata shida ya kujenga umoja wa kitaifa.

  Ni watu wachache wanaozimudu lugha hizi za kigeni, walio wengi wanaendelea na lugha zao za kikabila jambo ambalo linafanya mawasiliano kuwa magumu. Mfano nchini Uganda, taarifa ya habari ili iwafikie wanachi wote inatangazwa kwenye lugha zaidi ya sita!

  Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa lengo la kuwakutanisha vijana waliomaliza kidato cha sita na vyuo wa Tanzania nzima. Kipindi chote cha mafunzo ya vijana hawa uzalendo na umoja wa kitaifa ni mambo yaliyosisitizwa. Mfumo huu ulipunguza kasi ya ukabila, kasi ya ukanda, majivuno na kiburi. Jeshi liliwatendea vijana wote sawa, bila ya kujali mtoto wa tajiri, kiongozi na mtoto wa masikini, wasichana wala wavulana.


  Mfumo wa elimu wa kuwasambaza vijana kwenye shule mbalimbali za mikoa ya Tanzania, ulisaidia kuwakutanisha vijana na kujenga umoja wa kitaifa.


  Mwenge wa huru ulibuniwa kwa malengo ya kujenga umoja wa kitaifa. Mbio za kuuzungusha Tanzania nzima, zilichochea cheche za umoja wa kitaifa.


  Mwaka 1995, Tanzania, ilijiingiza katika mfumo wa vyama vingi vya kisiasa.Tunayoyashuhudia sasa hivi hakuna chama kinachoonyesha sera ya kujenga umoja wa kitaifa. Wapinzani wa leo ni tofauti kabisa na wapinzani wa zamani wakati wa utawala wa chama kimoja.

  Wapinzani wa leo pamoja na chama tawala cha CCM, wanaangalia zaidi umoja wa vyama vyao kuliko umoja wa kitaifa, wanatanguliza kuingia Ikulu, ruzuku, mbwembwe za madaraka na ushindani wa chuki na utengano. Wakati wanasiasa wa zamani walikuwa na sera ya uhuru na umoja, wanasiasa wetu wa leo wana sera ya ukoloni mambo leo (Utandawazi, ubinafsishaji, soko huria) na utengano.

  Katika awamu ya pili tumeshuhudia baadhi ya viongozi wa ngazi za juu serikalini kuanzisha mtindo wa kujenga nyumba za ibada katika ofisi za serikali. Uteuzi wa viongozi kufuatana na dini zao. Dini ilianza kutangulizwa. Waheshimiwa wengine walianza kubadilisha dini zao kwa siri. Malumbano kati ya Waislamu na Wakristu yalishika kasi. Magomvi yalizuka kati ya Waislamu na Wakristu.

  Mfumo wa elimu umevurugika, shule nyingi za binafsi zimeanzishwa na kuchochea watoto wengi wasiweze kuivuka mikoa yao. Watoto wa matajiri hawasomi tena na watoto wa masikini. Kiwango cha elimu kimeanza kutofautiana na kuleta hatari ya kuaanza kuunda tabaka katika Taifa. Tabaka ni aduni mkubwa wa umoja na amani.

  Baadhi ya watoto wameanza kuvuka mipaka ya nchi na kusomea Uganda, Kenya na nchi nyingine jirani kama Zambia na Malawi. Hii haiwezi kusaidia kujenga umoja wa kitaifa. Maana watoto hawa itakuwa vigumu kulelewa katika misingi ya utamaduni wa Mtanzania.

  Jeshi la Kujenga Taifa limefutwa na Mwenge wa Uhuru kimekuwa chombo cha kampeni! Badala ya kueneza amani katika taifa letu, Mwenge, wa huru umegeuka na kuwa chombo cha kusambaza virusi vya UKIMWI.Kila mwengi unapopita unaacha nyuma yake kumbukumbu ya watu kubakwa, ndoa kuvunjika, watu kufa na vitendo vingine vya kusambaza virusi vya UKIMWI.

  Mfumo uliokuwa umejengwa na waasisi wetu wa kuunda umoja wa kitaifa umeaanza kupotea! Ni wajibu wa kila Mtanzania kujiiuliza: Ni nani adui wa umoja wetu? Kama nilivyosema hapo juu, ni vigumu taifa lolote kusimama bila ya umoja. Kama tunataka Taifa letu liendelee kusimama ni lazima kujenga umoja.

  Tukigundua adui wa umoja wetu ni lazima tumpige vita kwa nguvu zetu zote. Kati ya mambo ambayo yanaonyesha dalili za kutishia uhai wa umoja wetu ni dini! Na hasa hizi dini mbili kubwa: Uisilamu na Ukristu.

  Pengine ili kuweka hoja sawa nitoe nukuu ya mteolojia mmoja wa Brazil, Leonard Boff aliyekuwa padri mtawa wa Kanisa Katoliki, aliyepambana na mifumo ya kanisa iliyokuwa inafumbia macho unyanyasaji, ukiukwaji wa haki za binadamu, uvunjaji wa umoja wa kitaifa, hadi akalazimishwa na utawala kuacha huduma ya upadri.

  Mteolojia huyu aliishia kufundisha kwenye vyuo vikuu nchini Brazil na kuunda jumuiya ndogo ndogoza Kikristu.

  Alipata kusema Boff: “ Kueneza Injili hakuna maana ya kueneza mifumo ya Ukristu. Kueneza Injili maana yake ni kuishi pamoja kama dada na kaka, kushirikiana katika kazi, kuwajibika kwa upendo katika maisha ya watu wengine, kuheshimu utamaduni, mila na desturi za watu wengine, maana kila utamaduni umejaa ukweli wa milele.

  Kueneza Injili maana yake ni: kuishi, kulia, kucheka, kufanya kazi na kujiingiza kikamilifu katika maisha ya watu wengine ili sote kwa pamoja tupate wokovu” (kutoka kwenye sinema ya “On the Way Together.” Tafsiri ni yangu).

  Pale niliposema “Kueneza Injili”, unaweza kuweka neno “Kueneza imani mpya kwa watu wengine”. Nikiangalia hali ya sasa hivi ya nchi yetu ninashawishika kukubaliana na maneno ya Leonard Boff.

  Bahati nzuri tuliyo nayo ni kwamba hata mfumo wa vyama vingi umeanza chini ya uongozi wa waasisi ndiyo maana hakuna vyama vya kisiasa vya kidini.

  Lakini tunakoelekea jambo hili litakuja tu! Kama tumeanza kujiuliza rais anatoka dini gani, utafika wakati wa kujiuliza rais anatoka kwenye chama cha dini gani. Kuna nchi ambazo zina vyama vya kidini. Ili uwe mwanachama ni lazima uwe mfuasi wa dini au dhehebu fulani.

  Nchi hizi hazisifiki kwa umoja wa kitaifa. Mfano nchini Uganda, kuna chama ambacho ili uwe mwanachama ni lazima uwe Anglikana na kingine ni lazima uwe Mkatoliki na kingine mwislamu au dini ya kujitegemea kama ya Joseph Konny.

  Chimbuko la tatizo ni wale walioneza imani hizi za kigeni katika nchi za Afrika. Badala ya kueneza imani walieneza mifumo ya dini zao. Na kila dini ilishikilia kuwa ndiyo yenye wokovu na malengo hayakuwa ya kuishi kama dada na kaka, bali bwana na mtwana!

  Hakukuwa na ushirikiano katika kazi za kila siku wakati wa kueneza dini hizi za kigeni wala uwajibikaji wa wageni katika maisha ya watu wenyeji. Historia inatueleza jinsi Ukristu na Uislamu zilivyoenea duniani kote kwa upanga, chuki na ubaguzi. Dini hizi zilifuta utamaduni, mila na desturi za watu wengine. Dini hizi hazikucheka na wanaocheka na wala hazikulia na wanaolia. Hazikujiingiza kikamilifu katika maisha ya watu wengine ili watu wote wapate wokovu. Aliyezikumbatia dini hizi alipokewa kwa mikono miwili, aliyezikataa alilaaniwa na wakati mwingine kuuawa!

  Watanzania wengi wamejiingiza kwenye dini hizi mbili. Ni vigumu kuwambia wazikimbie maana zinahatarisha umoja wa Taifa. Ushauri wa pekee ni kuzilazimisha dini hizi zikakubali utamaduni wetu. Waasisi walitujengea utamaduni wa umoja, utulivu na amani, hivyo ni lazima dini zetu ziheshimu utamaduni huu. Mtanzania Mwislamu ni Mtanzania, na ni lazima apate haki zote za Mtanzania. Aheshimiwe na Watanzania wote kufuatana na karama zake alizonazo na mchango wake kwa Taifa.

  Mtanzania Mkristu ni Matanzania na ni lazima apate haki zote za Mtanzania, aheshimiwe na Watanzania wote kufuatana na karama zake na mchango wake kwa Taifa.

  Mtanzania anayefuata dini za jadi ni Mtanzania na ni lazima apate haki zote za Mtanzania, aheshimiwe na Watanzania wote kufuatana na karama zake na mchango wake katika taifa letu.

  Wale wanaoiona hatari iliyombele yetu ya kuuvunja umoja wetu, na hasa hatari ya dini za kigeni, ni lazima wafikirie kwa haraka jinsi ya kuunda chombo cha kujenga umoja wa kitaifa.

  Nilivyodokeza hapo juu vyama vya kisiasa tulivyonavyo kwa sasa haviwezi kujenga umoja wa kaitaifa. Dini za kigeni ni adui mkubwa wa umoja wetu. Mifumo mingine imeharibiwa makusudi! Kiundwe sasa chombo cha kujenga umoja wa kaitaifa. Chombo ambacho hakitatawaliwa na vyama vya kisiasa, dini, matajiri, wawekezaji au ushawishi na nguvu kutoka nje ya nchi, ukabila wala ukanda .

  Chombo cha kujengwa na Watanzania wenyewe na wala si chombo cha kujengwa na Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika. Chombo ambacho kitamfanya kila Mtanzania kumthamini Mtanzania mwenzake si kwa vile ni wa chama fulani, dini fulani au kabila fulani, bali kwa vile ni Mtanzania.

  Kuna tetesi kwamba sasa Wakristu wanaomba na kusali kwa nguvu zote ili Tanzania isitawaliwe na rais Mwislamu tena, na Waislamu wanaswali kwa juhudi ili Tanzania, isitawaliwe tena na rais Mkristu!

  Kwa vile tumezoea kutawaliwa na unafiki, mambo haya yasemwi na kuonyeshwa wazi – ni agenda za siri ambazo kila kikundi kinazitunza kwa uaminifu mkubwa.

  Mwelekeo huu si wa umoja na wala si wa kujenga amani. Mwelekeo mzuri ni wa kumtambua adui wetu wa umoja wa kitaifa na kupambana naye kwa nguvu zetu zote!
   
 2. U

  Umsolopogas JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 256
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimesoma mistari mitatu ya article ya huyu mheshimiwa nikaboreka kabla sijaendelea. Dini za kigeni? sijamuelewa. Kwa sababu kama nimemuelewa sawasawa ina maana anadai kuwa matatizo yetu tuliyo nayo yameletwa na hizo dini za kigeni?

  Naomba mu-refresh memory yangu kidogo. Huyo ndiye yule padre alifukuzwa na kanisa katoriki? No wonder. Lakini ninachotaka kusema kama huyo Ex-padre anahusisha matatizo yetu na hizo anazoziita dini za kigeni, basi ana mtndikikio wa akiri. Ingawa naweza kukiri kuwa ni mwandishi mzuri na anaweza kuvuta hisia za watu wengi.

  Ushauri wangu wa bure. Karugendo, concentrate na maendeleo ya watu na huduma zao. Achana na dini au imani za watu. Kwa sababu hata kama una abudu mti au jua, utakuwa na matatizo yaleyale ya mtu anayeabudu, Mungu, Kristo, budha na wengineo.

  Kwa nini hamuuwezi kujenga hoja bila kuhusisha imani za watu?


  Ninavyofahamu mimi mtakufa kifo kile kile cha Karl Max, Lenin, Mao na wengine wengi waliojitahidi kufuta imani hizo hizo mna zipiga vita kwenye akiri za watu. Na bado zinazidi kuota mizizi na kuchipua kwenye mioyo ya watu.
   
 3. Chambo81

  Chambo81 JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kalugendo umeshasema UKWELI kuhusu KUELEWEKA its non of your bussness!!!!!
   
 4. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  hata mm nilipofika hapo tu "kuzikumbatia hizi dini za kigeni" kanikata appetite yote nikaachana nae
   
 5. Capital

  Capital JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,036
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mie naunga mkono hoja ya kalugendo. Siyo siri dini za kigeni zimechangia sana kumomonyolewa kwa tamaduni na falme mbalimbali hapa duniani, hususan watu weusi. Ilifikia mahali wenye dini hizo walitumia nguvu za kijeshi (kivita) ili dini zao zikubalike mfano waislam walipigana jihadi ili kuwaslimisha kwa nguvu wasio waislam hali kadhalika wakristo, japo wao walitumia mbinu nyingi ikiwemo covert wars (vita ya kujificha) rejea vita ya vietnam kwa mfano. Ni vigumu sana kuimarisha umoja wa kitaifa katika mazingira ambamo wananchi wana imani za kidini, ambazo msingi wake ni kuwa wale wasioamini usichokiamini siyo wenzako, wanakosea na hawafai kuwa watu. Ndio maana nchi kama china ikaamuwa kutotambua dini yoyote isipokuwa dini zake za asili. Ile nchi imekuwa stable kwa miaka mingi sana na sasa ni matajiri. Wale wanaobakia kuamini mambo wasiyoyafahamu vema kama watanzania na watu wengine wa chini, wamebakia maskini, wasio na utamaduni, mila na utambulisho, pia wasio na umuhimu katika dunia hii. Mtu kama kalugendo anafaham vema chimbuko la haya mambo yote, mambo ya dini ambayo watu wengi wanayafuata katika hali ya giza, bila kufahamu maana yake. Mtu anadhani ni dhambi (kulingana na mafundisho ya dini za kigeni) kuhoji uhalali au falsafa ya hizo dini.

  Waislamu eti wao hawataki kushiriki katika mchakato wa sensa eti hakuna kipengele cha kutambua idadi yao ni wangapi. Hakuna hoja mfu kama ya hawa jamaa. Yaani nchii hii ina wapumbavu sijapata ona. Ukiwa muislamu au mkristo... So what?

  Ushauri--- watu wasiamini kwa kufuata mkumbo, kupelekwa tu kama mang'ombe yanaswagwa pale pugu mnadani. Hizi dini zilikuja kutufanya sisi malofa, tuwaamini wageni na tuwasifu, tuwaogope (kwa mfano hakuna mtu kuhoji uwezo wa kasisi kukuondolea dhambi) na kisha wachukuwe vyetu. Na kusudi waendelee kuchukuwa vyetu, ilibidi tuendelee kugawanyika katika makundi madogo madogo ya kidini (sectarian) (divide and rule).

  Wenye akili na watambue

  capital
   
 6. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  yuko sahihi sana. Hapa history ni muhimu sana nadhani.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ahali yangu Padre Privatus Karugendo, kijana wa Karagwe
  Naona hapa Imekupuruchuka. Ni vizuri kabla kuandika mada yako hii ambayo mwenyewe umeioana kuwa ni Adhimu ungepitia na kudurusu vitabu vifuatavyo.
  1.Kitabu cha Jan P van Bergen katika kitabu chake, Development and Religion in Tanzania,
  2. Kitabu cha Padre mwenzako Dr John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985 .

   
Loading...