Alichosema jushua nassari kuhusu bajeti ya mwaka huu

ALEX PETER

Senior Member
Jan 17, 2012
117
23
[h=6] 268525_10150281205532938_5894563_n.jpg
Bajeti ya Mwaka huu 2012/2013 ni Bajeti ya Madeni

Serikali inapendekeza Bajeti ya TZS 15 trilioni(USD 8.75 Billion) katika mwaka 2012/13. Uchambuzi wa vitabu vya Bajeti unaonesha kwamba mafungu ya juu 5 kwenye Bajeti ni Kama ifuatavyo;

1 Huduma kwa Deni la Taifa Tshs 2.7 trilioni(USD 1.69 Billion)
2 Wizara ya Ujenzi. Tshs 1 trilioni (USD 625 Million)
3 Wizara ya Ulinzi Tshs 920 bilioni (USD 575 Million)
4 Wizara ya Elimu Tshs 721 bilioni (USD 451 Million)
5 Wizara ya Nishati na Madini Tshs 641 bilioni (USD 400 Million)
TOTAL TZS 5.982 Trilioni(USD 3.74 Billlion)
Chanzo: Vitabu vya Bajeti kwa Wabunge

Jumla ya mafungu haya ni sawa na asilimia 40% ya Bajeti. Kwa hiyo asilimia 40% ya Bajeti yote imepangwa kwa mafungu 5 tu. Fungu lenye kiwango kikubwa zaidi ya Bajeti kuliko vyote ni fungu 22 ambalo ni malipo kwa Deni la Taifa. Pia sehemu kubwa ya fedha zilizotengwa kwa Ujenzi na Nishati ni madeni kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya miaka ya nyuma.

Hii yaweza kuwa Bajeti ya kulipa madeni zaidi kuliko Bajeti ya kuchochea maendeleo. Bajeti hii pia yaweza pia kuwa ni Bajeti ya kukopa maana jumla ya TZS 5.1 trilioni(USD 3.19 Billion) zitachukuliwa kama mikopo kwa Serikali. Mikopo ya kibiashara ambayo ni mikopo ghali sana itachukuliwa kwa wingi zaidi kuliko mwaka wa fedha uliopita.

Wabunge wanapaswa kufanya uchambuzi zaidi wa Bajeti ya mwaka huu inayopendekezwa na Serikali. Kuna haja kubwa sana ya kuharakisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Bajeti katika Bunge na Kamati ya Bunge ya Bajeti ili kuweza kufuatilia kwa karibu, kuchunguza na kutoa taarifa kwa wabunge ili kuwezesha kuboresha Bajeti.

Misamaha yote ya Kodi na Madeni yote ambayo Serikali inaingia inabidi sasa ithibitishwe na Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ili kuongeza udhibiti na usimamizi wa Misamaha ya Kodi na pia Deni la Taifa.[/h]
SOURCE: ukurasa wake wa facebook
 
Kazi ipo! kama budget ni ya kulipa madeni!! wakati wa mkapa si ilisemekana madeni yote yalilipwa? sasa haya mengine makubwa hivi yalikupwa kufanyia nini?? wizara ya Ulinzi inatengewa pesa nyingi hivo kwa nini? kuna vita? Kilimo ambacho kinaajiri watanzania zaidi ya 70% mbona hakionekani kwenye top 4? kilimo kwanza kimekufa au ilikuwa political slogan tuu??
 
Kila mwaka mwaka una kipau mbele chake bila kujali kipau mbele kilichopita kilifanikiwa kwa asilimia ngapi.Mbona watawala mnafanya mchezo mchafu katika maisha ya Watanzania?
 
CCM HAWAACHI KUOTA MCHANA KWEUPE,KATIKA KAMPENI ZAO ZA KUWAPUUZA WATANZANIA WAMEANDAA ULAGHAI MWINGINE ILI WAPATE KURA ZA WAPUMBAVU.
1.KUANZISHWA BENKI YA WAKULIMA
2.KUANZISHA BENKI YA VIJANA
KATIKA UANZISHWAJI BENKI HIZO SERIKALI INA MPANGO WA KUWAHADAA WATZ KWA KUWAAMBIA WATAWAKOPESHA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU,KUANZIA MILLION 1MPAKA 15.LAKINI KATIKA UOMBAJI HUO UNAHUSISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KAMA MAWAKALA WAO ILI UPATE MKOPO,CHA KUCHEKESHA ZAIDI INAAMINIKA CCM IMEJIPANGA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA URAIA NA HASA CHA KUPIGIA KURA KAMA MTAJI WA KUWAPATA HAO WALENGWA.NA KUHAKIKISHA WANAOCHUKUA MIKOPO WOTE WATAIPIGIA CCM UCHAGUZI KUANZIA UDIWANI WA 2014 NA UCHAGUZI MKUU 2015.LAKINI WAJUMBE WENGI WANA WASIWASI KUWA VIJANA WALIO WENGI WAMEELEVUKA SANA NA WATAKULA PESA ZAO NA KUWAPIGIA WAPINZANI.CCM ILITUMIA MKUTANO WA JANGWANI KAMA KIPIMA JOTO SASA WAMEANZA KUINGIWA NA WASIWASI MAANA MKUSANYIKO ULE HAUKUKAMILIKA BILA YA PESA SASA WANAJIULIZA BILA VIKINDI VYA SANAA KWELI WATAKUBALIKA,MJUMBE ALIYE KARIBU NA NAPE KASEMA CHADEMA INAWANYIMA USINGIZI KULIKO HATA MAGONJWA YA WAZAZI WAO AU WANANDOA WAO.
BINTI MREMBO LUMUMBA CCM
:confused2:
 
Kazi ipo! kama budget ni ya kulipa madeni!! wakati wa mkapa si ilisemekana madeni yote yalilipwa? sasa haya mengine makubwa hivi yalikupwa kufanyia nini?? wizara ya Ulinzi inatengewa pesa nyingi hivo kwa nini? kuna vita? Kilimo ambacho kinaajiri watanzania zaidi ya 70% mbona hakionekani kwenye top 4? kilimo kwanza kimekufa au ilikuwa political slogan tuu??
Hilo swali kwenye RED nilijiuliza sana lakini sikujipatia jibu, ngoja tuambiwe
 
Kazi ipo! kama budget ni ya kulipa madeni!! wakati wa mkapa si ilisemekana madeni yote yalilipwa? sasa haya mengine makubwa hivi yalikupwa kufanyia nini?? wizara ya Ulinzi inatengewa pesa nyingi hivo kwa nini? kuna vita? Kilimo ambacho kinaajiri watanzania zaidi ya 70% mbona hakionekani kwenye top 4? kilimo kwanza kimekufa au ilikuwa political slogan tuu??
hata kama Mkapa angeacha deni la 0, safari peke yake zinatosha kufanya deni liwe juu sana, ukijumlisha na mengine! ......
 
Back
Top Bottom