Alichosema jana mgombea ubunge wa chadema jimbo la temeke hakistahili . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichosema jana mgombea ubunge wa chadema jimbo la temeke hakistahili .

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by babayah67, Oct 27, 2010.

 1. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jana nilipata bahati ya kuusikiliza mkutano wa Dr Slaa uliofanyika katika viwanja vya MwembeYanga. Mkutano ulianza vizuri na wote waliopata nafasi ya kuzungumza walizungumza kwa ufanisi mzuri saana HADI pale ilipobaki dakika tano za mwisho. Zilipobaki dakika tano za mwisho Dr Slaa aliwaoomba wagombea ubunge wa majimbo mbalimbali ya mkoa wa Dar wasimame kuwasalimia wananchi na kuwaomba kura zao. Wagombea ubunge wa majimbo ya Ubungo, Ukonga, Kinyerezi na Kigamboni, walisimama na kila mmoja aliutumia muda wake vizuri saana kuhamasisha watu na kuwaomba kura zao ziende kwa Dr Slaa. Ilipofika zamu ya mgombea ubunge kwa jimbo la Temeke, alianza kuongea mambo ambayo nahisi hata Dr Slaa yalimkwaza. Huyu bwana alianza kwa kumshambulia JK moja kwa moja kwa kusema kuwa yote mabaya yanayofanywa na JK yanatokana na kuwa hakufunzwa vizuri na mama yake. Na akatumia hata methali isemayo asofunzwa na wazazi hufunzwa na ulimwengu. Kwa mtazamo wangu naona huyu mgombea hakumtendea haki JK na hasa Mama yake kwa kumjumlisha katika masuala ambayo huyo mama hahusiki katika masuala ya kisiasa ya mwanae. Nisingempinga kama angemtukana JK bila kumhusisha mama yake. NDIO MAANA NINA WASIWASI HUENDA HUYU JAMAA AKAWA SI CHADEMA KINDAKINDAKI, ASIJE AKAWA NA LENGO LA KUVURUGA USHINDI WA CHADEMA DAR na TZ Kwa ujumla.
   
 2. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lets call a spade spade and not big spoon. Mi pia sikufurahishwa kabisa na kauli hiyo. Inamfanya mtu mzima makini afikirie hawa ni wahuni. Nashauri mambo ya jinsi hii Mhe: Rais Dr Slaa ayakemee hadharani ili vijana wake waogope na kuwa na adabu right from day one.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Umeisha wahi msikia Makamba akiongea? Hizi ni kampeni wacha watafute udhaifu wa JK
   
 4. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,554
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Provocation, name calling, kejeli etc. ni part ya campaign, Mbona CCM wanafanya hilo sana!! sidhani kama hiyo ni tatizo especially wakati huu wa kampeni, kwa wakati mwingine sawa.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yea that is what they call politics!
   
 6. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  waache wanasiasa waparurane, Grand Finale ni Oct 31st, then tunaendelea na kazi kama kawaida
   
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Mtu anayedanganya wazee na vijana na kuendeleza kuwadanganya kila siku anawavunjia heshima,usahihi ni kuwa mtu huyo hana adabu kwa wazee wake. kumwambia mtu huna adabu hujamtukana ila unamkumbusha awe na adabu. Alichosema hakukosea ila alitamka kwa ukali mno.
   
 8. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Binafsi pia sikufurahishwa na hilo na kumuingiza mama mzazi wa mgombea katika kampeni.
   
 9. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa, kwani kikwete kafunzwa na mamaye ufisadi wote aloufanya?
   
 10. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hapa ndio huwa nakoma na WANA UKOMBOZI wetu....Yaani kwa kuwa CCM nao pia wanafanya haya hivyo ni sawa tu hao tunaowapigia debe kututoa hapa tulipo nao wafanye kama wanayoyafanya CCM?

  Lakini pia kama anavyosema mwanzisha mada hii, alichokifanya yule mgombea wa Chadema Temeke ambacho kimeangaliwa live na mamilioni ya watanzania hakijawasaidia bali kimewaharibia sana CHADEMA.

  Mimi binafsi nimeshuhudia mtu mmoja mashuhuri ambaye daima amekuwa akiwaheshimu viongozi wa vyama vyote na hata kuwa karibu nao sana alivyokereka baada ya kumskiliza Dr Slaa na kufuatiwa na yule mgombea. Kwa kweli kumjua kwangu kote mtu huyo sijawahi kumuona so dissapointed kama jana baada ya kuacha mambo yake muhimu kukaa kufuatilia mkutano ule na kushuhudia matusi na lugha za ajabu kama zilizotolewa jana.

  Mama yangu Mzazi ambaye miaka yote anaamini kuwa mimi ni CHADEMA na alikuwa mshabiki mubwa wa Dr Slaa leo mchana amenipigia simu kuniambia kuwa hataki hata kuona sura ya Dr Slaa anayodai imekuwa mbaya kutokana na lugha ya matusi na chuki anayoendelea kuitoa.

  Mama yangu anachukia siasa lakini kwa miaka mingi yeye ndiye amekuwa akinipa taarifa za kila issue anayorusha Dr Slaa bungeni na alikuwa hakosi kufuatilia vikao vya bunge aongeapo mwanawe mpendwa Zitto na Dr Slaa lakini sio wengine. Leo ananipigia simu kuniambia amesikia Zitto anakuja na Dr Slaa katika jimbo lake na kunishauri nimshauri Zitto asiende huko na kuwa yeye alikuwa na hamu ya kuhudhuria mkutano wa CHADEMA lakini sasa hataki kusikia kuhusu chama hicho.

  Hizi ni feedback mbili tu ambazo nimezipata live kutokana na lugha iliyotumika jana katika mkutano wa pale Mwembe yanga.

  Nadhani kuna lidudu baya limeingia CHADEMA na nina wasiwasi dudu hilo linaitwa MABERE MARANDO.....
   
 11. N

  Ngoni Member

  #11
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiasi napata ugumu fulani kumsapoti huyu mgombea wa ubunge, Lakini LABDA mama yake Kikwete anaweza kuwa ameingizwa kwenye hizi kampeni kutokana na lile bango ambalo anaonekana amekaa na mwanaye huku likisomeka 'mapenzi ya mama kwa mtoto'. JUST THINKING ALOUD!!!
   
 12. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mnanikumbusha article ya Generali Ulimwengu-Kukosa haya huzaa aibu na mwishowe Hatari.....jikumbushe hapo chini
  "
  Inaelekea kila tunapomwona mwenzetu ana dalili za kupata kichaa, kavua nguo na kuingia mtaani, tumesahau kwamba tunachotakiwa kufanya ni kumkamata na kumrejesha ndani, kumfunga kamba na kumtafutia matibabu mwafaka.
  Badala ya kufanya hivyo, nasi tunavua nguo zetu na kumfuata huko huko mtaani tukiwa kama yeye. Ndiyo maana nasema tena, kwamba nchi hii inaanza kuonekana kama kijiji kisichokuwa na wazee, ambao watoto ndio wanaendesha mambo, lakini watoto wenyewe ndio hao hao waliotakiwa kuwa wazee wa kijiji chetu. Tutakuwa wageni wa nani"
   
 13. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ukielezea sera yako vizuri wananchi watakuelewa hauhitaji kutukana.
  Sio CCM wala CHADEMA wala nani anatakiwa kumtukana mtu mwingine.
  Hiyo ya jana na wengine wanaotukana wanaonyesha kukosa maadili na ustaarabu, I also didnt like that.
   
 14. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Wewe hujamsikia JK akisema "CHADEMA wana hubiri kumwaga damu?"

  Hiyo nayo si kweli, kwa nini sisi Chadema hatulalamiki?

  Toa upupu!!
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Not unexpected from you! HATUDANGANYIKI nenda kawaambie
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa upande mmoja mama yake JK hahusiki katika ulingo wa siasa, Lakini kwa upande wa pili kwani ni nani mwenye jukumu la kumfundisha adabu mwanaye?
   
 17. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hata mimi sijaexpect wewe kuelewa busara ya siasa za adabu na ustaarabu...lakini najua wapiga kura wa Tanzania mnaowaita mbumbumbu akiwemo mama yangu wanaelewa sana uzito wa busara hizo...sasa kama unadhani kuna mtu anaweza kuchukua nchi hii kwa kura za watu wa aina yako mliojawa na chuki na hulka ya magomvi, then nawatakia mafanikio mema hiyo jumapili...
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Siku zote inajulikana wewe na familia yako ni ccm damu damu, kwamba mama yako hataki kuwaona zitto kabwe na "mwanae Dr. Slaa" sio habari kabisa, kwani kwa mantiki ya kilichotokea jana, hakuna jambo jipya alilozungumza Dr.Slaa linalomhusu jk. Yote aliyoyasema jana ameyasema kila mahala alipokwenda tangu kampeni zimeanza. Ukiacha sera ya usalama ambayo aliizungumzia jana kwa mara ya kwanza mengine yote yalikuwa ni marudio tu. Alizungumzia pia ufisadi uliofanywa na ccm kwenye ujenzi wa matundu ya vyoo vya shule bagamoyo, na inajulikana kwamba alishamtaja jk kwenye list of shame tangu 2007 sasa utaona kuwa mama yako sio mkweli ama la unausemea moyo wa mama!
   
 19. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Omar

  Not sure kama unamchango wowote umeufanya kwa hii Tanzania, kama unafanya basi unatupigisha "maktyme"!

  Please vote for CCM as usual.
   
 20. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  Ni mambo ya kawaida katika politics na sidhani kama alimgusa mama ya kikwete directly. Hapa alikuwa anamuelezea kikwete na si mama yake kikwete. Kwani hakufika kuelezea tabia za mamaake na kikwete bali alimuelezea kikwete mwenyewe. Ni hali ya kawaida katika siasa ila kama angekuwa anamuelezea mama ya kikwete jukwaani ni kosa. Inakuaje mtu anapomgusa mke wa Dr slaa, ikiwa huyo mke agombei hata ubalozi wa nyumba kumi? Nafikiri bado tujafika mahali pa kulaumu chama au mtu binafsi, mambo ya ngoswe mwachie ngoswe mwenyewe. Asanteni.
   
Loading...