Alichosema Anthony Diallo kinasemwa na Watanzania wengi chinichini

Katiba yetu inalalamikiwa na Watanzania wote, wapinzani, wanaCCM na wazanzibar kwakuwa katiba hii pamoja na mambo mengine ina uwezo mkubwa wa kuzaa kiongozi dikteta, kiongozi mwizi wa kura, kiongozi mdini, kiongozi mbadhilifu, kiongozi mkabila na kiongozi kichaa ambaye wananchi hawawezi kumdhibiti.

Katiba hii ni tamu sana kwa wanasiasa walioko madarakani tu basi kwakuwa inawaruhusu kuwa chochote bila bugudha.

Tulitegemea Katiba mpya iwe kipaumbele cha awamu ya sita ndani ya mwaka mmoja tu wa kuingia madarakani. Lakini ona, utamu wa katiba hii hata awamu ya sita sio kipaumbele chao kuandika katiba mpya.

Diallo ni speaker tu lakini microphone wanayo Watanzania wote na wana CCM wenyewe. Kumlaumu Diallo ni kupteza shabaha.

Ni heri kusoma alama za nyakati kuliko nyakati zisome alama zetu. Kuna siku watu watalaumiana kwa kutofanya maamuzi mapema.
Kwamba anaomba Radhi alieleweka vibaya ndio ilikuwa kauli yake ya mwisho
 
Umenikumbusha kiongozi kijana anakwambia usipokubali ongezeko la tozo hamia Burundi
Ni wale ambao hawakustahili kupewa dhamani ya kuwaongozo wananchi,, huwezi kuniambia eti kama hamtaki hamia Burundi,, ni upumbavu wa hali juu kama kiongozi hupaswi kuongea maneno kama hayo kwa wananchi wako,, inatakiwa uwape njia mbadala au lugha tamu na laini bila kusahau kuwaelimisha
 
Sera nying hapa Tanzania hazifanikiwa kwasababu siyo shirikishi halafu hazina muongozo maalumu zingine hutumia sheria za zamani 'established without guiding principles and participation'
 
Back
Top Bottom