Alichonukuliwa January Makamba kuhusu "sitting allowance" tarehe 6 Februari, 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichonukuliwa January Makamba kuhusu "sitting allowance" tarehe 6 Februari, 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamisaa, Jun 21, 2011.

 1. Kamisaa

  Kamisaa Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeurudia kuutazama tena ule mkanda wa "Letter to my Fathers" ili kutafuta nukuu ya alichokisema January Makamba kuhusu "sitting allowance" tarehe 6 Februari, 2011...

  "Today we had orientation for new members of parliament at Ubungo Plaza. And eh... we are getting paid, fortunately (laughter). And eh... its called a sitting allowance. I think they should change. We can't be paid... we can't be given an allowance by "sitting". Its embarrassing... to say that you received an allowance by sitting"...

  Nukuu ni kutoka dakika ya 0.59 mpaka 1.55...

  YouTube - ‪"Letter to My Fathers" - Poem by January Makamba‬‏My take:

  Zitto alikaririwa kule Twitter akisema kwamba hoja ya "sitting allowance" ni hoja aliyoianzisha siku za karibuni na January Makamba. Akasema pia kwamba amesikia "sitting allowance" zimefutwa ndani ya vikao vya sekretarieti ya CCM kwa ushawishi wa Makamba Junior. Sasa imekuwaje hii hoja ya posho imeishia kuwa ya kisiasa ya upande mmoja tu wakati hata wana CCM wenye nguvu wanaikubali? Kwanini haikuwa hekima kwa CHADEMA kujenga consensus na wabunge wa CCM ambao nao ni wazi wanakubaliana na kufutwa kwa "sitting allowance"? Badala yake leo hii, hoja ya posho ya sitting allowance imegeuzwa-geuzwa kisiasa kupitia matamko ya CHADEMA na magazetini yanayowaunga mkono kuwa ni hoja ya kupinga posho ZOTE, hata zile za kujikimu! Pinda anapozunguzia kwamba kuna posho ambazo zipo kisheria, anazungumzia zile za kujikimu lakini anashambuliwa hata kwa hilo. Where is honest dialogue? Sasa jamani, mabadiliko ya sera yatakuja vipi kama kila wakati tunataka ku-score political points? Yaani hapa kulikuwa na mwanya hasa wa kuleta mabadiliko ya sera, lakini naona Chadema wameamua kufanya siasa zaidi kuliko uzalendo wa kujenga consensus. Anotehr missed opportunity.
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Uzalendo umekwisha zikwa kitambo.
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,206
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Yah niliwaona vizuri kule twitter wakijadiliana,january alikili kuwa kwenye vikao secretary ya ccm alishinikiza ziondolewe!
   
 4. h

  hoyce JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sijua kama walizungumzia au mleta mada hii anajua kuwa kupunguza posho hizo achadema imo kwenye ilani ya uchaguzi iliyoandikwa kabla Januari kukaa kwenye orientation meeting na kulamba hizo posho, kisha kuandika shairi na kujirekodi akiliimba. Tujiulize mbona hakutoa public kuzipinga hadi chadema waweke kwenye bajeti yao. Sijua pia kama huo mjadala wa twiter ulikumbushia kuwa Dk. Slaa (sio zitto anayeimbwa sasa) alilishupalia akiwa bado mbunge wakati akipinga ukubwa wa malipo ya wabunge? Mmesahau kuwa alibanwa kuwa anatoa siri za bunge akasema yeye anataja mshahara wake ambao haukuwa siri za bunge? Natumia mobile siwezi kuweka link. Nikipata fursa nitarejea kupitia PC
   
 5. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Nani asiyefahamu kuwa CCm na serikali yake ni wazuri sana ktoa matamko bila ya vitendo. Tazama suala la ununuzi wa magari ya serikali ni kwanini hadi sasa mabilioni ya walipa kodi yanaendelea kuteketea? Mdio maana Chadema wameamua kuchukua hatua kuondoa suala hili kwa vitendo,
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Jamani tuwe wa kweli: Angalia Ilani ya Chadema ya Uchaguzi:

  NI Chadema iliyoweka suala hili kwenye ilani yake. Wanaposimama kuanza kulitetea hawajadandia hoja za CCM. Sera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu ilisemwa hivi kwenye Ilani kuhusiana mpango wa kuboresha sekta ya sheria na mahakama.

  Somebody need to help me.. kati ya vyama hivi viwili ni kipi kiliahidi sera ya kupunguza posho na kubana matumizi kwa kugusa mishahara na posho za viongozi wetu?
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Acha Kuspin Pinda Tumemsikia Bana Acha Kumtia Maneno Mdomoni
   
 8. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwanza unapashwa kuelewa ya kua CCM wameondoa allowance hizo kutokana na matatizo makubwa ya kiuchumi yanayokikabili chama hicho Tawala CCM,hawakufanya hivyo kwa kupenda.Kama kweli wamefanya hivyo kwa kupenda na kwa uchungu wa ubadhirifu wa fedha za Umma ni kwa mantiki gani wanapinga kufutwa kwa posho za wabunge!HAINIINGII AKILINI NI USANII USIO NA MANTIKIO(igizo la chekechea katika jukwaa la chuo kikuu)MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 9. Kamisaa

  Kamisaa Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji,

  Okay, I will give it to you kwamba CHADEMA waliweka suala la kupunguza posho kwenye Ilani yao. That is well and good. Lakini hii haimaanishi kwamba hakuna watu ndani ya CCM ambao nao wanakubaliana na kufutwa kwa posho zisizo na lazima! Kujaribu kudai kwamba Serikali na wana CCM wote wanapenda sitting allowance ni upotoshaji pia (exhibit A ni Makamba junior), na isitoshe hata wabunge ndani ya Chadema wengine hawataki posho zifutwe (soma TheCitizen la leo). So what gives?

  Cha msingi hapa ni hichi... je CDM wanajaribu kutekeleza hii sera yao au wanataka umaarufu tu wa kung'ang'ania kwamba sera ni mali yao na sio ya wengine? Hii approach waliyochukua je italeta tija katika kubadilisha sera, au ni approach ya kujenga umaarufu tu? Narudia tena - huu ungekuwa ni wakati muafaka kwa Chadema kujenga concensus na coalitions ili kuwezesha mabadiliko katika posho, sio kupiga malumbano tu ili waandikwe magazetini. Wakati wa kukosoa tu CCM umepita, wananchi wanategemea results from CDM.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kamisaa kama kulikuwa japo na mti mmoja ndani ya ccm ni nani? Alisema wazo hilo kwenye kampeni gani? Kuwa na wazo tu haina maana yoyote kama hujatoa wazo hilo kama maoini. Mawazo hayahesabiwi.

  La pili ni kuwa siasa ni umaarufu; hakuna mwanasiasa asiyetaka umaarufu. Bahati mbaya CCM wameshapoteza umaarufu wao na wanazidi kupoteza na kutokana na hilo wanalalamikia umaarufu wa wenzao. Well.. wakifanya yanayoleta umaarufu watapewa umaarufu. Lakini umaarufu hauji kwa kulalamikia umaarufu wa wengine! Kumbuka siasa ni umaarufu.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..posho imeondolewa kwenye vikao vya CCM kama suala la mpito tu.

  ..hiki ni kipindi cha mpito wakati makundi ya kifisadi yakipokezana jukumu la kuifadhili CCM.
   
 12. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hivi how hard is it to merge all POSHO THREADS?
   
 13. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Join Date : 18th June 2011
  Posts : 11
  Thanks 0Thanked 2 Times in 1 Post

  Rep Power : 0

  Another crap
   
 14. Kamisaa

  Kamisaa Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siasa sio umaarufu kaka! Na umaarufu sio kipimo cha uongozi jasiri au uzalendo either! Lengo la siasa ni kukamata dola ili kustawisha maisha ya wananchi, sio kujilimbikia umaarufu. Hii falsafa ya viongozi wa upinzani itatumaliza, mark my words!
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Siasa Ni Umaarufu na Ndio Maana CCM waiteua Mgombea Maarufu wa Urais. Tofauti aliyokuwa nayo JK na Salim au Mwandosya ni UMAARUFU hata Makamba Senior alisema hili
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa Kamisaa sijui kama unajua maana ya neno maarufu. Ni kupendwa au kukubalika. Sasa usipokubalika/kupendwa utakamataje dola? Hii falfasafa ya CCM kupoteza umaarufu na kushindwa uchaguzi wa kidemokrasia kisha ikachachua matokeo halali itatuletea balaa huko mbeleni.
   
 17. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #17
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa Kamisaa sijui kama unajua maana ya neno maarufu. Ni kupendwa au kukubalika. Sasa usipokubalika/kupendwa utakamataje dola? Hii falfasafa ya CCM kupoteza umaarufu na kushindwa uchaguzi wa kidemokrasia kisha ikachachua matokeo halali itatuletea balaa huko mbeleni.
   
 18. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #18
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Mkuu, tafuta kamusi ya kiswahili angalia maana ya neno umaarufu. huwezi kuchaguliwa bila kuwa maarufu and so politics is about popularity ndugu yangu. lazima watu wakufahamu na ndiyo wakuchague.
   
 19. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #19
  Jun 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Toa kinyesi chako hapa. acha kuandika utumbo njoo na data. vyama vya upinzani viligawana na ccm kura kwenye kanda husika na chama husika. ccm won election. Period.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Jun 22, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na wewe usiite maoni ya mwenzako kuwa ni kinyesi. Kama CCM walishinda 60% mbona wanahaha na kujivua magamba? 60% should be very comfortable, no? But look at the way they are acting. They are panicking!
   
Loading...