Alichonifanyia huyu mama Ubungo stendi ya mabasi sio uungwana

Nyamwage

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
634
1,535
Hi,

Sikuhitaji anishukuru wala sikuhitaji anilipe hapana ila mikausho aliyo nionyesha kwa kweli ameninyanyasa kihisia.

Nilikua natoka Mwanza nakuja Dar niliwahi mapema sana kufika pale ofisini kwao yanakolala magari panaitwa Nata nikapanda nika kaa kwenye seat yangu ilikua msitari wa tatu kutoka mlango wa kuingilia na abiria wengine wakaingia sasa kuna dada mmoja kaingia akiwa na mtoto wa kiume mwenye umri kama miaka kumu hivi wakatafuta seat yao wakaipata.

Kumbe seat yake ilikua pamoja na mimi basi yule dada akaniuliza samahani kaka unashuka wapi nikamjibu nashuka mwisho ubungo yule dada kanikabidhi yule mtoto eti nimfikishe ubungo atapokelewa na mzazi wake na akanipa namba yake na namba ya mama wa huyo mtoto ambaye anatusubiri Ubungo.

Chuma ikaondoka ikapitia stendi kuu ya mabasi Nyegezi ikakusanya abiria wengine ilipofika saa 06:00 AM chuma zikaruhusiwa zikaanza kuikata mikoa kuitafuta Dar sasa huko njia yule mama ambae yuko Dar anasumbua kwenye simu kibaya zaidi ana beep mimi ndio nampigia anauliza mmefika wapi namueleza tuko sehemu fulani anatulia baada tena ya saa moja ana beep tena nampa maelezo yote tulipo fika mara abeep napiga anataka kuongea na mwanae okay sio mbaya nampa simu anaongea na mwanae.

Sikuweza hata kumnunulie dogo snacks sababu alikua anatapika kichefu chefu kinamshika mara kwa mara hata tulipo fika pale singida hotelini msosi alio nunua hakumaliza tumekuja mpaka giza linaaza kuingia bado hatujaingia hata Moro town yule mama bado ana endelea kuuliza tumefika wapi nampa maelezo yote tulipofika anatulia mpaka tunaingia Dar saa 23:58 PM.

Mpaka tunaingia stendi ananiuliza namwabia ndio tunaingia stendi bus tuliomo sisi ni Zuberi no2 chuma kimetafuta sehemu kika park vizuri abiria tukaanza kushuka nikampigia ndio tunashuka akasema haya na mimi niko hapa hapa tumeshuka huku dogo nimemshika mkono dogo kaniponyoka bwana kamkimbilia mama ake wameonana wana kumbatiana nikawasogelea nikasubiri wakumbatiane wamalize ili niwaage kua mimi naenda mwanao usha muona maana mmenikabidhi inabidi na mimi niwakabidhi.

Huwezi amini yule dada namemkaribia namsalimia kajikausha nikajua hajasikia nikaongeza sauti nikasalimia tena kanisikia hajaitikia kaniangalia alafu kanipotezea nikaona isiwe tabu niwaage mimi niende haya mimi naenda kimya hakuna hata mmoja alie nijibu nikaondoka zangu nimefika home nimelala kesho nampigia simu yule dada wa mwanza alie nikabidhi mtoto ili nimjulishe kua mtoto alifika kwa mama yake salama yule dada wa mwanza nae pia hapokei simu.

Sijui ni kabila gani watu wale.
 
Kwenye situation Kama hizi,ndipo inapoonekana umuhimu wa kauli ya mind your own business. Anyway kuna watu ndivo walivyo hawako civilized hata kidogo mpaka unajiuliza na kujijibu mwenyewe bila Shaka hichi kiumbe kitakuwa hakipo normal.

So endelee kutenda wema usisite eti kwasababu ya wapuuzi wachache kama huyo mdada.
 
Back
Top Bottom