Rostam Aziz: Ni ngumu kwa Mtanzania kuwekeza Kenya

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,352
14,629
Mfanya biashara billionea wa Tanzania bwana Rostam Aziz leo akizungumza kwenye kongamano la wafanyabiashara kati ya Tanzania na Kenya kwenye ziara ya rais Samia amesema mazingira ya uwekezaji kati ya hizi nchi mbili hayako sawa.

Rostam amesema ni rahisi sana kwa Mkenya kuwekeza Tanzania lakini ni ngumu sana kwa Mtanzania kuwekeza Kenya ndiyo maana makampuni mengi ya Wakenya yapo Tanzania na makampuni machache sana ya Watanzania yapo Kenya.

Rostam ametolea mfano kuwa mwaka 2017 aliongea na Rais Uhuru ili aende kuwekeza kwenye sekta ya gesi lakini mpaka sasa unaenda mwaka wa nne hakuna kilichofanyika.


My take
Rais Samia kuwa makini na wakenya ni wazalendo kupitiliza wa nchi yao wako tayari kusingizia mlima Kilimanjaro upo Kenya ili wapate watalii. Kenya wako tayari wawe wazalishaji (producers) na nchi nyingine kwenye jumuia ya Afrika mashariki ziwe watumiaji(consumers)

Rais Samia usisikilize kelele za majinga chadema ambayo yanachokijua ni kushangilia tu.

Mwananchi
 
Samia akicheka na nyani atavuna mabua.

Samia asipende sifa za kijinga kutoka kwa watu hasa wapinzani.

Wapinzani wengi kama sio wote nchi hii ni makuwadi/madalali wa watu. Wanafanya siasa kwa mwamvuli wa watu wengine walioko nyuma yao.

Naona wajinga wanampaka mama mafuta kwa mgongo wa chupa eti fungua nchi, afungue nchi kwani ilikua imefungwa?

Naona mama anataka kuingiingiza TPDC kwenye deni lingine kama lile la JK TPDC inadaiwa Trillioni 3.5 hadi mwaka jana June kwa taarifa ya CAG. Kujenga bomba lingine hadi Mombasa ni deal ya watu hiyo maana itahitajika mkopo tena wa zaidi ya Trillioni 4 ama Dollar Billion 2 za Marekani.

Tulikopa kujenga bomba toka Mtwara Dar, linatumika kwa 4% huku 96% haitumiki. Sasa tunataka kukopa tena tupeleke gas Mombasa.

Tusubiri tuone.
 
Utashangaa baadhi ya Watz wenzetu wanashabikia eti Rais Uhuru Kenyatta karuhusu wawekezaji kutoka Tz oooh karuhusu Watz kufanya kazi Kenya na mambo kibao.Kama huwajui Wakenya nyamaza, tuongee siye tuliowahi kukaa na kusoma Kenya .Wale watu ni wabaguzi hatari hawafai hawafai
 
Mlisema Miye Mpole Dawa Ni Kuleta Mkali
Naondoka Miye Nawaachia Chuma Hiki
Na Sasa Kimeanza Kutema Che~~Che
Pale Nilipochoka Miye Yeye Atakwenda Kwa Kasi
Nakwenda Msonga Nitalala Usingizi Mzuri

JK ๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜‡๐Ÿ˜‡๐Ÿธ
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom