Alichokisema Mo kuhusu uamuzi wake jana nimemuelewa, hata mimi hasira zikizidi nalipuka

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Mengine yanaumiza hayasemeki. Nafurahi kuona boss Mo is back na amekiri yaliotokea jana n bahati mbaya yameisha back to league.

Yule ni mtu mzima ana moyo wa binadamu jamani; hana moyo wa plastick. Majuzi tu bilioni nne zimekwenda lazima aumie.

Naomba niseme kwa maneno haya hajakana kujiuzulu; amegeuza maneno aliyoyasema na sasa tuko naye pamoja.

Kukana ni kukataa maneno ambayo hujasema.

Mh wangu amesema ya jana ya bahatimbaya. Akili za mkubwa ongeza na zenu; wengine mlitarajia aombe radhi, ng'oo sahauni!

Screenshot_20200114-193344.png
 
Ngoja waje uone watskavyokushambulia. Nasikia baada ya twitter ya Jana Viongozi wote was Simba wakiongozwa na Mropokaji wao Ndg. Haji Manara walikesha getini kwa Moo wakimbembeleza asiwape takaka ikapelekea kutoa statement ya kuwapoza Leo mchana, ila dhamira ya statement ya Jana bado hiko palepale.
 
Mengine yanaumiza hayasemeki. Nafurahi kuona boss Mo is back na amekiri yaliotokea jana n bahati mbaya yameisha back to league.

Yule ni mtu mzima ana moyo wa binadamu jamani; hana moyo wa plastick. Majuzi tu bilioni nne zimekwenda lazima aumie.

Naomba niseme kwa maneno haya hajakana kujiuzulu; amegeuza maneno aliyoyasema na sasa tuko naye pamoja.

Kukana ni kukataa maneno ambayo hujasema.

Mh wangu amesema ya jana ya bahatimbaya. Akili za mkubwa ongeza na zenu; wengine mlitarajia aombe radhi, ng'oo sahauni!

View attachment 1323373
Huyu Mo ana dharau sana, ndio maana aliwatunuku wachezaji bodaboda
 
Hii ni mbaya kama mmeingia mfumo wa kuuza hisa..zitaporomoka moaka basi
 
MO ni kati ya Watu wenye Moyo nzuri na wa Kiungwana.
Ingekuwa Mimi kwa bidii ninayoifanya kuisaidia Simba, halafu makocha na wachezaji wanafanya Upuuzi ule, nisingerudi Ng'o.
Ningenunua Benki na Kutulia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom