DPP awafutia Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kesi ya Uchochezi

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,353
2,137
Criminal Case No.208/2016 iliyokuwa ikimkabili Tundu Lissu na wenzake watatu katika Mahakama ya Kisutu, imefutwa na DPP kwa mujibu wa Kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo ya Makosa ya Jinai. Watuhumiwa wote wako huru.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine walikuwa ni Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh

Washtakiwa hao kwa pamoja Walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.

Patrick Mwita wakili wa serikali mbele Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisoma shitaka la kwanza na tano.

Mwita alidai kuwa shitaka la kwanza ni la kupanga njama za kutoa chapisho la uchochezi, kosa linalodaiwa kutendwa kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka 2016 ambapo;

Idrissa, Mkina na Lissu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam walipanga njama za kuchapisha taarifa za uchochezi.

Katika kosa la tano, mshitakiwa namba moja (Idrissa), namba mbili (Mkina) na namba nne (Lissu), wanatuhumiwa kuchochea hofu miongoni mwa wananchi kwa kuchapisha habari “Machafuko yaja Zanzibar” na kwamba, ingeweza kuzua vita au umwagaji damu.

Shitaka pili likimkabili Jabir, Mkina na Lissu, wakidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.

Shitaka la tatu linamuhusu Ismail akidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari ‘Machafuko yaja Z’bar’.

Shitaka la nne linamkabili Ismail akidaiwa kuchapisha gazeti bila kupeleka kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Zaidi, soma;

Thread 'Lissu, Mhariri wa Mawio wafikishwa kizimbani leo' Lissu, Mhariri wa Mawio wafikishwa kizimbani leo
 
1632297516919.png

---
1632312287563.png
 
22 September 2021
Maoni
Kesi Ya Tundu Lissu ( Chadema ) Ya Uchochezi Yafutwa Na DPP, yadaiwa Serikali Imekosa Ushahidi, je Tundu Lissu Ataipeleka Serikali Mahakamani Kudai Fidia?

Source : mubashara studio

Mahojiano ya gazeti la Mawio na Tundu Lissu kuhusu maoni yake juu uchaguzi uliofutwa Zanzibar 2015 ndiyo uliitwa "Uchochezi
Wahanga wa kesi namba 208/2016 wafunguka jinsi kesi ilivyoibuliwa na serikali, kufuatia gazeti la Mawio kufuatilia ahadi ya JPM kutafuta ufumbuzi lakini akakawia kutafutia jawabu lake na wao kama gazeti kuanza kutafua maoni ya mkwamo huo

Source : MwanaHALISI TV

KESI NAMBA 208/ 2016
Lissu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuandika habari za uchochezi


Kesi ya kwanza ya jinai namba 208 ya mwaka 2016, iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, inamkabili Lissu na wenzake watatu ambao ni Jabir Idris, Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina na Mmiliki wa mtambo liochapisha gazeti hilo kutoka Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote aliahirisha hadi Desemba 3, 2020.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Jabir Idrisa, Mhariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na mmiliki wa mtambo uliochapisha gazeti hilo kutoka Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Lissu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

DPP inabidi afanye bidii apitie mafaili mengi yaliyokuwa chini ya DPP aliyepita.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom