Alichokisema Ismail Jussa baada ya Tume kutoa Rasimu ya Katiba...

kigu

Senior Member
May 27, 2012
183
74
SAFARI YA KUELEKEA MAMLAKA KAMILI IMEPIGA HATUA KUBWA:

Na Ismail Jussa

Mamlaka ambayo tayari Zanzibar itakuwa imeyarejesha kwa kuondolewa kwenye Muungano kupitia Rasimu ilotangazwa leo ni:

1. Polisi.

2. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.

3. Kodi ya Mapato.

4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

5. Mabenki ya Kibiashara na Fedha za Kigeni.

6. Leseni ya viwanda na takwimu.

7. Elimu ya Juu.

8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.

9. Baraza la Taifa la Mitihani.

10. Usafiri na usafirishaji wa anga.

11. Utafiti.

12. Utabiri wa Hali ya Hewa.

13. Takwimu.

14. Mahkama ya Rufani.

15. Ushirikiano wa Kimataifa.

KAZI ILIYOBAKI KWA WAZANZIBARI ILI KUTIMIZA MAMLAKA KAMILI

Ni kutumia hatua zilizobakia kuyarejesha pia mamlaka katika mambo muhimu yafuatayo:

1. Mambo ya Nje.

2. Uraia na Uhamiaji.

3. Sarafu na Benki Kuu.

4. Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.

5. Usajili wa Vyama vya Siasa.

TANBIHI:
Wananchi na hasa Vijana wa Zanzibar tumefikia hatua ya kurejesha mamlaka katika mambo hayo 15 kutokana na umoja wetu na kutumia njia za amani huku tukiwa na msimamo usiyoyumba. Tuendelee kuwa pamoja, tukitumia njia za amani kabisa kukamilisha mamlaka kamili tunayoyataka.

Naiona ileeeee.........


Takriban mambo yote yanayohusu shughuli zenye gharama kubwa za kila siku za nchi yametolewa katika muungano na kila serikali ya nchi mshirika (Tanganyika na Zanzibar) itaendesha mambo hayo yenyewe. Mambo ambayo bila shaka yanahitaji pesa nyingi katika kugharamia uendeshaji wake. Tanganyika ina uchumi mkubwa na hivyo ikitumia vyema uchumi wake pamoja na mapato yatokanayo na muungano inaweza kuendesha serikali yake ya Tanganyika na kumudu vyema ghrama za uendeshaji. Zanzibar kwa upande wake ina uchumi mdogo na vyanzo vichache vya uchumi ambvyo pia vina misingi tofauti na vile vya Tanganyika. Vyanzo hivi vinahitaji kuwekewa sera tofauti na zile za Tanganyika na pia political will isiyotegemea hisani au ridhaa ya Tanganyika.
Zanzibar inahitaji mamlaka kamili ili iweze kupanga sera zake na uchumi wake na hivyo kuweza kumudu gharama za mambo lukuki ambayo sasa hayatakuwa chini ya mwamvuli wa muungano.
Wajumbe wa Mabaraza ya katiba na wajumbe wa Bunge la katiba wajipange vyema tokea sasa kuhakikisha mambo yafuatayo yanatoka katika orodha ya mambo ya muungano ili kuipa nchi yetu ya Zanzibar mamlaka kamili ya kisiasa na kiuchumi na hivyo kumudu gharama za kuendesha shughuli zote za nchi. Mambo hayo ni:
1. Uraia na Uhamiaji
2. Sarafu na benki kuu
3. Mambo ya nje
4. Vyama vya siasa

Mchezo wowote mchafu wa kuchakachua sauti kubwa ya wazanzibari ya kudai mambo hayo 4 katika hatua mbili zijazo za mabaraza ya katiba na Bunge la katiba kama ilivyofanyika katika kuandaa rasimu ya katiba itatupa sababu muafaka wazanzibari ya kuipigia katiba mpya kura ya HAPANA kwa kuwa haitokani na matashi yetu na hivyo kuufelisha mchakato mzima.
 
Ndugu yangu Ismail Juha... Mengi kati ya hayo hapo chini ni matumizi zaidi na sio uchumi zaidi... naomba ni highligth mzigo kwetu waZanzibar in red.
1. Polisi.

2. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.

3. Kodi ya Mapato.

4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

5. Mabenki ya Kibiashara na Fedha za Kigeni.

6. Leseni ya viwanda na takwimu.

7. Elimu ya Juu.

8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.

9. Baraza la Taifa la Mitihani.

10. Usafiri na usafirishaji wa anga.

11. Utafiti.

12. Utabiri wa Hali ya Hewa.

13. Takwimu.

14. Mahkama ya Rufani.

15. Ushirikiano wa Kimataifa

Ni Muhimu wakati unashangilia useme pia yako wapi mafuta na bandari ziko wapi za kuendesha huo uchumi wa kuendesha hizo huduma?
 
Mimi nadhani ingekuwa bora tuondokane na huu muungano maana chokochoko hazitaisha, tumetumia mabilioni ya pesa kuja na hii rasimu, pesa ambazo zingeweza kabisa kuinua elimu yetu.

Ipo harufu huko mbeleni tutakuja tumia matrilioni mengine kwa ajili ya hayo saba yaliyobaki kwenye muungano.

These people will never rest mpaka wahakikishe wameuvunja.
 
Go go Zanzibar. Go in one piece. Hivi unakazana kumwelimisha Jusa unadhani atakuelewa. Wakati mtu anachumbia ukimwambia lo lote kuhusu mchumba hakuelesi ni mpaka amweke ndani ndo unasikia, Lo, laiti ningewasikiliza ndugu zangu. Unakuwa umechelewa. Let Zenj go. Go,go Zanzibar, go in peace and in one piece.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Zanzibar tutasimama kwenye hoja hadi tufike pale tutakapo . Mungu ibariki Zanzibar
nchi kadogo tunalisumbua bonge la nchi .
Tembo lazima atamtapika chura alie mmeza
 
Sasa suala la elimu watasoma kwao sasa! Huo ndo utamu! Sijui wana vyuo gani huko kwao! Na serikali yao itagaramia wa zanzibar kwenye elimu!

Zanzibar kabla mungano mitihani ya secondary ilikuwa inatoka oxford England,ilimu ya juu walikuwa wanafunzi wanapelekwa kwenye vyuo vinavyojulikana kimataifa,unajua kuwa walimu wa mwanzo wa chuo kikuu cha Daresalam wengi walikuwa wazanzibar,wamebakia wachache chuoni akina Shifji.....hamna kisichowezekana mkuu
 
Jusa ni mwehu flani tu, anajidanganya na kuwadanganya waznz, hana uzalendo wwte, anadhani kuvunja muungano ndio cuf kuingia madarakani??? Znz ina uchumi gani wa kujiendesha
 
Jusa ni mwehu flani tu, anajidanganya na kuwadanganya waznz, hana uzalendo wwte, anadhani kuvunja muungano ndio cuf kuingia madarakani??? Znz ina uchumi gani wa kujiendesha

hayo ni maamuzi yetu wazanzibari si maamuzi ya jusa wala nini. Binafsi napenda uhuru wa znz.
 
Jusa ni mwehu flani tu, anajidanganya na kuwadanganya waznz, hana uzalendo wwte, anadhani kuvunja muungano ndio cuf kuingia madarakani??? Znz ina uchumi gani wa kujiendesha
Hamna ujanja mtaimbo umeganda!!!!Endeleeni kutoa povu ss hawooo mamlaka Kamili!!!
 
Mimi nadhani ingekuwa bora tuondokane na huu muungano maana chokochoko hazitaisha, tumetumia mabilioni ya pesa kuja na hii rasimu, pesa ambazo zingeweza kabisa kuinua elimu yetu.

Ipo harufu huko mbeleni tutakuja tumia matrilioni mengine kwa ajili ya hayo saba yaliyobaki kwenye muungano.

These people will never rest mpaka wahakikishe wameuvunja.
Nashindwa kuelewa faida tunayoipata kutokana na hii ndoa.
Mke mwenyewe kwanza hazai
 
Kutakuwepo na Jamhuri ya shirikisho ya zanzibar (serikali shirikishi zitakuwa serilaki ya unguja, pemba na ile ya wete).
 
Jussa yakiwazidi mnaomba Muungano na Kenya, ikishindikana Oman wapo wana wasubiri kaka zenu, ila mkiwauza wezenu kama Loliondo ilivyo fanywa mmwaambie jamaa, sio waone sukari guru n.k wakafikiria ni neema toka kwa mjomba au mafanikio ya uongozi bora kumbe mambo magumu.
 
Back
Top Bottom