SAFARI YA KUELEKEA MAMLAKA KAMILI IMEPIGA HATUA KUBWA:
Na Ismail Jussa
Mamlaka ambayo tayari Zanzibar itakuwa imeyarejesha kwa kuondolewa kwenye Muungano kupitia Rasimu ilotangazwa leo ni:
1. Polisi.
2. Mikopo na Biashara ya Nchi za Nje.
3. Kodi ya Mapato.
4. Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.
5. Mabenki ya Kibiashara na Fedha za Kigeni.
6. Leseni ya viwanda na takwimu.
7. Elimu ya Juu.
8. Maliasili ya mafuta na gesi asilia.
9. Baraza la Taifa la Mitihani.
10. Usafiri na usafirishaji wa anga.
11. Utafiti.
12. Utabiri wa Hali ya Hewa.
13. Takwimu.
14. Mahkama ya Rufani.
15. Ushirikiano wa Kimataifa.
KAZI ILIYOBAKI KWA WAZANZIBARI ILI KUTIMIZA MAMLAKA KAMILI
Ni kutumia hatua zilizobakia kuyarejesha pia mamlaka katika mambo muhimu yafuatayo:
1. Mambo ya Nje.
2. Uraia na Uhamiaji.
3. Sarafu na Benki Kuu.
4. Ushuru wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa.
5. Usajili wa Vyama vya Siasa.
TANBIHI:
Wananchi na hasa Vijana wa Zanzibar tumefikia hatua ya kurejesha mamlaka katika mambo hayo 15 kutokana na umoja wetu na kutumia njia za amani huku tukiwa na msimamo usiyoyumba. Tuendelee kuwa pamoja, tukitumia njia za amani kabisa kukamilisha mamlaka kamili tunayoyataka.
Naiona ileeeee.........

Takriban mambo yote yanayohusu shughuli zenye gharama kubwa za kila siku za nchi yametolewa katika muungano na kila serikali ya nchi mshirika (Tanganyika na Zanzibar) itaendesha mambo hayo yenyewe. Mambo ambayo bila shaka yanahitaji pesa nyingi katika kugharamia uendeshaji wake. Tanganyika ina uchumi mkubwa na hivyo ikitumia vyema uchumi wake pamoja na mapato yatokanayo na muungano inaweza kuendesha serikali yake ya Tanganyika na kumudu vyema ghrama za uendeshaji. Zanzibar kwa upande wake ina uchumi mdogo na vyanzo vichache vya uchumi ambvyo pia vina misingi tofauti na vile vya Tanganyika. Vyanzo hivi vinahitaji kuwekewa sera tofauti na zile za Tanganyika na pia political will isiyotegemea hisani au ridhaa ya Tanganyika.
Zanzibar inahitaji mamlaka kamili ili iweze kupanga sera zake na uchumi wake na hivyo kuweza kumudu gharama za mambo lukuki ambayo sasa hayatakuwa chini ya mwamvuli wa muungano.
Wajumbe wa Mabaraza ya katiba na wajumbe wa Bunge la katiba wajipange vyema tokea sasa kuhakikisha mambo yafuatayo yanatoka katika orodha ya mambo ya muungano ili kuipa nchi yetu ya Zanzibar mamlaka kamili ya kisiasa na kiuchumi na hivyo kumudu gharama za kuendesha shughuli zote za nchi. Mambo hayo ni:
1. Uraia na Uhamiaji
2. Sarafu na benki kuu
3. Mambo ya nje
4. Vyama vya siasa
Mchezo wowote mchafu wa kuchakachua sauti kubwa ya wazanzibari ya kudai mambo hayo 4 katika hatua mbili zijazo za mabaraza ya katiba na Bunge la katiba kama ilivyofanyika katika kuandaa rasimu ya katiba itatupa sababu muafaka wazanzibari ya kuipigia katiba mpya kura ya HAPANA kwa kuwa haitokani na matashi yetu na hivyo kuufelisha mchakato mzima.