Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Jana akiwa mkoani Kigoma, katibu mkuu wa CHADEMA, Dr.W.Slaa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake alisema CHADEMA hatumuogopi Slaa, hatumuogopi Mbowe, Hatumuogopi Mtei wala hatumuogopi Zitto. Hatuogopi mtu yeyote. CHADEMA tunaiogopa katiba!. Ukiitizama kauli hii unagundua kwamba ni kauli ya kifalsafa; falsafa sahihi kabisa inayopaswa kufanyiwa kazi na taasisi yeyote kubwa inayotaka kuendelea .
Hata hivyo nikilinganisha kauli hii sahihi (kimantiki), ya Kiongozi huyo maarufu kabisa nchini, na kile tunachokifanya, binafsi kuna vitu nashindwa kuvielewa!.Pengine tatizo ni uchanga wangu katika masuala ya katiba sheria na siasa na hasa siasa za CHADEMA!.Ni matumaini yangu basi kwamba wale ambao ni wakomavu katika mambo haya watanielewesha kiroho safi tu!.
1.Tumemshuhudia Msigwa! Namzungumzia Mchungaji Msigwa!, akiwatukana wanachama wenzake hadharani na hajachukuliwa hatua yoyote.Tumemsikia maneno aliyoyatoa Arusha kuwakashifu wanachama Fulani ndani ya chama.Ningependa wanaojua katiba vizuri wanisaidie, Mchungaji alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba katika hili!
2.Mh.Lema! Namzungumzia Lema wa Arusha! Tumemsikia akizua tuhuma na kejeli dhidi wa wanachama/viongozi wenzake bila kupitia vikao, bali mikutano na mitandao ya kijamii.Kila mtu ni shahidi wa hili na hajachukuliwa hatua yeyote, hata kukemewa!. Ningewaomba wenzangu ambao ni wajuvi wa katiba na mambo ya sheria na siasa wanifahamishe kama Lema alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba ya Chama au ya Nchi!.
3.Yericko, Namzungumzia Yericko Nyerere, yeye amekuwa akimkashifu mwanachama/aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa Chama kwa kumuita muhuni n.k.Yeye mwenyewe ni shahidi wa hilo na kwa kuwa yuko hapa atakana ikiwa namsingizia!.Yericko amekuwa akitusisitiza wakati wote kufuata misingi/katiba na si mtu.Ningependa yeye mwenyewe, au mtu mwengine ambaye anaijua katiba vizuri atusaidie kwamba alikuwa akitekeleza kufungu gani katika katiba!.
4. Ndani na nje ya bunge kuna watu wamekuwa wakiwaita wezao kwa majina ya kejeli na ya kuudhi.Ningependa wanaojua katiba wanisaidie kunielewesha kama hiyo nayo ni sehemu ya utekelezaji wa katiba.Ningependa wajuvi wa siasa wanijulishe ikiwa chama au kikundi cha siasa kinaweza kupata uungwaji mkono zaidi pale kinapowaita kwa majina mabaya na ya kuudhi wale ambao ndio wanatakiwa kukiunga mkono Chama.Hivi tunajua hakuna mtu anayezakiwa na chama? hivi tunajua CCM wa Jana ni CHADEMA wa leo n.k? Hivi mfano tunadhani tunaweza kumshawishi mtu wa CCM akajiunga na CHADEMA kwa kumuita "MACCM" "PIMBI" "NDONDOCHA" "MSENGENYAJI"n.k? Hivi wewe mtu akikushawishi kumuunga mkono kwa staili hiyo,unamuunga?
Hivi hatuoni kwa kutukanana! na kuitana majina ya kuudhi bila sababu kunachochea chuki isiyo ya lazima?Hivi tunadhani kama kila mtu akiamua kuchochea chuki dhidi ya mwenzake ni nini hatma ya nchi hii? Hivi tunajua hatua ya kwanza kuelekea mauaji ya kimbari ni ubaguzi, na hatua ya pili ni kuchochea chuki kati ya kundi na kundi, chama na chama n.k?
Najua wapo watakaonitukana ila najua wapo watakaonielewa vile vile.