Alichokisema Dr.W. Silaa Vs Kile Tunachokifanya!.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,427
Jana akiwa mkoani Kigoma, katibu mkuu wa CHADEMA, Dr.W.Slaa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake alisema “CHADEMA hatumuogopi Slaa, hatumuogopi Mbowe, Hatumuogopi Mtei wala hatumuogopi Zitto. Hatuogopi mtu yeyote. CHADEMA tunaiogopa katiba!”. Ukiitizama kauli hii unagundua kwamba ni kauli ya kifalsafa; falsafa sahihi kabisa inayopaswa kufanyiwa kazi na taasisi yeyote kubwa inayotaka kuendelea .

Hata hivyo nikilinganisha kauli hii sahihi (kimantiki), ya Kiongozi huyo maarufu kabisa nchini, na kile tunachokifanya, binafsi kuna vitu nashindwa kuvielewa!.Pengine tatizo ni uchanga wangu katika masuala ya katiba sheria na siasa na hasa siasa za CHADEMA!.Ni matumaini yangu basi kwamba wale ambao ni wakomavu katika mambo haya watanielewesha kiroho safi tu!.

1.Tumemshuhudia Msigwa! Namzungumzia Mchungaji Msigwa!, akiwatukana wanachama wenzake hadharani na hajachukuliwa hatua yoyote.Tumemsikia maneno aliyoyatoa Arusha kuwakashifu wanachama Fulani ndani ya chama.Ningependa wanaojua katiba vizuri wanisaidie, Mchungaji alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba katika hili!

2.Mh.Lema! Namzungumzia Lema wa Arusha! Tumemsikia akizua tuhuma na kejeli dhidi wa wanachama/viongozi wenzake bila kupitia vikao, bali mikutano na mitandao ya kijamii.Kila mtu ni shahidi wa hili na hajachukuliwa hatua yeyote, hata kukemewa!. Ningewaomba wenzangu ambao ni wajuvi wa katiba na mambo ya sheria na siasa wanifahamishe kama Lema alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba ya Chama au ya Nchi!.

3.Yericko, Namzungumzia Yericko Nyerere, yeye amekuwa akimkashifu mwanachama/aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa Chama kwa kumuita muhuni n.k.Yeye mwenyewe ni shahidi wa hilo na kwa kuwa yuko hapa atakana ikiwa namsingizia!.Yericko amekuwa akitusisitiza wakati wote kufuata misingi/katiba na si mtu.Ningependa yeye mwenyewe, au mtu mwengine ambaye anaijua katiba vizuri atusaidie kwamba alikuwa akitekeleza kufungu gani katika katiba!.

4. Ndani na nje ya bunge kuna watu wamekuwa wakiwaita wezao kwa majina ya kejeli na ya kuudhi.Ningependa wanaojua katiba wanisaidie kunielewesha kama hiyo nayo ni sehemu ya utekelezaji wa katiba.Ningependa wajuvi wa siasa wanijulishe ikiwa chama au kikundi cha siasa kinaweza kupata uungwaji mkono zaidi pale kinapowaita kwa majina mabaya na ya kuudhi wale ambao ndio wanatakiwa kukiunga mkono Chama.Hivi tunajua hakuna mtu anayezakiwa na chama? hivi tunajua CCM wa Jana ni CHADEMA wa leo n.k? Hivi mfano tunadhani tunaweza kumshawishi mtu wa CCM akajiunga na CHADEMA kwa kumuita "MACCM" "PIMBI" "NDONDOCHA" "MSENGENYAJI"n.k? Hivi wewe mtu akikushawishi kumuunga mkono kwa staili hiyo,unamuunga?

Hivi hatuoni kwa kutukanana! na kuitana majina ya kuudhi bila sababu kunachochea chuki isiyo ya lazima?Hivi tunadhani kama kila mtu akiamua kuchochea chuki dhidi ya mwenzake ni nini hatma ya nchi hii? Hivi tunajua hatua ya kwanza kuelekea mauaji ya kimbari ni ubaguzi, na hatua ya pili ni kuchochea chuki kati ya kundi na kundi, chama na chama n.k?

Najua wapo watakaonitukana ila najua wapo watakaonielewa vile vile.
 
Nchi hii ina vyama 21 kila Mwananchi Ana haki ya kuchagua chama anachokitaka..........Najaribu kuielewa mada yako na hasa dhumuni lake , ngoja nitumie kusoma huenda nikaelewa then nipate cha kuchangia .....
 
Mkuu pamoja na kuwa na vyama vingi, Ila nimegundua kwa kiasi fulani watanzania ndio wale wale.Kama mtu alikuwa CCM na anashinda baa, anaweza kuhamia chadema akashinda huko huko baa na akahamia cuf akashinda huko huko n.k. Nimegundua kitu cha msingi nikuelekeza pale pale mtu ulipo.Kemea mabaya hapo hapo ulipo kwani kwa mfano kama mtu ni mchonganishi, ni mchonganishi tu ndani ya chama chochote atakachokuwa na tabia hiyo itabakia kuwa tabia isiyokubalika hadi hapo atakapoamua kuiacha.Na miongoni mwa njia zinazoweza kumfanya akaicha ni pamoja na kumkosoa na kumkemea ikibidi.
 
Ni ngumu sana kumuamini Slaa, Kipindi cha kampeni aliaminisha wananchi kwamba akichaguliwa Raisi wa nchi atafuta mashangingi, nilipenda kauli yake ila baada ya kushindwa uchaguzi mkuu yeye anatembelea VX (shangingi) ambalo alituaminisha eti gharama ya gari moja ni sawa na zahanati nne..........Juzi tu kwenye uzi wa Chadema (kurugenzi ya habari) nilimuona akiwa Kakonko ndani ya VX dah nilichoka, nikajiuliza serikali yake ingekuwa inatumia magari ya kifahari sana na ingekuwa serikali ya anasa kwani pamoja na kuponda safari za JK yeye kwa kutumia pesa za Ruzuku wiki kadhaa akiwa marekani eti kwa kilichitwa ''safari ya mafunzo'', huku kurugenzi ya habari ikidanganya kwamba ni state visit duh........hivi angekuwa Raisi huyu jamaa pengine angehamia ulaya/marekani moja kwa moja huu ni ulaghai
 
Mimi ni kama wewe ulivyosema ni mchanga kwenye hiyo katiba ila nitakujibu kwa kutumia common sense tu. Watu wengi wanafanya makosa, akiwemo Slaa na hata Mbowe. Huwezi kila mtu anapoongea kitu basi wewe uanze kufuatilia kifungu gani katika katiba ili umchukulie hatua. Tukifanya hivyo nadhani hakutakuwa na muda wa kufanya chochote kwani watu wanaongea kila siku.

Zitto kafanya mambo mengi ya ajabu ajabu huko nyuma , ikiwemo kuwasema viongozi wake vibaya. Mbona katiba haikutumika ? Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida kwa maoni yangu mimi aliyoyasema ukifuatilia katiba amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa Chadema, Mbona hakuna mchakato ulioanzishwa wa kumvua uanachama ? Kwa hiyo sio kila kauli au activity inayotokea basi automatically watu wanafuatilia vifungu vya katiba na kuhakikisha vinatekelezwa.

Hekima nayo inatakiwa. Ndio maana Zitto amevumiliwa muda mwingi (na ameshaonywa huko nyuma), na sasa baada ya issue ile ya usaliti ya kutaka kukihujumu chama waziwazi, chama kimeamua kuchukua hatua (ofcourse kwa kufuata katiba na taratibu za chama).

Zitto kuendelea kukiponda chama kwenye vyombo vya habari baada ya yeye kuvuliwa uongozi, inapandisha hasira zaidi kwa watu (including me), na watu wanaweza wakareact in one way or another...Sioni sababu za msingi za kuanza kufuatilia vifungu vya katiba kwa reactions hizi.

Wewe juzi mwenyewe ulileta uzi ukiomba busara (sio katiba) itumike kwenye issue ya Zitto na Mkumbo....

Jana akiwa mkoani Kigoma, katibu mkuu wa CHADEMA, Dr.W.Slaa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake alisema "CHADEMA hatumuogopi Slaa, hatumuogopi Mbowe, Hatumuogopi Mtei wala hatumuogopi Zitto. Hatuogopi mtu yeyote. CHADEMA tunaiogopa katiba!". Ukiitizama kauli hii unagundua kwamba ni kauli ya kifalsafa; falsafa sahihi kabisa inayopaswa kufanyiwa kazi na taasisi yeyote kubwa inayotaka kuendelea .

Hata hivyo nikilinganisha kauli hii sahihi (kimantiki), ya Kiongozi huyo maarufu kabisa nchini, na kile tunachokifanya, binafsi kuna vitu nashindwa kuvielewa!.Pengine tatizo ni uchanga wangu katika masuala ya katiba sheria na siasa na hasa siasa za CHADEMA!.Ni matumaini yangu basi kwamba wale ambao ni wakomavu katika mambo haya watanielewesha kiroho safi tu!.

1.Tumemshuhudia Msigwa! Namzungumzia Mchungaji Msigwa!, akiwatukana wanachama wenzake hadharani na hajachukuliwa hatua yoyote.Tumemsikia maneno aliyoyatoa Arusha kuwakashifu wanachama Fulani ndani ya chama.Ningependa wanaojua katiba vizuri wanisaidie, Mchungaji alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba katika hili!

2.Mh.Lema! Namzungumzia Lema wa Arusha! Tumemsikia akizua tuhuma na kejeli dhidi wa wanachama/viongozi wenzake bila kupitia vikao, bali mikutano na mitandao ya kijamii.Kila mtu ni shahidi wa hili na hajachukuliwa hatua yeyote, hata kukemewa!. Ningewaomba wenzangu ambao ni wajuvi wa katiba na mambo ya sheria na siasa wanifahamishe kama Lema alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba ya Chama au ya Nchi!.

3.Yericko, Namzungumzia Yericko Nyerere, yeye amekuwa akimkashifu mwanachama/aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa Chama kwa kumuita muhuni n.k.Yeye mwenyewe ni shahidi wa hilo na kwa kuwa yuko hapa atakana ikiwa namsingizia!.Yericko amekuwa akitusisitiza wakati wote kufuata misingi/katiba na si mtu.Ningependa yeye mwenyewe, au mtu mwengine ambaye anaijua katiba vizuri atusaidie kwamba alikuwa akitekeleza kufungu gani katika katiba!.

4. Ndani na nje ya bunge kuna watu wamekuwa wakiwaita wezao kwa majina ya kejeli na ya kuudhi.Ningependa wanaojua katiba wanisaidie kunielewesha kama hiyo nayo ni sehemu ya utekelezaji wa katiba.Ningependa wajuvi wa siasa wanijulishe ikiwa chama au kikundi cha siasa kinaweza kupata uungwaji mkono zaidi pale kinapowaita kwa majina mabaya na ya kuudhi wale ambao ndio wanatakiwa kukiunga mkono Chama.Hivi tunajua hakuna mtu anayezakiwa na chama? hivi tunajua CCM wa Jana ni CHADEMA wa leo n.k? Hivi mfano tunadhani tunaweza kumshawishi mtu wa CCM akajiunga na CHADEMA kwa kumuita "MACCM" "PIMBI" "NDONDOCHA" "MSENGENYAJI"n.k? Hivi wewe mtu akikushawishi kumuunga mkono kwa staili hiyo,unamuunga?

Hivi hatuoni kwa kutukanana! na kuitana majina ya kuudhi bila sababu kunachochea chuki isiyo ya lazima?Hivi tunadhani kama kila mtu akiamua kuchochea chuki dhidi ya mwenzake ni nini hatma ya nchi hii? Hivi tunajua hatua ya kwanza kuelekea mauaji ya kimbari ni ubaguzi, na hatua ya pili ni kuchochea chuki kati ya kundi na kundi, chama na chama n.k?

Najua wapo watakaonitukana ila najua wapo watakaonielewa vile vile.
 
Ni ngumu sana kumuamini Slaa, Kipindi cha kampeni aliaminisha wananchi kwamba akichaguliwa Raisi wa nchi atafuta mashangingi, nilipenda kauli yake ila baada ya kushindwa uchaguzi mkuu yeye anatembelea VX (shangingi) ambalo alituaminisha eti gharama ya gari moja ni sawa na zahanati nne..........Juzi tu kwenye uzi wa Chadema (kurugenzi ya habari) nilimuona akiwa Kakonko ndani ya VX dah nilichoka, nikajiuliza serikali yake ingekuwa inatumia magari ya kifahari sana na ingekuwa serikali ya anasa kwani pamoja na kuponda safari za JK yeye kwa kutumia pesa za Ruzuku wiki kadhaa akiwa marekani eti kwa kilichitwa ''safari ya mafunzo'', huku kurugenzi ya habari ikidanganya kwamba ni state visit duh........hivi angekuwa Raisi huyu jamaa pengine angehamia ulaya/marekani moja kwa moja huu ni ulaghai
Mkuu nadhani hii hoja ya mashangingi unayoiibua ni hoja pana kidogo ambayo ingestahili kuwa na uzi wa peke yake.Kwa sasa hivi ningependa tujadili hili la kufuata au kutokufuata katiba na misingi yake kinadharia na kimatendo kwa sababu lenyewe ni mada pana kidogo ikiwa watu wataamua kuwa wawazi na wakweli.
 
Swali la nyongeza, Mhe.Magufuli aliposema wasio na nauli ya kivuko wapige mbizi kisha watokee upande wa pili alitumia kifungu gani cha katiba?
 
Mimi ni kama wewe ulivyosema ni mchanga kwenye hiyo katiba ila nitakujibu kwa kutumia common sense tu.
Watu wengi wanafanya makosa, akiwemo Slaa na hata Mbowe. Huwezi kila mtu anapoongea kitu basi wewe uanze kufuatilia kifungu gani katika katiba ili umchukulie hatua. Tukifanya hivyo nadhani hakutakuwa na muda wa kufanya chochote kwani watu wanaongea kila siku.
Mkuu kwa hiyo unashauri kwamba wakati fulani hata kama mtu anavunja katiba, inatakiwa aachwa tu ili tupate muda wa kufanya mambo mengine?Yaani Hata tusimkemee! Hivi kumkemea mtu kunachukua dakika ngapi? Si tumesema tukiruhusu mtu yeyote kuvunja katiba kwa namna yeyote na akaachwa kwa sababu yeyote ni lazima chama kitakufa kwa kuacha kuilinda katiba?au wewe hukubaliani na mtizamo huo?

Zitto kafanya mambo mengi ya ajabu ajabu huko nyuma , ikiwemo kuwasema viongozi wake vibaya. Mbona katiba haikutumika ?
Unaweza kutukumbusha kwa ushahidi kwamba ni lini na wapi Zitto alishawahi kumtukana kiongozi yeyote (awe wa CHADEMA au wa chama chochote)? Ikiwa zitto alivunja katiba na tukamuacha je tulikuwa sahihi? je! ni kwa nini tulimuacha licha ya kuwa alikuwa anavunja katiba? kama tulimuacha mtu akawa anavunja katiba na hali tunamuona na leo tunasema tunaiogopa na kuitetea katiba na si watu, inamaana tunaongea kitu ambacho sio cha uhalisia?
Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida kwa maoni yangu mimi aliyoyasema ukifuatilia katiba amepoteza sifa ya kuwa mwanachama wa Chadema, Mbona hakuna mchakato ulioanzishwa wa kumvua uanachama ?
Kwa hoja hii, ina maana katiba ya chadema haiheshimiwi! kwa kuwa kama ingeheshimiwa basi yule bwana alipaswa kutimuliwa?

Hekima nayo inatakiwa.
Hekima unazungumzia ni muhusika kuomba radhi!, muhusika kukosolewa!, au muhusika kukemewa!, au muhusika kuachwa tu aendelee apendavyo?
Ndio maana Zitto amevumiliwa muda mwingi (na ameshaonywa huko nyuma)
,Vipi kitila? naye kavumiliwa au kulingana na makosa yake hafai kuvumiliwa hata kama kaomba msamaha (tofauti na wengine ambao hata msamaha hawakuomba)?Je unadhani ni sahihi kumvumilia mtu anayevunja katiba bila hata kumuonya?n
Zitto kuendelea kukiponda chama kwenye vyombo vya habari
Katika historia ya Zitto kuna mahali ameshawahi kukiponda Chama chake kwenye vyombo vya habari? unaweza kunukuu maneno machache kutuonesha alivyokuwa amekiponda? unadhani kwa nini hakuchukuliwa hatua?

Mwisho wewe unakubali kwamba niliowataja hapo juu wamevunja katiba au unakataa?na kwa nini!
 
Swali la nyongeza, Mhe.Magufuli aliposema wasio na nauli ya kivuko wapige mbizi kisha watokee upande wa pili alitumia kifungu gani cha katiba?
Kauli ya jana ya Dr.Slaa ilikuwa inamuhusu Magufuli (ccm)?je! role model wa CHADEMA ni CCM? ile kauli ya magufuli ilikuwa ya kuudhi na tuliikemea hasa sisi CHADEMA.Au wewe uliiunga mkono?
 
Mkuu nadhani hii hoja ya mashangingi unayoiibua ni hoja pana kidogo ambayo ingestahili kuwa na uzi wa peke yake.Kwa sasa hivi ningependa tujadili hili la kufuata au kutokufuata katiba na misingi yake kinadharia na kimatendo kwa sababu lenyewe ni mada pana kidogo ikiwa watu wataamua kuwa wawazi na wakweli.
Nimetoa mfano tu ili angalau watu walinganishe kama maneno na matendo ni tofauti, je maandishi (katiba) na matendo itakuwaje ni hayo tu mkuu
 
Jana akiwa mkoani Kigoma, katibu mkuu wa CHADEMA, Dr.W.Slaa alipokuwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake alisema "CHADEMA hatumuogopi Slaa, hatumuogopi Mbowe, Hatumuogopi Mtei wala hatumuogopi Zitto. Hatuogopi mtu yeyote. CHADEMA tunaiogopa katiba!". Ukiitizama kauli hii unagundua kwamba ni kauli ya kifalsafa; falsafa sahihi kabisa inayopaswa kufanyiwa kazi na taasisi yeyote kubwa inayotaka kuendelea .

Hata hivyo nikilinganisha kauli hii sahihi (kimantiki), ya Kiongozi huyo maarufu kabisa nchini, na kile tunachokifanya, binafsi kuna vitu nashindwa kuvielewa!.Pengine tatizo ni uchanga wangu katika masuala ya katiba sheria na siasa na hasa siasa za CHADEMA!.Ni matumaini yangu basi kwamba wale ambao ni wakomavu katika mambo haya watanielewesha kiroho safi tu!.

1.Tumemshuhudia Msigwa! Namzungumzia Mchungaji Msigwa!, akiwatukana wanachama wenzake hadharani na hajachukuliwa hatua yoyote.Tumemsikia maneno aliyoyatoa Arusha kuwakashifu wanachama Fulani ndani ya chama.Ningependa wanaojua katiba vizuri wanisaidie, Mchungaji alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba katika hili!

2.Mh.Lema! Namzungumzia Lema wa Arusha! Tumemsikia akizua tuhuma na kejeli dhidi wa wanachama/viongozi wenzake bila kupitia vikao, bali mikutano na mitandao ya kijamii.Kila mtu ni shahidi wa hili na hajachukuliwa hatua yeyote, hata kukemewa!. Ningewaomba wenzangu ambao ni wajuvi wa katiba na mambo ya sheria na siasa wanifahamishe kama Lema alikuwa akitekeleza kipengele gani cha katiba ya Chama au ya Nchi!.

3.Yericko, Namzungumzia Yericko Nyerere, yeye amekuwa akimkashifu mwanachama/aliyekuwa kiongozi mwandamizi wa Chama kwa kumuita muhuni n.k.Yeye mwenyewe ni shahidi wa hilo na kwa kuwa yuko hapa atakana ikiwa namsingizia!.Yericko amekuwa akitusisitiza wakati wote kufuata misingi/katiba na si mtu.Ningependa yeye mwenyewe, au mtu mwengine ambaye anaijua katiba vizuri atusaidie kwamba alikuwa akitekeleza kufungu gani katika katiba!.

4. Ndani na nje ya bunge kuna watu wamekuwa wakiwaita wezao kwa majina ya kejeli na ya kuudhi.Ningependa wanaojua katiba wanisaidie kunielewesha kama hiyo nayo ni sehemu ya utekelezaji wa katiba.Ningependa wajuvi wa siasa wanijulishe ikiwa chama au kikundi cha siasa kinaweza kupata uungwaji mkono zaidi pale kinapowaita kwa majina mabaya na ya kuudhi wale ambao ndio wanatakiwa kukiunga mkono Chama.Hivi tunajua hakuna mtu anayezakiwa na chama? hivi tunajua CCM wa Jana ni CHADEMA wa leo n.k? Hivi mfano tunadhani tunaweza kumshawishi mtu wa CCM akajiunga na CHADEMA kwa kumuita "MACCM" "PIMBI" "NDONDOCHA" "MSENGENYAJI"n.k? Hivi wewe mtu akikushawishi kumuunga mkono kwa staili hiyo,unamuunga?

Hivi hatuoni kwa kutukanana! na kuitana majina ya kuudhi bila sababu kunachochea chuki isiyo ya lazima?Hivi tunadhani kama kila mtu akiamua kuchochea chuki dhidi ya mwenzake ni nini hatma ya nchi hii? Hivi tunajua hatua ya kwanza kuelekea mauaji ya kimbari ni ubaguzi, na hatua ya pili ni kuchochea chuki kati ya kundi na kundi, chama na chama n.k?

Najua wapo watakaonitukana ila najua wapo watakaonielewa vile vile.
Nakuunga mkono kwa kuliona tatizo linalowakabili wapinzani wengi.
Kuichukia CCM haina maana mpinzani ana mikakati mbadala endelevu.

Na tumeona wengi kama Slaa wakiwakashifu mafisadi kwa vile walikuwa hawana hela.
Fedha zilipoeafikia tu wakazila kwa staili ile ile ya mafisadi walioko kiwango cha chekechea!

Matusi, kejeli, kuudhiana huzaa chuki baina ya vikundi tofauti vya siasa, na ndio maana nasema kama kuna ma-CCM, na mi-CCM , kama alivyosema , tena msomi uchwara Tundu Lissu, basi tuna ma Form Four Failures(F4F) wengi tu ndani ya uongozi wa CDM.

Na kwa mshangao wangu wana CDM wengi wamelielewa hilo!
 
mkuu! ninapozungumzia utumiaji wa lugha ya kuudhi, matusi, dharau, kejeli na kadhalika, simaanishi kwamba ni CHADEMA tu wanao yafanya hayo.Hayo yanafanywa na baadhi ya wanachadema na baadhi ya wana CCM vile vile na hata baadhi ya watu kutoka vyama vingine.Kwa hiyo nasisitiza; dharau ni dharau tu, naitabakia kuwa tabia mbaya bila kujali mfanyaji anatoka chama gani.Kwa mfano wewe unaposema chadema kuna Form four; wewe ujuavyo form four hawanana haki katika nchi hii? ee! au kinachotuma unawabagua, kuwapuuza kuwakejeli na kuwadharau nini? je! unajikweza kijana! kujifaharisha ni Tabia mbaya hata kama una masters, na mtu yeyote anayejifaharisha hapaswi kuwa kiongozi. Nawe kwa hili jirekebishe vile vile.
 
Kama nilivyosema mimi natumia common sense.....Lakini ukienda kwenye vifungu vya katiba na tafsiri yake kisheria unaweza kuta hata hayo unayosema wewe yamevunjwa, hayajavunjwa kwa tafsiri ya kisheria kuhusiana na vifungu hivyo (ambavyo hukuvitaja)

Nikupe mfano rahisi....Zitto alipoongelea issue ya vifaranga na mama yao....kila mtu anayefuatilia masuala ya siasa za Tz na hasa Chadema atakubaliana na mimi kwamba alikuwa anamsema Slaa au Mbowe au wote na actually alikuwa anasema kwamba wao ndio wanawaagiza/wanawatuma wafuasi wao (vifaranga) wamchafue yeye (hakutoa ushahidi wowote) - ingawa hapo nyuma tu (kabla ya kusema hiyo statement) alisema hana matatizo na viongozi wenzake - unafiki wa hali ya juu...Hii obvious ni kuwasema viongozi wenzake vibaya na mtu anaweza kukutolea kifungu cha katibu alichokwenda kinyuma nacho vibaya lakini nadhani kisheria hakuja hoja yeyote hapo....

Vile vile wewe juzi juzi uliposhauri (tena kwa udharura wa hali ya juu) kwamba haya mambo ya Zitto na Mkumbo yaishe kwa busara (bila kufuata kanuni na taratibu za chama), huoni kwamba ulikuwa unafasisitiza haya haya ya busara ambayo leo unaonekana kuyapinga ?
 
mkuu! ninapozungumzia utumiaji wa lugha ya kuudhi, matusi, dharau, kejeli na kadhalika, simaanishi kwamba ni CHADEMA tu wanao yafanya hayo.Hayo yanafanywa na baadhi ya wanachadema na baadhi ya wana CCM vile vile na hata baadhi ya watu kutoka vyama vingine.Kwa hiyo nasisitiza; dharau ni dharau tu, naitabakia kuwa tabia mbaya bila kujali mfanyaji anatoka chama gani.Kwa mfano wewe unaposema chadema kuna Form four; wewe ujuavyo form four hawanana haki katika nchi hii? ee! au kinachotuma unawabagua, kuwapuuza kuwakejeli na kuwadharau nini? je! unajikweza kijana! kujifaharisha ni Tabia mbaya hata kama una masters, na mtu yeyote anayejifaharisha hapaswi kuwa kiongozi. Nawe kwa hili jirekebishe vile vile.
Safi mkuu now we are talking!
Lakini kwa vile kauli derogatory,ya ma-CCM na 'mi-CCM imetoka kwa kiongozi wa juu sana CDM, Tumdu Lissu, na kupokelewa kwa shangwe na wana CDM na viongozi wengine, sioni jinsi ya kuwaenzi watu hao bali kuwapachika kule wanakostahili-mtaa wa kudharauliwa!
 
Kama nilivyosema mimi natumia common sense.....
Lakini ukienda kwenye vifungu vya katiba na tafsiri yake kisheria unaweza kuta hata hayo unayosema wewe hayajavunjwa kwa tafsiri ya kisheria kuhusiana na vifungu hivyo (ambavyo hukuvitaja)
Mkuu, ukiona wadau hawaji kuchangia ujue wananielewa vizuri na wanajua vizuri wamefanya nini.Mkuu, kwa majibu wa katiba ya chadema (ukitaka vifungu ntakuonesha), inakataza mwanachama kumchafua au kumtukana kiongozi/mwanachama mwenzake kwa namna na sababu yeyote ile.(hata ki ustaarabu tu wa kawaida hii iko wazi kabisa).

Nikupe mfano rahisi....Zitto
Mkuu mbona unamkimbilia zitto sana na unakwepa kabisa kuwazungumzia niliowataja hapo juu? zitto keshaadhibiwa kwa hiyo kumfanya kama mfano kumlinganisha na ambao si tu kwamba hawakuadhibiwa bali pia hawakukemewa mfano wako unakuwa si sawa sana.
alipoongelea issue ya vifaranga na mama yao....kila mtu anayefuatilia masuala ya siasa za Tz na hasa Chadema atakubaliana na mimi kwamba alikuwa anamsema Slaa au Mbowe au wote
mkuu, wa uelewa wangu mdogo wa sheria, ni kosa kumuhukumu mtu kwa kudhani (kama nimekosea mjuvi yeyote wa sheria anikosoe).Sasa mfano mimi nikiwa napigwa mawe nikiwa napita mahali fulani, halafu nikamjua anayejipiga mawe kwa mfano kwamba ni mtoto na huyo mtoto si tu kwamba sina ugomvi na yeye bali pia hatufahamiani. Kwanza hapo wewe unagundua nini? halafu nikasema "ukiona kifaranga yuko juu ya chungu ujue nyuma yuko mama yake" halafu mtu akanihuku kwa kauli hiyo kwamba nimemchafua" wewe hapo unagundua nini? kama ni adhabu kwa kuwa mwaminhifu unamwadhibu nani na kwa nini?
na actually alikuwa anasema kwamba wao ndio wanawaagiza/wanawatuma wafuasi wao (vifaranga)
alisema kina nani ndio wanawaagiza?kama hakusema alimchafua nani? kama kuna mtu analalamika kwa hilo kwamba kachafuliwa wewe unatafsiri nini? (hata hivyo zitto sasa sio mfano mzuri tena katika uzi huu kwa sababu yeye keshaadhibiwa! hebu tuwazungumzie niliowataja hapo juu zitto tumuache kwanza.Tushamjadili mno)
alisema hana matatizo na viongozi wenzake - unafiki wa hali ya juu...

Vile vile wewe juzi juzi uliposhauri (tena kwa udharura wa hali ya juu) kwamba haya mambo ya Zitto na Mkumbo yaishe kwa busara (bila kufuata kanuni na taratibu za chama),
Nimeshawahi kushauri yaishe bila kufuata taratibu za chama? mbona unanisingizia ndugu yangu? unaniwekea maneno mdomoni ndugu? aaa! jamani tunaelekea huku tena?
huoni kwamba ulikuwa unafasisitiza haya haya ya busara ambayo leo unaonekana kuyapinga ?
Kuna mahali nimepinga utumiaji wbusara? unapozungumzia utumiaji wa busara unakusudia nini? hebu nipe mfano wa busara unayozungumzia halafu mfano uwe ni nilichokigusia hapo kwenye uzi wangu.
 
Safi mkuu now we are talking!
Lakini kwa vile kauli derogatory,ya ma-CCM na 'mi-CCM imetoka kwa kiongozi wa juu sana CDM, Tumdu Lissu, na kupokelewa kwa shangwe na wana CDM na viongozi wengine, sioni jinsi ya kuwaenzi watu hao bali kuwapachika kule wanakostahili-mtaa wa kudharauliwa!
Mkuu, ukigundua mtu kakuloga, kwa busara yako nawe unatakumloga? ukigundua mtu katoka na mkeo nawe unatoka na mke wake? ukigundua mtu kafanya ufisadi dawa nawe ni kufanya ufisadi? kama ndio hivyo, ni nini hatima ya nchi hii kwa mujibu wa maoni yako?
 
We betlehem a.k.a Lumumba haueleweki
mkuu bias husababisha mtu kufanya maamuzi yasiyokuwa sahihi(kama uongo sema!). ungechangia mada halafu ukaniambia ni wapi hapaeleweki na kwa nini, nadhani ingekuwa vyema lakini kunishambulia mimi halafu bila sababu za msingi badala ya kuangalia msingi wa hoja yangu sidhani kama ni sahihi sana.Any way hebu acha kuni judge mimi. Hebu Judge mada yangu (Hivyo ndivyo wanavyofanya wasomi). Naona ma Great Thinkers wamekimbia kwenye mada hii.Bila shaka watakuwa na sababu za msingi kabisa.
 
Uliposhauri busara itumike, wakati unajua amevuliwa madaraka kwa kikao halali cha chama na hatua zaidi zitachukuliwa kwa kikao halali cha chama...ina maana ulikuwa hujui kwamba that will imply kwenda kinyume na taratibu za chama ?....Sikukuwekea maneno mdomoni nilionyesha what you implied na ninashangaa sana unapodai kwamba hukujua implication (iliyo wazi sana) ya huo ushauri wako.

Unaposema kwamba huwezi kusema kwamba Zitto aliwataja Mbowe na Slaa alipozungumzia vifaranga kwani Mch. Msigwa alimtaja Zitto kwa jina ? Ndio maana nikakwambia haya mambo ya mipasho kisheria hayana maana yeyote, ndio maana mimi sioni sababu ya kufuatilia kila kauli mtu anayotoa inakinzana vipi na vifungu vya katiba......
 
Uliposhauri busara itumike, wakati unajua amevuliwa madaraka kwa kikao halali cha chama na hatua zaidi zitachukuliwa kwa kikao halali cha chama...ina maana ulikuwa hujui kwamba that will imply kwenda kinyume na taratibu za chama ?....Sikukuwekea maneno mdomoni nilionyesha what you implied na ninashangaa sana unapodai kwamba hukujua implication (iliyo wazi sana) ya huo ushauri wako.
Any way jalia nilikosea kwa sababu naona tunaelekea kutoka kwenye mada ya msingi.Kwa kuwa lile lilikuwa ni wazo, wazo laweza kuwa sahihi au lisiwe sahihi.Hata hivyo kutoa wazo lisilo sahihi si kosa kwa kuwa mawazo ni subjective, na ndio maana nikashauri kama mtu ana cha kuongeza au kasahihisha angeweza kuchangia kwenye mjadala ule.Turudi kwenye mada ya msingi hapo juu.

Unaposema kwamba huwezi kusema kwamba Zitto aliwataja Mbowe na Slaa alipozungumzia vifaranga kwani Mch. Msigwa alimtaja Zitto kwa jina ?
Msigwa alimtaja zitto kwa jina, yericko alimtaja kwa jina, Lema alimtaja kwa jina (kama ukitaka uthibitisho kumbu kumbu ziko humu humu JF.) JE UKIGUNDUA KWAMBA WAHUSIKA WALIMTAJA KWA JINA UTABADILI MSIMAMO?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom