Alichokifanya huyu mwanamke kwa huyu msichana sio sahihi

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Mwanamke mmoja amemfumania mumewe akifanya mapenzi kitandani na msichana mwenye umri wa miaka 17 nyumbani kwake. Mwanamke huyo alimpiga msichana huyo na kumchania nguo zake kisha akamtembeza uchi mtaani.
Je, unauonaje uamuzi wa mwanamke huyu?
 
Je wewe uliyeweka picha inayomdhalilisha huyu binti upo sahihi? Tuanzie hapo kwanza

Maana aliyemfumania kamtembeza mtaani ww unamtembeza mitandaoni.
 
Ana wivu wa kijinga inabidi ashitakiwe sema na Wewe mleta Uzi ungewaziba hata sura zao basi
 
ivi tatizo ni wanaume hawaridhiki au ni wanawake kutotimiza wajibu wao?


Binafsi mwanamke anayelia na dyudyu ya mwanaume iwe ya kwake pekee huwa namuona hana akili timamu... kuhusu tatizo yote yanawezakuwa ni chanzo pia
 
Sasa si angedili na huyo mumewe tu..

Ya nini kuhangaika na michepuko bana..

Na ana bahati kakutana na mchepuko dhaifu. Michepuko mingine inaweza kuchepuka na mwenza wako na ikatoa dozi ya kichapo vilevile.

Hapo inakuwa double whammy! Umechepukwa na kichapo umechezea.

Unapochepukwa dili na mchepukaji. Achana na mchepuko.
 
ha ha ha haa..ngabu bhana...ila mie huwa naita ushamba!..mwanaume mbona guest nyingi tu!...huyo mchepuko nae..kitandani kwa mwenzio loooh!
 
Alikuwa hajui kama huyo kidume kaoa? Wote walistahili adhabu mchepukaji na mchepushwaji loh! Ila hiyo adhabu hakustahili.btwn mtoa mada ingetosha tu kueleza kwa kuweka picha manake nawewe unaendelea kumdhalilisha huyo binti,angalia sheria isikugeukie badala ya huyo mama!pole yake binti alinogewa na dudu ya mwenzie ee teh!
 
Back
Top Bottom