Alichojibiwa Mkuu wa Wilaya Baada Ya kuomba Mchango wa Mwenge Kwa Mbunge

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni rapa, Joseph ‘Prof: Jay’ Haule, amedai alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ambayo Mikumi inapatikani kujulishwa kuwa alitumiwa barua kuomba achangie mchango wa shilingi milioni 5 kwa ajili ya mbio za Mwenge.

Akizungumza na wananchi wa Ruaha Mkoani Morogoro, Prof Jay amesema alimjibu mkuu wa Wilaya hiyo kuwa, kuliko kuchangia Mbio za Mwenge ni bora fedha zake aelekeze kwenye maendeleo ya Wananchi.

“Wakati nakuja njiani Mkuu wa Wilaya alinipigia simu, akanambia Mh tumeleta barua ofisini kwako kuomba mchango wako katika mbio za mwenge, nikamwambia daah hizo hela za kuchangia karibu milioni tano, ni bora nipeleke Ruaha maji yatoke tu” Alisema.
 
Huku kijijini kwetu (Mpepai) wafanyabiashara hawataki hata kusikia habari za hiyo michango ya mwenge...wamekataa, hawataki kabisa.
 
Mwenge hauwezi kufutwa....
Kwa nini Mkuu? Mwenge ni janga au tuseme ni jipu kwani mwenge umechangia kueneza maambukizi kuwa na watoto wasio na baba etc Mimi nilitegemea Magufuli hili lingekuwa la kwanza kushughulikiwa
 
Magufuli hawezi futa mwenge kwa kuwa wakati wa kampeni ilionekana wazi anasupport ushirikina wa mwenge. Uniform zake zilikuwa na nembo ya mwenge....ila wananchi kama hawaoni umhimu wa mwenge ya nini kuchangia?
 
Mwenge kwa kiasi fulani unatokana na pesa za wananchi kuchangia maendeleo yao kwa njia isiyo ya kodi. Kwahiyo ipo miradi isingekuwepo km mwenge ungekufa.
 
Back
Top Bottom