BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
ALICHOFANYA RAIS SAMIA KWA WAFANYAKAZI NI ZAIDI YA KUUPIGA MWINGI.

Na Bwanku M Bwanku.

Leo Jumatatu Mei 16, 2022 kwenye Gazeti la TANZANIA LEO Ukurasa wa 6 nimechambua kiundani hatua ya Serikali ya Rais Samia kukata kiu iliyosubiliwa kwa hamu kubwa na Wafanyakazi kwa miaka 6 kwa kuongeza mishahara kwa asilimia 23.3. Hatua hii imevunja rekodi ya kuwa nyongeza kubwa zaidi ya mishahara kuwahi kutolewa kwa Wafanyakazi Nchini toka Tanzania ianze na kuweka rekodi ya kuwa ongezeko kubwa zaidi la mishahara ukilinganisha na Mataifa majirani na ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Bara zima la Afrika.

Ni ukweli ulio wazi kwamba, changamoto za Wafanyakazi ni zaidi ya kuongezewa mishahara kwahiyo licha ya Rais Samia kuongeza kiwango hicho kikubwa cha mishahara, bado ametatua kero nyingi na za muda mrefu za Wafanyakazi zilizoliliwa kwa muda mrefu na zilizokuwa zinakula sehemu kubwa ya mishahara yao ikiwemo kupunguza Kodi ya mishahara (PAYE) kwa 1%, Kufuta tozo ya 6% kwa Watumishi wenye Mikopo ya Elimu ya Juu na kuondoa adhabu ya 10% kwa kuchelewa kulipa Mkopo huo, kupandisha Vyeo na madaraja Watumishi 198,215, kutoa ajira zaidi ya 40,000 ndani ya Mwaka Mmoja, kulipa malimbikizo ya mishahara kwa Wafanyakazi 75,000 kwa Bilioni 124.3 na mengine mengi sana. Pata sasa Nakala yako ya Gazeti letu hili usome mwenyewe namna Rais Samia alivyoupiga Mwingi kwa Wafanyakazi kwa kipindi kifupi sana cha Uongozi wake.

IMG-20220516-WA0026.jpg


IMG-20220516-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom