Alichofanya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Makonda kwa Pierre Mzee wa Liquid ni udhalilishaji na kinyume cha haki za binadamu

Cesar Saint

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
424
725
Nadhani kila mara hili limekuwa likijirudia kwa kijana mwenzetu Paul Makonda “Hekima ya uongozi “

Kwa mfano unaweza kuwa na mzazi asiye na mvuto wa sura na hata jamii yako ikampachika majina na kumtambua hivyo lakini si hekima wewe kwenda mbele za watu na kusema yale majina anayoitwa mama yako si kwakuwa si ukweli la hasha ila si hekima.
949019c787c7038898bcc6a5c4715006.jpg

Pierre leo alikuwepo pale kama wahamasishaji wengine walioalikwa hekima tu angetumia ndugu Makonda na kwa maneno machache kwa walengwa bila kumuhusisha moja kwa moja Pierre .

Yawezekana amepata umaarufu kwa tabia isiyo nzuri ila matokeo yake amefanya mambo machache mazuri mpaka hili la hamasa ya tokomeza zero akahusishwa.

Hakumtendea vyema ndugu Pierre leo

Video ya Makonda akimdhalilisha Pierre

Habari zaidi, soma=>https://www.jamiiforums.com/threads...wake-kama-katiba-inavyoelekeza.1567031/unread

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumuona binadam mwenzio wa hovyo kisa anatumia kilevi na kimempa umaarufu huo ni upungufu wa hekima...

Mtoa mada ambaye sio wa hovyo tuone kama utapata promo baada ya tangazo la shemej ako bashite...

Mda mwingine unajiuliza hvi hii mbegu inatumia akili kweli kufikiri??.. utamuitaje binadam mwenzio “hovyo” mbele ya umat wa watu na unaye umekaa naye hapo?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nadhani kila mara hili limekuwa likijirudia kwa kijana mwenzetu Paul Makonda “Hekima ya uongozi “

Kwa mfano unaweza kuwa na mzazi asiye na mvuto wa sura na hata jamii yako ikampachika majina na kumtambua hivyo lakini si hekima wewe kwenda mbele za watu na kusema yale majina anayoitwa mama yako si kwakuwa si ukweli la hasha ila si hekima.

Pierre leo alikuwepo pale kama wahamasishaji wengine walioalikwa hekima tu angetumia ndugu Makonda na kwa maneno machache kwa walengwa bila kumuhusisha moja kwa moja Pierre .

Yawezekana amepata umaarufu kwa tabia isiyo nzuri ila matokeo yake amefanya mambo machache mazuri mpaka hili la hamasa ya tokeza zero akahusishwa.

Hakumtendea vyema ndugu Pierre leo

Sent using Jamii Forums mobile app
Unafiki mtupu, mbona kwenye uhamashishaji wa timu ya taifa pierre alimtumia na yeye alikuwa mwenyekiti, ukiona hivi ujue kamdhulumu, kitu cha kawaida awamu hiii
 
Kwakweli nimemkubali sana makonda kwa kile alichokemea media na waandishi kutoa promo kwa walevi na wababaishaji kama dr shika.
Sasa naelewa kwanini magufuli alimteua.
Pongezi sana Rais wetu magufuli kuchagua viongozi makini

Sent from my iPhone using JamiiForums
Acha wivu,wewe ambaye siyo wahovyo umetusaidia nini waTanzania!tupige kura sasahivi tuone Kati ya makonda na Pierre liquid nani atapata wafuasi wengi,acheni wivu wakike, liquid atabaki kuwa juu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu mwenyewe alimstili KAHABA, elewa neno KAHABA, walipomleta mbele zake ili wampige MAWE, Yesu aliwaambia, Ambaye anajiona ni MSAFI awe Wa kwanza kumtupia JIWE,...MAKONDA kamtupia JIWE Pierre! jiwe la kumuona Wa HOVYO...
 
2019-03-31_05.45.45.jpg
"watu kama wakina Pierre sijui,watu wa hovyo hovyo ndio wanakua maarufu watu wa maana hawajulikani,tunajenga jamii ya watu gani?"

Haya ndio maneno ya Makonda wakati anahutubia kwenye tamasha la tokomeza zero Kisarawe,lililofanyika jana Mlimani City,ambalo pia Pierre alikuwa moja kati ya watu waliohudhuria.

Hivi mtu kama Pierre kuwa maarufu yeye inamuuma nini? anaposema ni mtu wa hovyo katika lipi? kati ya Pierre na hao wasanii wake ambao daily wanshinda makahamani kwa kesi za hovyo hovyo,wanatukanana mitandaoni live, wanavujisha picha za ngono mitandaoni, wanabadili wanawake/mabwana kila uchwao na bado anawahusudu na kuwaona wa maana nani ni wa hovyo sasa?

Muache mzee wa watu aingize kipato chake kihalali, ilimradi havunji sheria za nchi.
 
Yesu mwenyewe alimstili KAHABA, elewa neno KAHABA, walipomleta mbele zake ili wampige MAWE, Yesu aliwaambia, Ambaye anajiona ni MSAFI awe Wa kwanza kumtupia JIWE,...MAKONDA kamtupia JIWE Pierre! jiwe la kumuona Wa HOVYO...
Kwa maneno yako mwenyewe alitakiwa atokee mtu aulize "Ambaye hajawahi kuwa wa Ovyo" asimame amshambulie Pierre Konki!! Hapo ndipo Muandaaji (Jokate) angekumbuka picha zake za Uchi zilizozagaa mitandaoni, Albert Bashite angekumbuka Zero alizopata mara 2 hadi kununua cheti cha Paulo Makonda na kukituia kujiendeleza na huku kampeni ikitaka kutokomeza zero. Hakuna ambaye angemkashifu mwenzake na sherehe ingemalizika kwa amani bila kukwaza mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom