Alichofanya Joseph Fritzl, hata shetani asingethubutu

Siri ya ulimwengu usioonekana ni beyond our thinking...

Kwa hali ya kawaida kabisa kitu hiki mwanadamu wa kawaifa hawezi kabisa kufanya...ni sawa na baba anayembaka binti yake wa miaka 3...

Haya mambo hayana majibu kwa ulimwengu wetu huu unaoonekana.

Lazima kuna msukumo unaofanilisha mambo haya...kifupi ni roho za mababu...roho za kiukoo zenye kila aina ya laana zinazo kushukia na unakuwa huna choice u need to do it...either u like it or not..roho zinakamata nafsi yako bila ridhaa yako na unafanya chochote zitakazo zenyewe..kiwe kizuri ama kibaya.

Kwa akili ya kawaida kabisa utamwona huyu jamaa si mzima kichwani....

Mambo haya ya laana za familia huwa zinazoibuka baada ya vizazi kadhaa ...unakuta familia ina wasagaji ama mashoga, majambazi, ma changu, mavivu ya kazi..nk

Kuua laana hizi ni kazi kubwa mno!! Ni ma roho yanayoishi katika familia husika na yanakuwa na amri kuu juu yenu.


Hiyo ^whether you like it or not^ umeharibu ^car-bee-sir^ yaani. No one can be successfully forced to do what they do not want or like. Ukiona umefanya kitu, jua umeridhia. Ule usemi kwamba huwezi kumlazimisha punda anywe maji, japo umemburuza hadi kumto, unahusika sana hapa. Lastly, siyo ngumu kuondoa hizo laana, kama usemavyo. People must be taught kuhusu right & wrong; God & the Devil. Halafu wafundishwe kumpenda Mungu na kumchukia Shetani na matendo yake yoooote. That's it!
 
Kijue kisa cha bwana Josef Fritzl, baba mzazi aliyemshikilia bintiye mateka kwa miaka 24, bila kuona jua wala mwanga wake, akambaka zaidi ya mara 3000 na kumzalisha watoto 7 huko nchini Austria. Ukishangaa ya Mwafrika; utastaajabu ya Mzungu.

Ilikuwa ni kipindi cha majira ya joto cha mwezi Agasti 1984. Mwaka na mwezi ambao Prince, msanii wa RnB na Pop wa Marekani alikuwa anaachia kibao chake cha "Purple Rain" kilichotikisa Dunia. Mwezi na mwaka ambao Thomas Sankara, Rais wa Burkina Faso, alikuwa anabadili jina la nchi hiyo ya Burkina Faso kutoka Upper Volta. Na hasa ndio mwezi na mwaka ambao binti wa miaka 18, Elizabeth Fritzl, alianza kuishi maisha ya kuzimu aliyoingizwa na baba yake mzazi.

Katika kipindi hicho cha majira ya joto, wakiwa peke yao katika viunga vya bustani ya nyumba ya bwana Fritzl huko nchini Austria katika mji wa Amstetten, alimwita bintiye(Elizabeth) ili amsaidie kushika mlango aliokuwa anautengeneza katika nyumba ya chini(handaki). Kama ilivyo imani ya mtoto kwa baba, huwa ni kubwa sana, na hakuwa na mawazo mengine zaidi ya "huyu ni baba", na anajihisi yu salama. Basi akashuka ngazi ili amsaidie.

Bila kujua masikini! Elizabeth alikuwa anasaidia kushika mlango wa jela yake ambayo aliishi kwa robo karne. Ndivyo wanavyosema waswahili, "Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa kiza". Hakujua masahibu yanayofuata dakika chache mbele. Naam, ilikuwa ni dakika chache tu, baadaya kumaliza kumsaidia baba yake, akitaka kupanda ngazi kutoka, kitambaa kinyevu kilicholowekwa kenye dawa aina ya 'ether' kilishindililiwa puani na mdomoni mwake. Alilala. Alopozinduka alijikuta katika jela ya madhira.

Ilikuwa ni mwazo wa maisha mengine, ambayo hata wewe msomaji katu hutopenda kuyapitia. Maisha yasiyo na uhuru na ya hovyo. Baba yake alimfungia humo kwa miaka 24 bila mtu kujua, si polisi waliokuwa wanahaha kupeleleza na kumtafuta, si ndugu na jamaa, wala mkewe Rosemarie (mama yake Elizabeth) aliyeweza kujua. Aliyejua Elizabeth yupo wapi ni bwana Fritzl tu. Na huyu Fritzl ndiye aliyewaambia ndugu na polisi kuwa Elizabeth amekwenda kujiunga na makundi maovu 'cults'. Kwa maana si mara moja aliweza kutoroka na kujiunga na rafiki zake katika maisha ya ujana mjini Vienna, ila aliweza kurudishwa na baba yake, au mara nyingine na polisi. Hivyo, baada ya Fritzl kusema ametoroka kujiunga na makundi maovu ya rika lake, kila mmoja aliamini, na hakuna aliyeweza kutilia shaka yupo katika handaki.

Ndiyo, Elizabeth alikuwa handakini huku juu polisi na ndugu wakimtafuta. Handaki ambalo bwana Fritzl alijenga bila vikwazo vyovyote. Ilikuwa ni rahisi sana kujenga nyumba za chini au handaki nchini Austria, ilikuwa ni kawaida, na mamlaka za serikali walitoa ruhusa bila vikwazo. Kwanini ilikuwa rahisi? Ni kipindi cha fukuto la vita baridi Duniani, na hususani vilivyogusa Ulaya, na Austria ikiwemo, japo ilikuwa huru kujiamulia iwe upanda upi.

Ni vita iliyoipasua Dunia pande mbili -za kibepari na kijamaa, na kuleta tahadhari kubwa, kwani watu walipata funzo kutoka vita mbili za moto za Duniia zilizotangulia.Na nchi hiyo ndogo ilikuwa kama kituo cha kimkakati. Basi kutokana na hili, watu nchini humo kujenga mahandaki kwa ajili ya silaha na vyakula ilikuwa kawaida. Hata Fritzl alopoomba kibali mwishoni mwa miaka ya 1970, hakunyimwa, na zaidi alifadhiliwa na serikali za mji kujenga handaki hilo , ila hakuna aliyejua alikuwa na lengo gani.

Aliajiri mtu wa kuchimba shimo kubwa kwa ajili ya ujenzi. Mtu ambaye alikaa viungani mwake kwa siku 30. Majirani walikuwa na wasiwasi walipoona mtu akitoka na vifusi vya udongo juu ya toroli, ila hakuna aliyeweza kuuliza, kutokana na ukali wake ambao kumuadhibu mkewe au watoto ilikuwa kawaida.

Hakupata shida kuchanganya zege imara, alitumia ujuzi alioupata katika makampuni ya ujenzi alikokuwa ameajiriwa. Hivyo alichanganya zege imara na kuliweka juu ya vyuma. Akiwa na elimu ya uhandisi wa umeme, alisuka mlango mzito wa kutumia "remote control". Na ili uweze kuufikia mlango huo na kuweza kuingia ndani, ilibidi ufungue milango mingine nane ya kawaida. Na humo ndani mlikuwa na bafu, choo, jiko na chumba cha kulala, na kukiwa na vizuizi vizito vya sauti "sound proof". Humo ndimo alimokuwemo Elizabet.

Mwaka mmoja mbele, ili kuua wasiwasi waliokuwa nao majirani juu ya vifusi vilivyokuwa vikibebwa na yule mchimbaji, alijenga bwawa kubwa la kuogelea "swimming pool" juu ya handaki hilo alimokuwamo bintiye ili watu waliokuwa na mashaka ya; tani na tani za vifusi vilivyokuwa vinabebwa na toroli, wajue vimetoka hapo katika bwawa.

Maskini, ndugu walikuwa wakijivinjari kwa kuogelea juu ya bwawa hilo, wasijue wanaogelea juu ya binti yao aliye ardhini futi sita. Na labda unaweza kujiuliza, kwanini mkewe, Rosemarie hakuweza hata kuhisi au kwenda kwenye nyumba hiyo ya chini? Vyanzo mbalimbali vinasema bwana Fritzl alikuwa ni mkali na katili aliyekuwa anampiga mkewe mara kadhaa na kutishia kumuua, jambo ambalo lilifanya Rosemarie asifuatilie kabisa mambo ya mumewe. Na hata kipindi cha nyuma, bwana Fritzl aliwahi kumbaka bintiye (Elizabeth) akiwa na miaka 11 na mkewe akajua, lakini hakuwahi kutoa taarifa kokote kuhofia maisha yake. Ukatili wake, ndio uliomfanya asifuatilie mambo yake. Na hata mawazo ya kushuku kuwa bintiye anaweza kuwa handakini, hakuwa nayo.

Siku ya kwanza tu, alipofungiwa huko chini, alifungwa na mnyororo kwenye mikono yake iliyofungwa pamoja kwa nyuma, kisha mnyororo huo kufungiwa kwenye tendegu la kitanda cha chuma. Hakuweza kujongea zaidi ya mita moja. Baada ya siku mbili, alimpa zaidi uhuru wa kujongea baada ya kuifungua mikono yake na kuufunga mnyororo huo kiunoni mwa bintiye. Si kwamba alifanya hivi kwasababu alikuwa anamuonea sana huruma bintiye, la hasha, alitaka afaidi vizuri penzi lake bila bughudha yoyote.

Maisha ya Elizabeth huko chini yalikuwa magumu mno! Unyevu usiokwisha ulichuruzika ukutani ukitoka katika bwawa la kuogelea lilijengwa juu na aliufuta kila siku kwa mataulo, panya waliokuwa wengi ambao alilazimika kuwashika wengine na mikono, na upweke katika miaka mitano ambayo alifikiria kujiua mara kadhaa kabla ya kupata mimba na kupata mtu wa kumliwaza na kuachana na mawazo ya kujiua.

Huku juu dunia iliendelea kujizungusha katika muhimili wake sanjari na kulizunguka jua; siku na miaka ilikwenda wakati Elizabeth akiwa ardhini akiwa hana siku wala miaka. Matukio makubwa yalikuwa yanatokea, kama: kuanguka kwa ukuta wa Berlin, kuvunjika kwa umoja wa Kisovieti, kuachiliwa huru kwa Nelson Mandela, mauaji ya Kimbari Rwanda, tukio la kigaidi la septemba 11 nchini Marekani, na mengine mengi. Hakuweza kujua kinachoendelea. Zaidi matukio makubwa kwake ilikuwa ni kubakwa kila siku na baba mzazi ambaye alidhani ndiye mlinzi wa kwanza wa maisha yake.

Alibakwa mara nyngine, zaidi ya mara moja kwa siku. Alioneshwa filamu za ngono na akaamuriwa amfanyie kile anachokiona humo. Naam, ni baba mzazi ndiye alikuwa anafanya haya kwa mwanaye wa kumzaa.

Baada ya miaka mitano ya upweke, alipata mimba ya baba yake na kuzaa mtoto wa kwanza wa kike aliyeitwa Kerstin. Alijifungua katika mazingira magumu na yasiyo salama kabisa. Hakuwa na msaada wala akili juu ya masuala ya uzazi, zaidi alipewa mkasi na kitabu chenye dondoo za uzazi ili kimuongoze.

Kerstin alikuwa mtoto wa kwanza kwake, na hakuishia hapo, bali alizaa watoto saba na baba yake. Huku kazi kubwa ya bwana Fritzl ilikuwa ni kumbaka na kuleta chakula kilichokuwa kinatunzwa kwenye jokofu. Maisha ya kiafya yalikuwa ni magumu sana. Mara nyingine bwana Fritzl aliweza kumuadhibu bintiye kwa kumzimia taa. Mwanzoni Elizabeth alikuwa analia sana, ila miaka inavyokwenda alizoea.

Alifanya majaribio kadhaa ya kutoroka bila mafanikio. Fritzl alipogundua alimtisha kuwa amefunga shoti ya umeme mlangoni, na hata akijaribu kutoroka atamuua na wanawe papohapo kwa sumu kali. Licha ya mara nyingine kupiga kelele za kuomba msaada, hakuna ambaye angeweza kusikia kutokana na "soundproof' nzito iliyokuwa imefungiwa humo.

Mnamo mwaka 1996, akiwa amepata uzazi mwingine na kujifungua mapacha; pacha mmoja aliyepewa jina la Michael alifariki akiwa na masaa 66 tu. Alifariki kutokana na matatizo ya kupumua - alishindwa kupumua vizuri. Hivyo baba yake alimchukua mtoto huyo na kumyeyusha kwa dawa.

Bwana Fritzl aliwapandisha watoto watatu - wadogo juu ili wakalelewe na mkewe Rosemarie. Alichofanya, alimlazimisha Elizabeth huko chini aandike barua kuwa yeye ameshindwa kuwalea na hivyo amemuachia yeye na mama yake wawalee na yeye anaendelea vizuri hivyo wasimtafute. Elizabeth alifanya hivyo. Hivyo alipanda nao juu kwa siri akiwa na kipande cha barua ya bintiye. Mbinu aliyotumia, ni kuwatelekeza hapo jirani na nyumba yake sanjari na kipande hicho cha barua, alafu akajifanya kwanza ndio anawaona huku wakiwa na ujumbe huo wa kuwalea watoto hao ambao Elizabeth alishinikizwa auandike. Rosemarie, mkewe aliamini, na hivyo kuanza kuwalea wajukuu hao wa mke mwenza(mtoto), asijue kinachoendelea. Ijapokuwa polisi walipokuja, bado hawakuweza kutilia shaka moja kwa moja, lakini walikuwa na wasiwasi na jambo hilo, waliendelea na upelelezi wao.

Kupokonywa watoto wake watatu na kupandishwa juu, kulimpa Elizabeth simanzi kubwa, lakini moyoni alijua watakwenda kupata maisha mazuri kuliko hao aliobaki nao chini ya ardhi ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Habari iliyokuwepo Austria kwa wakati huo, ni kupotea kwa binti huyo, ambapo polisi na ndugu walishindwa kumpata. Licha ya upelelezi mkali, lakini hakuna aliyeweza kutilia shaka kuwa yupo ardhini, katika viunga vya nyumba ya baba yake.

Hatimaye ilifika wakati. Ilikuwa ni tarehe 19 ya mwezi Aprili, 2008 baada ya miaka 24, ndipo Elizabeth aliuona uso wa dunia kwa mara ya kwanza. Inawezekana haikuwa mipango ya bwana Fritzl, bali wakati ulifika tu, na hakuna mwenye mabavu ya kushindana nao. Ni siku ambayo mtoto wa kwanza- mkubwa, wa Elizabeth na baba yake, Kerstin aliyekuwa na miaka 19, alikuwa anaumwa mahututi. Ndipo Elizabeth akamuomba baba yake ili apelekwe hospitali. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, bwana Fritzl alishikwa na huruma.

Hivyo, Fritzl alimuamuru Elizabeth amsaidie kumbeba Kerstin kupanda naye juu. Na ndio kwa mara ya kwanza Elizabeth anauona uso wa dunia, ila aliamuriwa arudi tena chini punde tu baada ya kumsaidia, na milango ikafungwa. Akampakia Kerstin kwenye gari yake aina ya Marcedes na kumpeleka hospitali ya jirani. Hapo hospitali kukaibuka jambo jipya, nalo ni wasiwasi wa Madaktari na Manesi juu ya tukio hilo la kupotea kwa Elizabeth lililoripotiwa miaka kenda na vyombo vya habari.

Kwanza, madaktari walishtuka kupokea kiumbe kilichokuwa na muonekano mbovu wa mpangilio wa meno na kikiwa na matunzo hafifu. Pili, walikuwa wanajua kisa kizima cha kupotea kwa binti wa bwana Fritzl kilochokuwa kimeripotiwa mara nyingi katika vyombo vya habari. Hivyo, baada ya Fritzl kusema mtoto huyo ni wa Elizabeth ametelekezwa kama wale wengine, madaktari wakamkatalia, wakamwambia hawawezi kumpa matibabu hadi mama yake awepo.

Mpango mzima wa Fritzl, ulikuwa ni kumfungulia bintiye bila kuzua maswali ambayo wangeweza kumshuku kwa kumshikilia. Kwani alikuwa na mpango huo miaka ya karibuni kutokana na umri kusogea sana, hivyo aliona ni vema kuziweka familia zake karibu. Lakini sasa mpango huo uligonga mwamba, hivyo hakuwa na budi kumuachilia bintiye ili aende hospitali kwa mwanaye.

Hatimaye, kwa mara ya kwanza Elizabeth aliyepotea miaka 24 iliyopita alijitokeza katika uso wa dunia akiwa mwanamke wa umri wa miaka 42 na kuwastaajabisha watu. Jambo la kwanza akaambiwa atashitakiwa kwa malezi ya hovyo na ya kizembe kwa mwanaye aliyekuwa mahututi. Na neno zito la kwanza kutoka mdomoni mwa Elizabeth, ilikuwa: "Jamani nitakacho wasimulia hakuna atakayeamini hapa". Ila aliomba kabla ya kusimulia, ahaidiwe kutomtia tena machoni baba yake. Akaahidiwa na polisi. Aliwasimulia kisa chote kilivyokuwa. Siku hiyohiyo, Fritzl alikamatwa na kutiwa nguvuni.

Akafunguliwa mashitaka matatu; mauaji, ubakaji, kumshikilia bintiye utumwa. Kesi ikaendeshwa, na Fritzl akakana kosa la utumwa. Wakili wake, bwana Rudolf Mayer alijaribu kumtetea kwa kigezo kuwa Fritzl alifanya vile kwa nia ya kumlinda binti yake asijiunge na makundi maovu. Na akaongeza alikuwa alikuwa baba mwema, ambaye alitoa mahitaji yote na kuwanunulia watoto vitabu. Utetezi ambao ulitupiliwa mbali na mwaka unaofuata, 2009, bwana Fritzl akahukumiwa kifungo cha maisha katika jela maalumu ya makosa ya jinai iitwayo "Krems- Stein Prison", huku akiambiwa baada ya miaka 15 mbele anaweza kupata msamaha. Lakini hadi sasa bado yupo jela akiwa na miaka 84. Na taarifa zinasema, hali yake kiafya si nzuri, na yale matumaini aliyokuwa nayo ya kuwa huru siku moja yamefifia hivyo ananiona ni wa kufia humo.

Pia, mwaka 2016 bwana Josef Frizl amebadili jina lake la ukoo kwa kulipa serikali ya mji wake kiasi cha £465, na sasa anaitwa Mayrholf.

Mkewe Rosemarie alimkimbia, na hajawahi kwenda kumtembelea jela kutokana na madhira hayo. Na mwaka 2012 bwana Fritzl aliamua kuachana na mkewe.

Mwaka huo wa 2016, mwaka ambao alibadili jina lake la ukoo, aliuza nyumba yake kwa thamani ya £140,784 kwa Herbet na Ingrid Houska, ambao wameiboresha na kuipangisha kwa kiasi cha £700 kwa mwezi. Lakini sehemu ya chini(handaki) alikowekwa Elizabeth kwa miaka 24 bila kuona jua, hakutumiki ili kuepusha madhira.

Kwa sasa Elizabeth wanamahusiano mazuri na mama yake Rosemarie, kuliko hata alivyokuwa mdogo. Kwani mahusiano yao baada ya kutoka shimoni hayakuwa mzuri, kwani Elizabeth alihisi kuwa mama yake anashirikiana na baba yake na husususani alivyobakwa na akatunza siri, lakini haikuwa hivyo. Na Rosemarie anaendelea kuwalea wale watoto watatu wa Elizabeth, na wanafurahia mahusiano mazuri.

Kwa upande wa Elizabeth akiwa na umri wa miaka 52 kwa sasa, wanaishi huko mashambani kaskazini mwa Austria, Kijiji kilichopewa code za siri kikijulikana kama"Village X". Hakuna mtu yoyote anayeruhusiwa kufika eneo hilo, si waandishi wa habari wala nani. Hakuna picha inayoruhusiwa, na ndio maana hakuna picha za watoto wake, wala ya Elizabeth baada ya kutoka shimoni, zaidi ya ile aliyopiga na miaka 18. Ni eneo lonalolindwa na mamlaka za usalama za Austria. Na wamepewa mtaalamu wa masuala ya ushauri kazi yake ni kuwaweka sawa kiakili.

Kwa sasa, Elizabeth anaishi na mpenzi mpya ambaye ni mlinzi wake, bwana Thomas Wagner, ambaye wanapendana na anamlinda Elizabeth na wanawe watatu.

Kisa hiki cha kweli ni kama unatazama filamu ya kutisha hivi "Horror Movie". Ni kisa kilichoishangaza dunia, na pasi na shaka hata wewe unayekisoma kimekushangaza. Lakini je, umepata somo gani? Naamini kila mmoja amepata somo kwa nafasi yake, hususani kwa wazazi juu ya malezi na mazoea ya mtoto na mzazi.
#Sky_videos_production_tz
#Mr_camera_man

By Hillary A Silayo

View attachment 1715263View attachment 1715264

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Mara ya kwanza nimeuona utakatifu wa shetani.
 
Kuna wale wapuuzi wanasema mzazi hakosei au ni mungu wa duniani, wakamuambia huyo binti haya maneno.
 
Wakati mwingine mawakili ni wapumbavu kujaribu kutetea upumbavu kwa njaa za kipumbavu.

Wakili alijua VYOVYOTE VILE lazima mteja wake angefungwa miaka mingi jela kama siyo maisha; who in the world would not attempt kusekyua mali zileee given huyo jahili jambawazi alikuwa very rich!??? Usisahau kuwa uwakili ni ajira kama ajira zingine zitambulikazo kisheria, sawa!???
 
Ninamlaumu mke wa huyo jamaa! Alishindwa kutoa taarifa polisi!!
Nadhani uoga kwa kichapo na vitisho vya kuuliwa vilichangia na kwakua hakuwa na uhakika kama kafichwa humo ndani.

just imagine hayo maandalizi ya kujenga HANDAKI yalichukua mda gani?? na wakati wote huu kumbe mlengwa alikuwa Mwanawe
 
Hiki kisa nilikisikia bbc miaka ya nyuma huko.

Ila mawakili mbinguni watapasikia tu yani huyo mzee ni wakutetewa kweli!

Halafu huyo kima alikuwa na matumaini ya kutoka jela aende wapi tena🙄jinga kabisa afie hukohuko.
Anarudi uraiani kufanya mambo mengine:(:(:(
 
Back
Top Bottom