Alianza Kasesela kisha Diallo na sasa Mtaka. Je, kuna ombwe kubwa la uongozi?

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
7,298
9,524
Kuna ombwe la uongozi, pengine kila mtu anataka apitishe ajenda zake kwa nguvu.

Tunapoona viongozi wetu wanaamua kutoka nje hadharani wanatema nyongo, wanatukana, wanakosoa hadi raia tunashituka na kuwakanya waombe msamaha hakika kuna shida.

Ni muhimu mkatumia vikao maalum kuyachuja haya mambo na mkamaliza salama.

Ukitoka huku nje kuongea hautakosa wa kukuunga mkono na hata wa kukukosoa watakuwepo.

Madhara yake ni makubwa mno. Jamii inagawanyika bila kutarajia.

Msitangulize tamaa zenu. Tangulizeni jamii mnayoiongoza. Tangulizeni mshikamano na Amani kupitia nafasi mlizopewa.
 
Kwann mtu anapotoa hisia zake mnataka atoe hisia za kutukuza na kukubalika na watu wote?

Binadamu tumetofautiana, ukiona mawazo ya mwenzako yanakinzana na yako ujue huo ndio uhai na ubinadamu wenyewe

Kupishana kimawazo ni 'Devine power and God's mysterious'

Hamna kitu kizuri kama kutofautiana kimawazo, ni jambo la utukufu kwa Mungu

Wapo sahihi wanaotoa mawazo mbadala

Wasibugudhiwe
 
Seminar elekezi zilikuwa muhimu sana japo ziliondolewa sababu hakujua umuhimu wake.
 
Anthony Diallo na Anthony Mtaka wanaweza kuwa ni viongozi wachapakazi lakini siyo viongozi intelligents!
Hawajui wazungumze nini, wapi na wakati gani! Mtu intelligent anajua kwamba si kila jambo au ukweli fulani lazima usemwe hadharani!
Akili ambazo viongozi hawa wameonyesha ni za ki CHADEMA CHADEMA! Kauli zao hazina sense ya collective responsibility ndani yake!
Anthony Mtaka akiendelea na kutafuta cheap popularity ata sustain kwa muda mfupi sana! Diallo yeye mwisho wake tumeshauona!
 
Uko sawa kabisa mkuu,sikutarajia Kama Mtaka atafanya hayo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom