Ali Kiba: Sipigi tena playback, ni muziki wa live tu

Mbulu

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
5,620
5,510
Muimbaji wa ‘Chekecha’, Alikiba amesema kwa sasa hafanyi tena muziki wa playback bali ni live peke yake.

Akiongea na 255 ya XXL kupitia kituo cha redio cha Clouds FM, Kiba alisema siku si nyingi ataitambulisha bendi yake.

“Nimeamua kuacha kufanya muziki wa playback, na sio muda mrefu wataniona na bendi yangu na nimeshafanya mipango hiyo tayari bado tu kuitangaza,” alisema.

“Burudani ya show yangu yoyote ya Kiba itakuwa ni live band labda itokee tu bahati mbaya hiyo sehemu band haiwezekani. Kingine ukifanya na bendi unakuwa na uchungu zaidi na hela yako na kingine unakuwa serious zaidi yale sijui mambo ya mikono juu kidogo yanapungua.”
 
Nyumba ya jirani playback zinaendelea tu, live hatuwezi
 
Hongera yake,ila mi ningekuwa management yake nisingemshauri amiliki Band,ila kuimba live haina ulazima wa kumiliki Band kwa sababu kumiliki Band ni gharama mno maana sasa itambidi amiliki wapiga vyombo wasiopungua 8 waimbaji na wacheza show si chini ya 5 (kumbuka hawa utakuwa nao muda wote ili muwe munafanya mazoezi na mambo mengine) kwa hiyo kuna mambo ya mishahara na posho,unajua kitakachofuata ITAMBIDI AWE NA SHOWS ZA MARA KWA MARA TENA ZA SEHEMU MAALUM KILA SIKU FULANI UTAMKUTA HAPO unajua kitakachofuata HATOKUA NA MVUTO WA KUTAKA KUMJUA ANAKIPYA GANI KWA KUWA UKIENDA MAHALI FULANI UTAMKUTA akawaulize wakina Ally Choki,T.I.D,Banana Zorro. Hajiulizi kwa nn WASANII WA U.S. NA EUROPE WANAIMBA LIVE LAKINI SWALA LA KUMILIKI BAND KWAO HALIPO NA BADO PLAYBACK WANAIMBA. Ni ushauri tu si lazima auchukue, matusi yanakaribishwa kwa sababu nina degree kipengere hiko
 
I agree...

Back
Top Bottom