Ali Kiba na Abby Daddy waingia katika mgogoro mzito, WCB wahusishwa

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,078
12,379
Pengine 'Aje' inaweza ikawa nyimbo ya mwisho ya Ali Kiba chini ya producer Abby Dad ambaye ametengeneza nyimbo kadhaa za Ali Kiba.

Abby dad ametengeza hits kama [HASHTAG]#Nagharamia[/HASHTAG] [HASHTAG]#Chekecha[/HASHTAG] na [HASHTAG]#Aje[/HASHTAG] ambazo zilifanya vizuri sana.

Hivi karibuni ilikuwa inatarajiwa kuachiwa Aje remix ambayo ilipangwa kuachiwa November 29 siku ya birthday ya Ali Kiba, lakini habari zinazoendelea kusambaa ambazo zilianza kama masihara ila kwa sasa zinaanza kuaminika kutokana na taarifa za watu wa karibu, ni kwamba Abby dad nido anayechelewesha kutoka kwa Aje Remix na mpaka sasa amekataa kutia sahihi yake kwenye mkataba ili ngoma iwe released.

Abby dad anataka 50%/50% katika nyimbo ya aje ikiwemo katika show iTunes na mapato yatakay patikana anataka nusu kwa nusu.

Kuna taarifa kwamba WCB wanamrubuni Abby dad ili aachane na Kiba japo taarifa hizo sio confirmed. Hii ni baada ya Ku tengeneza 'kokoro'.

figisu_figisu.jpg

Prodyuza Abby dad..
 
Ulianza vizuri na nikawa nataka nimlaum abydad ila ulivo malizia na WCB nikajua hii BS na abydad ana haki ya kudai chochote.
Lakin si lazima kila kwenye tatizo la Kiba bas Diamond auhusishwe, hii imekuwa ni tabia ya mida mrefu ya Camp ya Kiba. Punguzeni basi kulalamika na kila tatizo kuonesha nyie hamna kosa bali ni domo. Deal with it.
 
Baada ya kokoro abydad amebadilika Sana kafuta hadi promo ya aje remex kaanza new life
 
Ali Kiba hawezi kutikiswa na Abydad,Ali Kiba ni brand huyo Abydad ni nani?

Maproducer wapo kibao tu,tena huwezi kufananisha ngoma alizotengeneza Man Walter (Mwana & Dushelele) na hizo alizotengeneza yeye.

Alizingua Akhenato mpaka tukaogopa kumpoteza Kiba ila hakufua dafu ijekuwa yeye?

Kiba atabaki kuwa Kiba.
Period
 
Mkuu pwilo,

Umekosea sana kumuhusisha Simba na tofauti iliyopo kati ka kiba na aby daddy! (Kama tofauti zao zimekuwa kubwa kiasi hicho)

Kuhusu wimbo wa kokoro:
Wimbo huu haujarekodiwa juzi juzi kama unavyodhani.. Wimbo umerekodiwa kabla mavoko hajamwaga wino rasmi wcb (ndio walikuwa kwenye mazungumzo)

Kwahiyo kipindi mavoko ameingia rasmi wcb tayari alikuwa na huu wimbo ukiwa umeingizwa verse moja tayari na ulikuwa na chorus tofauti kidogo na hii chorus ya sasa (zinafanana kidongo ingawa).
Na ieleweke kuwa mavoko pia anazo nyimbo nyingine nyingi hazijatoka zimerekodi kabla hajaingia wcb!

So miezi kama miwili iliyopita baada ya kukubaliwa kuwa wimbo huu utoke na kufanyiwa video, kilichofanyika ni kuurekebisha kiasi na kuuboresha... Ndio hapo Simba akaingiza verse yake na kuingiza sauti kwenye chorus.. Kisha Laizer akaujazia vionjo vichache na kuufanyia 'mastering'..
Hicho ndicho kilichofanyika..

Si sawa kumuhusisha Diamond na kila kitu cha Kiba kinachoenda kombo!
Kwa niaba ya mashabaki wote wa Diamond platnumz na WCB, tuwaoombee heri Kiba na Abby Daddy wafikie muafaka na waendelee na kazi.. Tunahitaji wasanii wengine waongezeke kuiwakilisha Tanzania kimataifa! Kiba kukosana na Abby daddy ni setback na sio suala linalosogeza mziki wetu..

The Bold.
 
Watu hawawezi kuishi bila kupost hawa watu wawili.... fanyeni ya kwenu.
 
Tunampa ofa ya kurekodi ngoma moja na Laizer, tunajua anataka ila anashindwa kusema.. Mpeni taarifa # aje wasafi studios wala asiogope
Sidhani kama hata ana wazo hilo,yeye baada ya kutoa idhini ya Kamwambie irekodiwe Sharobaro haitaji anything in return.
Huyo ndiye Ali Kiba
 
Mkuu pwilo,

Umekosea sana kumuhusisha Simba na tofauti iliyopo kati ka kiba na aby daddy! (Kama tofauti zao zimekuwa kubwa kiasi hicho)

Kuhusu wimbo wa kokoro:
Wimbo huu haujarekodiwa juzi juzi kama unavyodhani.. Wimbo umerekodiwa kabla mavoko hajamwaga wino rasmi wcb (ndio walikuwa kwenye mazungumzo)

Kwahiyo kipindi mavoko ameingia rasmi wcb tayari alikuwa na huu wimbo ukiwa umeingizwa verse moja tayari na ulikuwa na chorus tofauti kidogo na hii chorus ya sasa (zinafanana kidongo ingawa).
Na ieleweke kuwa mavoko pia anazo nyimbo nyingine nyingi hazijatoka zimerekodi kabla hajaingia wcb!

So miezi kama miwili iliyopita baada ya kukubaliwa kuwa wimbo huu utoke na kufanyiwa video, kilichofanyika ni kuurekebisha kiasi na kuuboresha... Ndio hapo Simba akaingiza verse yake na kuingiza sauti kwenye chorus.. Kisha Laizer akaujazia vionjo vichache na kuufanyia 'mastering'..
Hicho ndicho kilichofanyika..

Si sawa kumuhusisha Diamond na kila kitu cha Kiba kinachoenda kombo!
Kwa niaba ya mashabaki wote wa Diamond platnumz na WCB, tuwaoombee heri Kiba na Abby Daddy wafikie muafaka na waendelee na kazi.. Tunahitaji wasanii wengine waongezeke kuiwakilisha Tanzania kimataifa! Kiba kukosana na Abby daddy ni setback na sio suala linalosogeza mziki wetu..

The Bold.

mtani una cheo gani wcb
Ni mkuu wa kitengo cha propaganda na fitna, same as those found at Lumumba n Ufipa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom