Ali Karume kugombea urais Zanzibar 2010

Teamo

JF-Expert Member
Jan 9, 2009
12,272
1,034
Chanzo: TBC1 News (saa mbili usiku)

Balozi huyu WA TANZANIA ITALIA ni miongoni mwa wanaowania KWA RIDHAA YA UONGOZI WA CHAMA kinyang'anyiro cha urais huko visiwani. Amekiri wazi kwa kinywa chake.

CHANGAMOTO: Urais Zanzibar ni "ufalme''?
 
.....Karume Dokta si anataka kubadili katiba ili agombea muhula mwingine tena?
 
Kila binadamu ana haki ya kutaka uongozi katika jamii yake, ingawa ni kweli itafanana na ufalme na kuonyesha kwamba nje ya familia ya Karume thinkers wa level ya rais hawapatikani. Yeye kama Karume (Ally) hana kosa katika hili tutakachoona kwamba ni kituko ni pale ambapo CCM watampitisha.kama mgombea.
 
kwakweli ndivyo ilivyo
 
Hapana sasa inakuwa kam vile ilivyokuwa Marekani mkuu, inatupsa kuchagua watu wengine mkuu wangu,
zanzibar hakuna mwingine(KWA MTIZAMO WA HARAKA HARAKA)....

au uniambie ungependa awe nani?
 
Sasa hawa jamaa wanataka kukifanya kisiwa ni cha familia? au wanadhani wengine hawawezi kuongoza. Anyways, waache wakirudishe kisiwa katika enzi za umwinyi na usultani na kama kawaida mawe yatawaondoa tu!
 
Kwa hakika Ali Abeid Amani Karume, bila ya kujali jina lake, anayo haki ya msingi ya kikatiba, kugombea nafasi yoyote katika nchi yake ya Tanzania kama alivyo na haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi yeyote anayemtaka. Ni unyanyashaji na ubaguzi wa hali ya juu sana kumnyima haki yake hiyo.

Kama wananchi wataona kuwa hafai kwa sababu moja au nyingine basi wasimpe kura zao wakati wa kura za maoni au za uchaguzi rasmi wenyewe. Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni.
 
Hata sishangai ni uhuru wa maoni ndo unakuongoza!
 
Kwa hakika Ali Abeid Amani Karume, bila ya kujali jina lake, anayo haki ya msingi ya kikatiba, kugombea nafasi yoyote katika nchi yake ya Tanzania kama alivyo na haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi yeyote anayemtaka. Ni unyanyashaji na ubaguzi wa hali ya juu sana kumnyima haki yake hiyo.

Kama wananchi wataona kuwa hafai kwa sababu moja au nyingine basi wasimpe kura zao wakati wa kura za maoni au za uchaguzi rasmi wenyewe. Mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni.
sisi wazanzibari tunaona anafaa.na kwakweli hakuna mwingine zaidi yake
 
Tuachane na dhana ya kuwaabudu hawa watu walio kwenye uongozi ambao wanafikiri hakuna anayeweza kuongoza nchi isipokuwa wao.
Wajitokeze Watanzania walio na uwezo wa uongozi ambao bado hawajatumia nafasi yoyote katika uongozi kwa maana nyengine tunahitaji fresh blood.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom