Ali Karume Aanza Kampeni za Urais Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ali Karume Aanza Kampeni za Urais Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Jul 26, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  BALOZI wa Tanzania nchini Italia ambaye pia ni mtoto wa rais wa kwanza wa Zanzibar, Ali Abeid Karume ameanza kampeni za kuwania kiti cha urais wa Zanzibar kumrithi kaka yake Rais wa sasa wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume.

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa Balozi huyo, ambaye kwa sasa yupo hapa nchini, ameanza kampeni za kusaka kuungwa mkono na baadhi ya watu muhimu ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Hata hivyo, katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, alisema hakuenda Dodoma kwa ajili ya kujifanyia kampeni bali yeye kama Mkuu wa Mabalozi wa Tanzania Nchi za Nje, alienda kama mtaalamu ambaye angeweza kuhitajika wakati wowote kusaidia kutoa ufafanuzi wakati bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikijadiliwa.

  Mwaka 2005 Balozi Ali Karume alikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM ambao walikuwa wakiwania kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano ambapo Rais Jakaya Kikwete alishinda nafasi hiyo.

  Katika kampeni zake Karume amekuwa akitamka bayana kuwa atajitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kugombea Urais visiwani humo kuchukua nafasi ya kaka yake Amani Karume ambaye anamaliza muda wake wa urais Novemba 2010, baada ya kuongoza kwa miaka 10.

  Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, mtu yeyote akichaguliwa nafasi ya rais, haruhusiwi kuongoza kwa zaidi ya miaka 10.

  Akiwa mjini Dodoma, Balozi Karume alikutana na wabunge mbalimbali wa CCM, miongoni wakiwamo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) pamoja na Kamati Kuu ya chama hicho (CC).

  Mwananchi lilimshuhudia akifanya mazungumzo na viongozi mbalibali wenye ushawishi ndani ya chama katika viwanja vya bunge.

  “Ni kweli amekutana nami, lakini mambo haya yalikuwa mazungumzo baina yangu naye na ameniomba nimuunge mkono kwa vile atagombea Urais wa Zanzibar. Nilimsikiliza sasa kama nitamuunga mkono ama laa hiyo ni juu yangu” alieleza mmoja wa viongozi ambaye alikutana na Karume na kuombwa kumuunga mkono kwa sharti la kutotajwa jina.


  Mwananchi Jumapili lilipowasiliana kwa njia ya simu na Karume, alisisitiza ukweli wa nia hiyo ya kuwa rais wa Zanzibar kipindi kijacho, lakini akakanusha kuwa alienda Dodoma kufanya kampeni.

  "Hiyo siyo kweli kabisa. Napenda kwanza ufahamu kuwa mimi ni Mkuu wa Mabalozi wote wa nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Karume akifafanua:

  "Mimi nilienda kule kuona jinsi mijadala ilivyokuwa inaendeshwa na pili nilikuwa kama mshauri iwapo lingejitokeza suala linalohusu mambo ya kibalozi wakati inajadiliwa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa."

  Alibainisha kuwa kama ni suala la kampeni basi angelifanya wakati ambapo mkutano wa NEC au CC unakaribia.

  Alipotakiwa kueleza kama haoni kama akichaguliwa Itaonekana uongozi wa Zanzibar ni wa kupokezana kama ule wa Kisultani, alipinga akisema utawala wa namna hiyo kwa kawaida baba humrithisha mwanaye na siyo ndugu.

  "Nalizungumzia hili kwa sababu wengi wamekuwa wakilihoji. Kama ungekuwa ni utawala wa namna hiyo basi Rais Amani angemrithisha mwanaye. Tena anao wakubwa na wenye uwezo wa kupewa nafasi iwapo utawala ni wa namna hiyo."


  “Anasema utawala wa kurithi ni ule wa baba kumuachia mtoto uongozi na kueleza kuwa hakuna urithi wa utawala kutoka kwa kaka kwenda kwa mdogo mtu, hivyo uamuzi wake wa kugombea usitafsiriwe katika maana hiyo,” alieleza Mbunge mmoja huku akimnukuu Balozi Karume maelezo yake.

  Amekuwa akieleza kuwa kugombea ni haki alisema kuwa yeye anagombea kwa sababu anajua anao uwezo hasa ikizingatia kuwa, ana elimu ya kutosha pamoja na uzoefu mkubwa wa kimataifa.

  "Mimi ni Mzanzibari mwenye uzoefu wa muda mrefu wa uongozi ndani na nje ya nchi. Nimekuwa Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda kwa miaka sita. Nina elimu ya kutosha, nimesoma Marekani taaluma ya siasa na uchumi. Ninayo shahada ya uzamili.

  "Nimekuwa na uzoefu wa uongozi kimataifa kwa kuwa balozi wa Tanzania nchi mbalimbali na sasa mimi ni Mkuu wa Mabolozi wa Tanzania nchi za nje."

  Kutokana na hali hiyo alisema amejiona ana sifa zote za kuwaongoza Wazanzibar na amekusudia mambo mengi yenye manufaa kwao.


  Uchunguzi unaonyesha kuwa hata baadhi ya wabunge wanamuunga mkono kwa kile wanachoeleza kuwa katiba ya nchi inampa haki ya kuchaguliwa kiongozi mtu yeyote bila kubagua kuwa ni mtoto au ndugu wa kiongozi aliyewahi kushika wadhifa huo.

  Cha msingi, baadhi ya wabunge hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe, walisema kuwa jambo la muhimu ni kama katiba inamkubali na pili ni sifa zake za uongozi.


  Karume alipoulizwa juu ya vuguvugu la kero za muungano ambalo linaashiria kuuvunja, alisema anaheshimu sana mambo yote yaliyoasisiwa na baba yake, Abeid Karume.

  Hivyo, akasema akiwa rais moja ya mambo ambayo atayalinda kwa nguvu zote, la kwanza ni kutetea mapinduzi hadi dakika ya mwisho na pili ni kulinda muungano.

  Alisema chokochoko za muungano ni za kawaida kwa sababu popote duniani ambako kuna muungano wa nchi na hata majimbo, malalamiko ya hapa na pale hayakosekani.

  "Hata Tanganyika ilipopata uhuru, baadhi ya mikoa kama vile kule Rukwa, walilalamika kuwa hawapati haki… Hata kule Marekani ambako kuna muungano ambao unaonekana kuwa imara, yapo majimbo ambayo yanalalamikia muungano," alibainisha Karume.

  Kwa sababu hiyo alisema dawa si kuvunja muungano bali ni kutatua kero zinazojitokeza.

  Alipoulizwa kama tatizo ni muundo wa muungano ambao umezaa serikali mbili, alionya kuwa zikiundwa serikali tatu, mvutano unaweza kuwa mkubwa zaidi na kulisambaratisha taifa.

  Alisema kuwa muundo wa serikali mbili au moja, ndio unaoweza kuwa imara na wenye manufaa.

  Alisema kuwa Wazanzibar wengi wanaunga mkono muungano kwa sababu una manufaa mengi kwao.


  SOURCE: MWANANCHI
   
 2. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwani Viswani licha ya hii familia ya Karume hakuna wengine wanoweza kuwa raisi/mabalozi??
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kibaraka mwengine huyoooo on the making.
  Wazanzibari meli hiyooo!!
   
 4. m

  mswazi Member

  #4
  Jul 26, 2009
  Joined: Nov 18, 2007
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jamani Zanzibar ni ya Wanzanzibari wote, hatutaki utawala wa kindugu kama nchi ya Kifalme.
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Haya haya yalisemwa mwaka 2000, na hata chama tawala Zanzibar wakapendekeza mtu mwingine agombee baadaye tukashuhudia mizengwe huko Dodoma na mkaletewa mtoto wa rais wa zamani, bahati mbaya hamkuonyesha hasira zenu kwenye kura!

  Nafikiri huu ni ufalme na wataendelea kupokezana hadi yafanyike mapinduzi mengine.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa kama ni ya Wazanzibari wote kwa nini Ali Karume akataliwe, au yeye si mzanzibari?
   
 7. M

  Mtwike Senior Member

  #7
  Jul 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asema usultani hurithishana baba kwa mwana! hivi hajui hata historia ya anakojinasibisha! hivi barghash na majid na sijui humudi walikuwa baba/ mtoto au ndungu? hivi usultani wa saudiya ni wa baba/mwana au undugu? halijui hata historia ! zuzu! kweli alizaliwa unguja, lakini kaishi umri wake wapi, kasoma shule wapi? anajuwaje shida zetu? si jingine ni usultani tu! kesho mtasikia mtoto wa mzee ruksa naye atajiita mzanzibari! Udumu usultani! jana wa warabu leo wa mwafrika! kidumuuuu!!
   
 8. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilishawahi kusikia mama mzazi wa Rais wa Zanzibar alikuwa anamuomba Mungu amuweke ili ashuhudie wajuu zake wakishika madaraka ya Urais huko Zanzibar.
   
 9. C

  Chakarota Member

  #9
  Jul 26, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atleast huyu mama kakumbuka kumuomba Mungu lakini Baba wenu wa Taifa hakuweza hata kukumbuka kama kuna Mungu aliomuumba yeye ndio akasema kua atashuhudia serikali ya awamu ya 4 & 5
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu nitamfagilia kwa sababu mbili. Kwanza ni rafiki yangu na pili anataka kudumisha mwungano.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huyo kama anataka kuenda jela muacheni azoee anga hizi za Zanzibar Wazalendo wa Zanzibar wana hasira nae sana sana ,ila sishangai kwa CCM bara wauajio ndio wanaopewa kipau mbele.
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hiki ni kipindi cha watu wa mujini, mambo ya Kaskazini, Kusini ama Kisiwa cha pili waendelee kusubiri tu...
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kibs,
  Komandoo anarudi ikulu kwa miguu
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kazi kweli kweli!!!! Naoa hata shemeji yetu DJ Mansoor naye anautaka urais. Niliwahi kusema, ndugu zangu wa CUF wasikubali CCM wakatumia mafuta kuwa karata yao ya kisiasa. Awali CUF ndio walikuwa wakipiga kelele kuhusu mafuta na hao hao SMZ ndio walikuwa wakimbeza Maalim Seif (rejeeni kampeni za uchaguzi).... sasa wameona hawana ajenda wala hoja wameibuka na mafuta na sasa unasikia mara Ali Karume na baadaye utasikia hata yale ya Salmin ya kutaka katiba ibadilishwe ama hata Muungano ufe ili Rais wetu aendelee!!!!!! he!!!! amkeni na musome alama za nyakati, CCM wanaaza kuiba kuanzia hoja, daftari na baadaye kura na kumalizia hata hesabu za kujumlisha na wakiona haitoshi wataiba hata utangazaji kwa maana utashinda wewe watatangaza yule!!!! Huu si utani, upo ushahidi wa yote haya.
   
 15. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  angesubiri aje mtu mwingine baada ya kaka,kisha labda ndiyo yeye, huyo mtoto wa mwinyi sawa tu.
   
 16. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wamesema sio ufalme, ila ni KULINDA MAPINDUZI.
   
 17. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mmungu amesema yupo na wenye kusubiri sasa tusubiri kauli ya aliyemiliki na ya mpangaji ipi yenye nguvu.
   
 18. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ana haki ya kugombea kama anatimiza masharti na kanuni zilizowekwa ili ufae kuwa mgombea wa kiti cha uRais Zanzibar. Baba na Kaka yake kuwa maRais waliopita haimfanyi asigombee. Lakini ni wale tu watakaokuwa katika mchakato wa kupitisha mgombea wa uRais ndio wataangalia jee kati ya walioomba ni nani anafaa zaidi ya wenzake.
   
 19. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nafikiri wakati Umefika wa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kumteuwa mmoja kati ya watoto wake kuwania URAIS kama inavyofanyika ZANZIBAR.
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa nini asubiri?
   
Loading...