Ali Hassan Mwinyi : Mzee rukhsa Safari ya Maisha Yangu

Mzee mwinyi, raisi bora kuwahi kutokea tz. Anashika no. 1 akifuatiwa na kikwete, no 3 mkapa. Nne na 5 simalizii, naona mama anakuja kasi kuna watu watapitwa soon. Sina haja ya kuwataja
Umetumia criteria gani mkuu ?
 
Ikiwa nakumbuka vema, mwanzo wa Mheshimiwa Mwinyi kuitwa Mzee Rukhsa ilikuwa ni hotuba fulani aliyoitoa.

Kwenye ile hotuba, Rais Mwinyi alikuwa akiwaasa wananchi kuwa wastahamilivu kwenye imani za watu wengine.

"Alotaka kula ng'ombe, mwache ale, ruksa!"

"Alotaka kula nguruwe mwache ale, ruksa!"

"Alotaka kula konokono mwache ale, ruksa!"

n.k.

Katuni kwenye gazeti fulani ikachomekea "mbona ruksa zimezidi?"

Ni kipindi hichohicho sera ya serikali ilikuwa ni kufungulia uchumi kuwa huria ("Economic Liberalization") n.k.

Mzee Ruksa jina likashika kasi.
 
Hivi Magufuli yeye hakwandika kitabu chochote,huku ndio alikuwa Rais Msomi kuliko wote hapa Tanzania.
Eti nini???? Nyerere unamjua??? Kenge weee!!!
Yule alisoma mpaka vyuo vya watoto wa wafalme na Ma Rais tupu Duniani unavijua???

Jiwe eti Udsm ndo msomi mweee!! Hao Ma profesa wala ugali wa muhogo hao!! Wana roho ya kutuuuuu!!!

Nadhani hukusoma weye kabisaaa...kitabu cha kiada Historia ya Tanzania Drs la nne!!
 
Nimekisoma kitabu cha mzee Ruksa. Pamoja na kwamba ni kizuri, kinaeleweka ila kina mpungufu baadhi ya vitu ambavyo ni muhimu sana katika Autobiography. Kwa wale wanaosoma sana vitabu vya historia za watu kama zilivyoandikwa na wao wenyewe atagundua kwamba Mzee Mwinyi hakutenda haki kwenye mambo yafuatayo:

1. Kwa sababu kitabu hiki kinamhusu yeye bunafsi, tulitegemea kuona vitu vinavyomhusu yeye personally kwa upana zaidi. Mfano amesema yeye ni mzaliwa wa Mkuranga na wazazi wake waliishi huko, Unguja alienda tu kusoma, ila hakutuambia uzanzibari wake ulitokana na nini (maana si wa kuzaliwa). Je wazazi wake nao walihamia Zanzibar, baadae au waliendelea kuishi na kumalizia maisha yao huko Mkuranga?

2. Aliwataja wake zake, ila hakutuambia aliwapata wapi, walikutana katika mazingira gani nk. Mambo kama hayo yananogesha kitabu kwa maana kwamba autobiography inaongea zaidi yasiyojulikana.

3. Hakuongelea kabisa wanae zaidi ya kuonesha picha akiwa ubalozini Misri pamoja na wakeze na watoto hao. Kuna watoto wake ambao ni wanasisa ila hakueleza chochote kuhusu hali hiyo, kama kuna mchango wake katika kuwafanya wawe wanasiasa bora na hatimaye kupewa nyadhifa kubwa kubwa kama uwaziri na ubunge nk.

4. Kitu cha nne ambacho nimeki note kwa haraka ni kwamba aliandika katika kivuli cha Mwalimu Nyerere. Ni kama hakutaka kuwaudhi wapenzi wa Nyerere, kila mara alijitetea kwamba kitu fulani kilianza wakati wa Nyerere au Nyerere alikubaliana na kitu hicho as if yeye hakuwa na maamuzi yake bunafsi kama Rais.
 
Sasa unamchagulia mtunzi kipi aseme...
 
Back
Top Bottom