Ali Hassan Mwinyi kupewa Phd na Open University (Honorary Doctor Of Letters D. Lett) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ali Hassan Mwinyi kupewa Phd na Open University (Honorary Doctor Of Letters D. Lett)

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mpandafarasi, Nov 22, 2011.

 1. Mpandafarasi

  Mpandafarasi Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu kama kawa tunaendelea kuwapata madoctors hapa Bongo. Open University nao kwa kufuata wenzao wa Mlimani wameamua kumtuza Mzee Ruksa lidigrii la Udaktari.

  Kwa maelezo zaidi bofywa katika mtandao wa Chuo Kikuu Huria katika list ya prospective graduands pg 53.
   

  Attached Files:

 2. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hongera Mh. Rais mstaafu kwa kupat PhD ya heshima. Lukuvi pia atapata shahada ya uzamili kutoka chuo hicho. Pengine niulize swali la ufahamu: PhD ya heshima hutolewa kwa mtu mwenye sifa zipi?
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Halafu eti Doctor of Letters, ameandika nini huyu? nakumbuka Mkapa alipewa baada ya kuandika kitabu.
   
 4. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,382
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Mwinyi anastahili hiyo tuzo mara mia kuliko JK
   
 5. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Kaizari juliazi aliwahi kuveshwa taji la heshima mara tatu,na mara tatu amelikataa. Jamani kwanini sisi tunakuwa wepesi wa kukubali rundo la titles?. If you deserve it ,heshima pale pale taji or no taji.
   
 6. K

  Kudi Shauri Senior Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jama HAKUNA UNIVERSITY DUNIANI INAYOTOA PhD [Doctor of Philiosophy] ya HESHIMA. Wanachopewa hawa wote Kikwete; Mwinyi etc ni Doctor of Letters Honoraris Casa [DLett] au Doctor of Laws Honoraris Casa [LLD Honoraris Casa]. Hizi ni degree za heshima kutambua mchango wa mpewa katika jamii. Anaweza kupewa mtu yeyote yule ili mradi Senate ya University imeridhika kuwa mchango wa mpewa kwa jamii unastahili kupata heshima kama hiyo. Sio lazima mtu anayetunukiwa hizi digrii za Honoraris Casa awe ana digrii ya kwanza au MSc/MA.

  Uamuzi wa kutoa LLD/DLett Honoraris Casa unafanywa na wajumbe wa Senate na Council ya University kwa kupiga kura - majority lazima wa kubali na mwisho Chancellor wa University naye kukubali. Honorary D.Lett na LLD unaweza kunyanganywa saa yoyote ile kama vile University of Edinburgh mwaka 2004 ilipomnyanganya Mugabe Hon DLett. [waliyomtunukiwa kwenye early 1980s] baada ya kutaifisha mashamba ya walowezi wa kiingereza huko Zimbabwe.. Hii inafanyika kwa Senate na Council kupigia kura hoja ya kumnyanganya.

  Katika miaka 40 ya kwanza ya UDSM sidhani kama walitoa any Honorary Degree. Nakumbuka katika miaka ya early 1980s kulikuwa na mjadala wa kumpa kiongozi mmoja wa nchi aliyekuwa rafiki wa karibu wa Mwalimu Hon LLD - lakini Senate ilisita kutoa digrii hiyo hasa baada ya kutafakari hali tete ya siasa huko Southern Africa wakati ule na mchango wa Kiongozi yule katika hali hiyo. Sasa hivi inaelekea kuna mashindano katika universties za hapa nchini kuzitoa hizi Hon LLD na DLett ambazo zinatolewa kama zawadi!

  PhD inatolewa na University baada ya mtu kufanya utafiti na kutayarisha thesis yenye original work ambayo imetahiniwa na kukubalika na examiners [usually senior professors waliobobea kimataifa katika fani hiyo] watano au zaidi. Ni lazima apewaye PhD awe na qulifications za kupewa shahada hii - at least a Masters degree. PhD ikishatolewa na University haiwezi kunyanganywa - walichofanya Waingereza katika London School of Economics kumnyanganya Saif Gaddafi PhD yake baada ya vita vya Libya kuanza ni umalaya wa kisiasa na kitaaluma.

  Kwa hiyo tusichanganye PhD na hizi degree za Honoraris Casa - ni vitu tofauti kabisa.
   
Loading...