Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,395
- 92,721
Kura haziibiwi kwenye kituo cha kupiga kura, kura za Rais zinaibiwa kwenye majumuisho ya nchi nzima.Kwa mtu yoyote mwenye akili timamu anajua fika ccm wanategemea kura za wizi ili kutangazwa washindi. Sababu hasa ya kusema wakala wa kituo atapewa nakala ya matokeo ni ili kulinda wizi huo. Kuna hili la tume kupeleka mawakala sehemu watakayo wao, lengo ni ili wachelewe vituoni waingize hayo mabox ya kura yenye kura ndani. Ushauri mchungu, bila kujiandaa kwa machafuko tutegemee uchaguzi wa kihuni kupita maelezo, na uhuni huo utakuwa ndiyo njia rasmi ya ccm kuendelea kukaa madarakani.
Hakuna namna yoyote ya kuiba kura mkiwa na mawakala wakweli na mkawa na senta yenu kila kata ya kujumlisha kura za diwani, kura za jimbo na kura za Rais.
Huitaji Tume ya uchaguzi kukutangazia mshindi, mshindi mnamjuws nyinyi wenyewe mkiwa na timu nzuri ya kuratibu ukusanyaji wa nakala za matokeo kila kata, jimbo na mkoa kwa ujumla.
Maalim Seif huwa anakuwa ameshaliza majumuisho ya kura kabla ya Zec na ndio maana Jecha akaona isiwe tabu bora afute uchaguzi.
Nina wasiwasi mkubwa na Chadema sidhani kama wana timu ya uhakiks ya kusimamia kura za urais.
Makao makuu ya Chadema pamepwaya hakuna briefings zozote za uchaguzi badala yake sasa Lisu ndio anaibeba Chadema.
Kwenye uchaguzi uliopita Ukawa walikuwa na ngome yao Kawe kwa ajili ya briefings, kule Kenya Odinga alikuwa na ngome yao waliita Pentagon ndio ilikuwa inaratibu, lakini Chadema sijui tatizo ni nini?
Bila Lisu kurudi ni kweli Chadema ilikuwa inakwenda kupata aibu ya mwaka, ila Mungu mkubwa Lisu amerudi amebadili upepo ccm inakwenda kuangushwa, lakini kuna mikakati gani ya kichama badala ya kumtegemea Lisu kwa kila kitu?