Algeria: Vijana wasio na ajira kuanza kulipwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune amesema ili kulinda utu wa vijana serikali itawalipa vijana kila mwezi, robo tatu ya kima cha chini cha mshahara wanachopokea wafanya kazi

Nchi hiyo inayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika itawalipa vijana kila mwezi dinari 13,000 sawa na takribani Tsh. 230,000 kuanzia mwezi wa tatu mwaka 2022

Pamoja na hilo vijana watanufaika na bima ya Afya na kuondolewa kodi kwenye baadhi ya bidhaa. Kiwango cha kutokuwa na ajira nchini humo ni 15%

=======

Algerian President Abdelmadjid Tebboune said Tuesday that the government would introduce youth unemployment benefits as the North African nation struggles with a jobless rate of almost 15 percent.

The payments will be made “to preserve the dignity of young people,” Tebboune said in an interview broadcast on Algerian television.

Algeria will offer its jobless a monthly grant of 13,000 dinars (around $100), a decision aimed at alleviating the economic crisis,d Tebboune told reporters.

The allowance — equivalent to nearly two-thirds the minimum wage of 20,000 dinars ($142) — will begin in March.

It will be accompanied by medical benefits, while some taxes on consumer products will also be suspended, Tebboune said.

Algeria, Africa’s biggest gas exporter with around 45 million people, earns some 90 percent of its state revenues from hydrocarbons.

Tebboune said the youth payments were part of the 2022 budget.

In November, lawmakers voted to scrap generous state subsidies on basic goods that had long helped maintain social peace, but that had strained state budgets as energy revenues fell.

Meanwhile, the Algerian leader also said that an Arab League summit will be held in the fourth quarter of this year, after previously announcing that it would be postponed.

The 31st Arab League Summit was set to be held in March after Tebboune said his country would host it in November. The new date of the meeting will be announced next month.
 
Mama anasema vijana tuchangamke,fursa ni nyingi.Na kama mtu hana pesa basi hafanyi kazi. Mikopo ya halmashauri wanayaoinadi imejaa urasimu mkubwa na rushwa.Viongozi wa CCM wanaunda vikundi wanaiba na Serikali ipo inaangalia!

Hivi hapa Tanzania kuna fursa gani kuizidi Algeria!.na watu hawana bado ajira huko! Serikali iache kutoa majibu mepesi tu kwa vijana kuhusu suala la ajira,hii ni crisis ya Nchi nyingi.Suala ni nyeti na inabidi litazamwe kwa upekee wake.

Kuwaambia watu kuna mikopo halmashauri wakati mnajua mmeweka miungu watu huko,ni kuwakosea vijana. Ni bora Iundwe idara itakayokusanya hizo asilimia mbili kwa kila halmashauri kisha vijana wakaomba mikopo midogo hapo.

Vinginevyo hiyo hela ambayo ni makusanyo kutoka kwa wananchi wenyewe mmeamua kuiiba. Sisi hata bima ya afya hatuna,kama huna pesa watu wanakuangalia unakufa,na baada ya hapo maiti yako inazuiwa mpaka ulipe deni!

CCM,CCM,CCM...jiangalieni sana.
 
Rais wa Algeria ametangaza kuwalipa vijana
Wasio na kazi nchin humo kila mwenz 213000
Mpka pale watakp pata kaz na kutoa mahitaji Mengine bure kama matibabu
 
Tuombe dua Tutafika huko na zaidi!
Kumbuka zama za jiwe tuliambiwa pesa ile tuliyo dhulumiwa kwenye madini tu wakisha tulipa kila Mwananchi Atamiliki NOAH!
 
Yeye ni nani mpaka akatae pesa anatoa yeye?
Yeye anataka watu waige kutoka kwake hata kama mabaya,.Ukifanya mazuri hata kwa Raia wako yeye hapendi,Anataka watu wawe Wanatubu ili yeye apate chance ya Kuingia.
 
Ukosefu wa ajira ni 15% tu,sio huku asilimia 85% na bado uongo mwingi,wachache wanafaidika na walioshika mpini kwa kuwa wapambe au kujuana.
 
Back
Top Bottom