Alfu lela u lela: Kisa cha punda, fahali na mkulima

Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
19,217
Likes
26,139
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
19,217 26,139 280
HAPO kale, akaanza Waziri Mkuu, paliondokea mkulima mmoja tajiri aliyekuwa na kundi la wanyma wa kila namna na
aliyejaaliwa kujua lugha zao. Hakuna aliyejua siri hiyo kwani ali￾yemfundisha alimwonya asiitoe ama sivyo atakufa!
Basi katika banda moja mkulima huyo aliwaweka wanyama
wawili: punda ampandaye aendapo safarini, na fahali amlimiaye
shamba lake. Ikawa kila jioni, baada ya kazi, fahali humwendea
punda aliyewekwa mahali pazuri penye nafaka nyingi na maji safi
ya kutosha, ili aongee naye.
Kwa kuwa yule mkulima hakuwa na safari nyingi, ikawa
kazi ya yule punda ni kula na kupumzika tu mle bandani wakati
mwenzake fahali anababuka kwa kazi ngumu ya kukokota jembe
zito kule shambani!
Siku moja yule mkulima alimsikia fahali wake akimwambia
punda, “Bahati ilioje hiyo uliyo nayo mwenzangu! Mimi humenyeka
kutwa shambani ilhali wewe mwenzangu wapumzika kutwa humu
bandani ukilishwa na ukinyweshwa vizuri bila hata kupandwa na
bwana wetu!”
Punda akamwambia fahali, “Tumia akili, rafiki yangu; bila
kutumia akili mambo hayaendi. Kwa hiyo, nakushauri ufanye
hivi: kesho utakapotiwa hatamu kwa madhumuni ya kupelekwa
shamba, jibwage chini ujifanye mgonjwa! Usinyanyuke hata kama
watakutandika mijeledi mia! Ukinyanyuka, jibwage tena chini; na
watakapokurudisha hapa na kukuletea nyasi, susa kabisa kuzila!
Fanya hivyo kwa muda wa siku mbili tatu upate kupumzika!”
Mfanyakazi alipompeleka shamba asubuhi ya pili, yule
fahali akajifanya mgonjwa wa kufa! Na aliporudishwa bandani
na kuletewa nyasi, akafuata ushauri wa mwenzake punda. Ndipo
mkulima akamwambia mfanyakazi wake, “Leo mwache fahali
apumzike, mchukue punda akafanye kazi yake!”
Jioni, baada ya kufanyishwa kazi kweli kweli, yule punda
akarudishwa bandani yu hoi taabani! Alipoingia ndani, yule fahali
akamshukuru punda kwa ule ushauri wake mwema uliomfaa sana;
lakini punda hakujibu kitu ila alijuta kimoyomoyo kwa kumshauri haraka mwenzake bila kufikiri matokeo yake yatakuwaje!
Siku ya pili mfanyakazi akaja tena, akamchukua punda,
akaenda akamfanyisha tena kazi kutwa mpaka jioni. Aliporudishwa
hoi, yule fahali akamshukuru tena mwenzake.
“Laiti nisingemshauri!” Punda akajuta kimoyomoyo; hapo
akamgeukia mwenzake akamwambia, “Sahib yangu, nilipokuwa
nikirudi, nilimsikia bwana wetu akimwambia mfanyakazi: ‘kama
fahali hakupona, kesho mpeleke machinjoni akachinjwe!’ Kwa
kuwa u rafiki yangu mpenzi, nimeona ni kkheri nikuarifu mapema
upate kujua mambo yalivyo!“”
Fahali kusikia vile, akamshukuru tena mwenzake, akamwam￾bia, “Kesho nitajitolea mwenyewe kwenda kazini!”
Asubuhi ya pili mkulima na mkewe wakenda kule bandani
kumwangalia fahali huku wakiongozana na mfanyakazi. Wal￾ipofika, wakamwona fahali anatimka mbio mle bandani huku
akitoa mashuzi kuthibitisha kuwa yu mzimwa wa kigongo! Hapo
mkulima akaanguka kicheko akacheka sana!
“Una cheka nini, mume wangu?” Akataka kujua mkewe.
Mume akamjibu, “Linalonichekesha halifai kuambiwa mtu; si
wewe wala si mwingine.”
Mke akashikilia lazima aambiwe; mume akakataa katakata
mpaka kule nyumbani kwao kukawa hakuna tena furaha isipokuwa
bughudha, manung’uniko na kununa kwa mke aliyedai sharti aam￾biwe lililomchekesha mumewe siku ile.
Alipoona hali ya nyumbani mwake imekuwa mbaya, siku
moja mume akamwambia mkewe, “Nitilie maji nikaoge nivae
nguo tohara nisali ndipo nitakapokuambia kile kilichonichekesha
siku ile; lakini ujue kuwa mimi si mumeo tena maana nikikuambia,
nitakufa!”
Mke asijali; mradi atimiziwe lile alilolitaka. Basi akafanya
kama vile alivyoambiwa na mumewe.
Alipokwisha sali, mume akamwambia mkewe, “Kwanza
nakwenda kuwaaga wazee wangu, ndugu zangu, na jamaa zangu.
Nitakaporudi, nitakuambia kilichonichekesha siku ile.”
Wakati alipokuwa akielekea kwa wazazi wake, njiani mkulima
akamkuta jogoo wake amewakusanya makoo hamsini akiwabe￾beza huku wote wakiwa katika hali ya furaha na ya maridhawa.
Lakini mbwa wake aliyekuwa karibu na aliyekuwa amejikunyata
kwa huzuni na majonzi, akamwambia jogoo, “Mbona mwenzetu
huna huzuni?”
“Kwa nini niwe na huzuni?” Jogoo akataka kujua.
“Unacheka na kufurahi na makoo wako ilhali unajua kuwa
bwana wetu atakufa leo; huna hata huruma?” Akasema mbwa
kwa huzuni.
“Nini kitakachomwua bwana wetu? Mbona namwona yu
mzima wa kigongo tena anaonekana ana afya nzuri?” Akauliza
tena jogoo.
“Sababu,” akajibu mbwa, “ni mkewe ashikiliaye kuambiwa
neno ambalo bwana wetu akimwambia, atakufa!”
Jogoo kusikia vile akasema, “Basi bwana wetu ndiye mjinga
wa mwisho! Hebu nitazame mimi; nina makoo hamsini wanitiio
wote kwani nawafurahisha na nawaridhisha vilivyo bila tatizo lolote
ilhali bwana wetu ana mke mmoja tu amsumbuaye na kumwumiza
kichwa kutwa kucha! Kama mkewe hasikii maneno yake, basi aende
dukani akanunue hainzarani amtandike mikwaju mpaka mke ashike
adabu na akome kuulizauliza mambo yasiyomhusu!”
Yule bwana kusikia maneno ya jogoo, akaenda zake moja
kwa moja mpaka dukani, akanunua bakora nyembamba ya mtobwe,
akarudi nayo nyumbani kwake. Alipoingia ndani, akamwita mkewe
chumbani. Alipokuwa ndani, akaubana mlango vizuri, akamtandika
mkewe bakora za kutosha mpaka mke akakoma kuzaliwa! Mke
akataka kujua sababu ya kupigwa vile; ndipo mumewe akamjibu,
“Lililonichekesha siku ile na ulilialo sikuzote ndilo hili; na kama
unataka zaidi sema!”
“Toba ya Rabbi!” akalia mke kwa maumivu makali huku
akipiga mayowe, “Nimekoma, mume wangu, wala sitaki tena kulijua
lile lililokuchekesha siku ile!”
* * *
BAADA YA Waziri Mkuu kusimulia kisa hiki, Shahrazad
akasema, “Hakuna chochote kitakachonibadili nia katika jitihada
yangu niliyoikusudia kuitekeleza.”
Basi Waziri Mkuu ikawa hana budi kumpamba bintiye kwa
lebasi za hariri na vito vya tunu kabla hajampeleka kwa Sultani.
Lakini kabla hajaondoka, Shahrazad akamwambia Dunyazad,
“Mdogo wangu, nitakapopelekwa kwa Sultani, nitakuagiza uje.
Usiku, kabla hakujapambazuka, uniamshe, useme, ‘Dada yangu,
tafadhali nakusihi unisimulie moja ya hadithi zako tamu za kusi￾simua ili nipate kuipitisha sehemu iliyobaki ya usiku huu tutaka￾okuwa pamoja kwa mara ya mwisho.’ Halafu nitakusimulia visa
ambavyo, Inshaallah, natumaini vitakuwa ni chanzo cha mwisho
wa msiba uukabilio umati wa mji huu.”
Basi Waziri akamchukua Shahrazad mpaka kwa Sultani.
Sultan Shahriyar alipoufunua ushungi wa Shahrazad, akastaajabu
sana kuona uzuri wake usio kifani.
Basi usiku wa manane, baada ya starehe na maburudiko,
Shahrazad akamwambia Sultani kwa unyenyekevu, “Ewe Seyyid
yangu, nina mdogo wangu nimpendaye kuliko mboni za macho
yangu; nataka kumuaga kabla hakuja kucha. Nakusihi niidhinie aje
niagane naye kwa mara ya mwisho.”
Mara ileile Sultani akatoa amri Dunyazad akaletwe. Alipofika,
akamkumbatia dada yake na kabla hakujapambazuka, akasema,
“Dada yangu mpenzi, tafadhali nakusihi unisimulie moja ya hadithi
zako nzuri ili tuipitishe sehemu ya usiku huu tutakaokuwa pamoja
kwa mara ya mwisho.”
Hapo Shahrazad akamgeukia Sultan Shahriyar, akasema,
“Itakuwa ni furaha kwangu iwapo Sultani ataniridhia.”
Sultani, ambaye hakuwa na usingizi wakati ule, akakubali na kumsikiliza Shahrazad akasimulia.
 
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
19,217
Likes
26,139
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
19,217 26,139 280
Hiki kitabu ninacho,ninakipenda sn.nilikichukua maktaba mwaka 1984 nikiwa shule.nimekitunza sn.na pia ninakipenda sn.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pongezi na hongera sana chief, watoto wa kileo watakushangaa na hawato kuelewa ikiwa watasoma jinsi unavyo kithamini na kukitunza kitabu hiki
 
Ochumeraa

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2015
Messages
1,916
Likes
1,559
Points
280
Ochumeraa

Ochumeraa

JF-Expert Member
Joined May 18, 2015
1,916 1,559 280
Ngoja nicoment kwanza,halafu nikaisome
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,633
Likes
125,262
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,633 125,262 280

siku alfu na moja... Boss usisahau kuleta na Adili na nduguze

Jr
 
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
19,217
Likes
26,139
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
19,217 26,139 280
siku alfu na moja... Boss usisahau kuleta na Adili na nduguze

Jr
Unenikumbusha jinsi ambavyo Adili, kijanamwenye roho na tabia njema, alihusudiwa na ndugu zake (Hasidi na Mwivu), walimchukia na kumpatia mateso na kumweka katika hali ngumu katika nyakati tofauti.

Hao walimtesa kiasi cha kutosha na kama malipo ya makosa yao wakageuzwa manyani na jini liitwalo Huria. Lakini kwa moyo wake mwema Adili akayaombea msamaha baada ya miaka mingi yakitunzwa naye kwa mateso ya kuyapiga kiboko kila usiku na kuyapa posho.

Baada ya hapo Huria alikubali pendekezo la Adili wakarejea katika utu tena. Mara baada ya baba yao kufariki dunia Adili na nduguze waligawana mali sawa kwa sawa katika sehemu tatu.

Ebu subiri pakuche chief.....
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
104,633
Likes
125,262
Points
280
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
104,633 125,262 280
Unenikumbusha jinsi ambavyo Adili, kijanamwenye roho na tabia njema, alihusudiwa na ndugu zake (Hasidi na Mwivu), walimchukia na kumpatia mateso na kumweka katika hali ngumu katika nyakati tofauti.

Hao walimtesa kiasi cha kutosha na kama malipo ya makosa yao wakageuzwa manyani na jini liitwalo Huria. Lakini kwa moyo wake mwema Adili akayaombea msamaha baada ya miaka mingi yakitunzwa naye kwa mateso ya kuyapiga kiboko kila usiku na kuyapa posho.

Baada ya hapo Huria alikubali pendekezo la Adili wakarejea katika utu tena. Mara baada ya baba yao kufariki dunia Adili na nduguze waligawana mali sawa kwa sawa katika sehemu tatu.

Ebu subiri pakuche chief.....
agiza za moto mbili usije kupata vichomi ukashindwa kuendelea

Jr
 
Forum statistics

Threads 1,251,652
Members 481,834
Posts 29,779,298