MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Hawa ni viongozi wastaafu wa jeshi la polisi ambao walitenda wajibu wao kwa weledi mkubwa kwa kuitumia sheria ipasavyo, kuitambua katiba ya nchi na demokrasia kwa ujumla pamoja kutumia hofu ya Mungu!
Ni viongozi ambao walitumia njia ya majadiliano kutafuta suluhu kila kunapotokea sintofahamu hasa kuhusu masuala ya kisiasa!Hawakupenda kushinikizwa kufanya kazi ispokua walizingatia sheria,kanuni na taratibu za kazi zao. Lakini pamoja hayo yote nao walikua na mapungufu makubwa tu lakini kuna tofauti kubwa kabisa ya utendaji wao na hawa wa Sasa tunaowaona, polisi wa Sasa kazi zao zinapwaya kabisa, wanafanya upendeleo wa wazi wazi bila hata kuzingatia sheria za nchi.
Kwa utendaji huu wa jeshi letu la polisi kwa muda huu wa uchaguzi watasababisha maafa makubwa kwa raia!
Binafsi sioni mantiki yeyote ya kumwacha mtu anayetukana wazi wazi na kuhangaika na yule anayetembea mtaani kusalimia wananchi wenzake kwa kisingizio cha kuhatarisha amani yake, kuna mantiki gani kuzia wanachama wa chama kimoja kuandamana kuelekea kwenye mikutano yao ya kampeni ili hali chama kiingine wanaandamana, mtu akikwambia "usipoyapata mabadiliko nyumbani kwako utayapata nyumbani kwangu" anaitwa mchochezi!Haya yote hatukuyashuhudia huko nyuma lakini leo tunayaona.
Kwahiyo kuna kuna kila sababu ya kuwakumbuka makamanda hawa wastaafu kwa maana wamaliza kazi mikono yao ikiwa misafi! Na hawa pia tunawaomba wafuate nyao ya wastaafu hawa ukizingatia siasa sasa ni tofauti na ya zamani, watu wameongezeka,mazingira yamebadilika,mbinu za kufanya siasa zimebadilika zimekua za kisasa zaidi!
Wasitumie mabavu na ubabe kuzuia vuguvugu flani badala ya kuzingatia uhalisia wa mambo na kutafuta suluhu kwa majadiliano na wahusika.