Elections 2010 Alfred Tibaigana kugombea Ubunge

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Na Maulid Ahmed
Daily News;
Saturday,May 24, 2008



Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Alfred Tibaigana anayetarajia kustaafu Julai mwaka huu amesema huenda akagombea ubunge katika Jimbo la Muleba Kusini mwaka 2010.

Mbunge wa sasa wa Muleba Kusini ni Wilson Masilingi wa CCM ambaye wakati wa awamu ya tatu, aliwahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais aliyeshughulikia Utawala Bora. Akizungumza na gazeti hili jana, Tibaigana ambaye anatarajia kustaafu rasmi Julai 5 mwaka huu, alisema amepata ujumbe kutoka kwa wakazi wa Muleba Kusini wakimtaka aende kugombea ubunge katika jimbo hilo.


“Kwa sasa bado sijaamua kwa sababu familia yangu imegawanyika, nusu yake wanataka nigombee na nusu wengine hawataki, sasa tunajadiliana na wakikubali basi nitagombea mwaka 2010,” alisema Tibaigana ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Muleba.


Mbali na nia hiyo ya kugombea ubunge, Tibaigana alisema kuwa atakapostaafu atajihusisha na biashara ya kuendesha hoteli ambayo ameshaijenga pamoja na wenzake eneo la Mkuranga mkoani Pwani. Hakuwataja wenzake. Kwa mujibu wake, Mkuranga pia ana shamba la mananasi, mapasheni na anafuga nguruwe, mbuzi, ng’ombe na kondoo.


Pia kijijini kwao katika Kata ya Buganguzi, wilayani Muleba ana shamba la migomba na anafuga ng’ombe. Wakati anaondoka katika nafasi hiyo ya ukamanda wa Dar es Salaam, Tibaigana mbali na kuwashukuru wakazi kwa ushirikiano waliompa katika kazi, ametoa mwito waheshimu sheria kupunguza ajali.


Kabla ya mwaka 2006 alipoteuliwa kushika wadhifa alio nao (Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam), Tibaigana alikuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu 2001. Kanda ya Dar es Salaam inajumuisha mikoa ya polisi ya Kinondoni, Ilala na Temeke.


Alitokea mkoani Arusha ambako alishika wadhifa huo wa ukamanda wa mkoa tangu mwaka 2002. Alianza kushika wadhifa wa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Tanga mwaka 1997.
http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9202
 
Sasa kama ni kweli watu wa Muleba Kusini wanamtaka na CCM hawataki kumpitisha kugombea na yeye hataki kujiunga na chama kingine kwanini asiruhusiwe kusimama kama mtu huru bila kulazimishwa kuingia upinzani au kuanzisha chama chake? Kama kweli watu wa Muleba wanamtaka si wanaweza kumchagua hata akiwa mtu huru?
 
NAFIKIRI HUU NDIO WAKATI MUAFAKA WA KUTUMIA ZILE HELA ALIZOKUWA ANAPATA KUTOKA KWA MAJAMBAZI BAADA YA KUPIGA DILI.....RASTA ,-ILALA,,MAPESA-KINONDONI,,DOTTO NAONA HIVI SASA MTAHAMIA MULEBA KUPIGA KAZI MLEZI WENU ANAAHAMA JIJI SASA KAZI KWENU...HAWA NA WENGINEO MZEE MAHITA ALIMWACHIA URITHI MZEE WETU KUWALINDA ASIINGIE NDANI HATA MMOJA ...MKUU KOVA KAMA UNAITAJI MORE INFO INGIA HUMU TUKUMUGIE NANI WAHUNI WA HIZI DILI ZA MILION 100-500,,WANAJULIKANA NA KWA TAARIFA YAKO KABLA YA KUPIGA GARI ZA POLISI DEFENDER ZILIZOKUWA KARIBU NA MAENEO ZINADANGANYWA KWANZA KUNA WIZI UMETOKEA LABDA MWENGE WAKITOKA SINZA WAZEE WANAPIGA KAZI WAKIFIKA MWENGE HAKUNA KITU WANAPISHANA NA JAMAA WANARUDI KUPELEKA FUNGU...WEWE MWEMA UTAWAWEZA HAWA HIVI VIZAZI VYA MAHITA SI VYA KUBAIDLISHA TU NA KUSAMBARATISHA KABISA ...MZEE KOVA BILA KUSAHAU UKIINGIA EMBU KIFANYIE KAZI KILE KITUO CHA KINONDONI NA CHANGOMBE POLISI WAKE WENGI HUWA WANAAZIMA SILAHA KWA WAZEE WA KAZI KUFANYIA SHUGULI ASBH KABISA WANARUDISHA...NA KAMA UHAMINI WALIVYO WAJINGA WENGINE WANAPOKEA KWEUPE KABISA WEHU WAKUBWA POLISI HAWA ...MNAWAUA WATU KWA SILAHA ZA KODI ZAO WENYEWE...
MAAMA KOKU BABA KOKU RIDIGIRII NISHALIPATA NARUDI KWETU MULEBA

baba kribu mkuu....uendelee kukumbuka wanaw wako uliokuwa ukitulinda...ila angalia vyema KOVA zake anapiga watu risasi uliza alivyowasafisha uko alipotoka....ukileta ujinga anakumaliza ndio maana nashauri marasta mapesa msibaki nyuma huyu jamaa anawaondoa acheki....Embu tazameni jamani ilifika wakati mtu anaenda kuripoti kaibiwa gari saa kumi usiku pale kituo cha OSTERBAY anaambiwa aahh sehemu gani wakitajiwa polisi anasema aahh huyo marasta..unaulizwa unshillingi ngapi gari ikapatikana .....ukitangaza dau njema hakika gari unaikuta ama wameiacha ama wanawafwata kuwawahi wanapoleka magari yao.....
kila la khero baba KOKU
 
Sasa kama ni kweli watu wa Muleba Kusini wanamtaka na CCM hawataki kumpitisha kugombea na yeye hataki kujiunga na chama kingine kwanini asiruhusiwe kusimama kama mtu huru bila kulazimishwa kuingia upinzani au kuanzisha chama chake? Kama kweli watu wa Muleba wanamtaka si wanaweza kumchagua hata akiwa mtu huru?

...........ok..............!!
 
mahita Nae Si Nasikia Anasubiri Kwenda Morogoro.....??????
 
ninachompendea Mwema Anasoma Nyakati...maana Hata Huyu Ndug Yetu Kamanda Rinbow Alishaanza Kuingia Kundini Labda Akaliendekeze Uko Aliko...
 
•
Mabadiliko makubwa Polisi, Tibaigana ang'atuka


JESHI la Polisi limefanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na wakuu wa upelelezi kufuatia maofisa wake wengi kufikisha umri wa kustaafu kwa lazima ifikapo Julai 1, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema, Kamishna wa Utawala na Fedha, Bw. Clodwig Mtweve, alisema Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Alfred Tibaigana anastaafu na nafasi yake inachukuliwa na Bw. Suleiman Kova, aliyekuwa Mbeya.

Atakayeziba nafasi ya Bw. Kova ni Kamanda wa Mkoa wa Bw.Stephen Zelote ambaye nafasi yake inachukuliwa na Bw. Jamal Rwambow, akitokea Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Bw. David Saibullu anastaafu na nafasi yake inachukuliwa na Bw. Liberatus Lyimo Barlow, ambaye kabla ya uteuzi huo, alikuwa Ofisa Nadhimu Utawala na Fedha Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Aliyeteuliwa kushika nafasi ya Bw. Rwambow Mkoa wa Kinondoni ni Bw. Mark Kalunguyeye, ambaye kabla ya uteuzi wake alikuwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Bw. Ray Karama, aliyekuwa Kikosi cha Kutuza Ghasia, Dar es Salaam ameteuliwa kuwa Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Wezi wa Mifugo Makao Makuu Arusha.

Bw. Mtweve alisema, Bw. Abdallah Msika amehamishwa kutoka mkoani Kagera na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam huku ASP Salewi aliyekuwa Kamanda Mkoa wa Pwani akipelekwa kuziba nafasi yake.

Mabadiliko hayo pia yamemgusa Bw. Mwakyoma aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi na sasa anaenda kuwa RPC Mkoa wa Pwani huku RPC wa Tabora, Bw. Mshahili akirejeshwa makao makuu Dar es Salaam na nafasi yake kuzibwa na Bw. Emson Mmari, aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi.

Bw. Lucas Kusima aliyekuwa Baraza la Ulinzi na Usalama, amehamishiwa Makao Makuu na nafasi yake itazibwa na Bw. Brown Lakey kutoka Makao Makuu ya Upelelezi.

Katika mabadiliko hayo pia yamewagusa wanawake wawili ambapo Bi. Marry Nzuki aliyekuwa OCD Mkoa wa Dodoma anakwenda kuwa Kaimu Kamanda wa Polisi TAZARA huku SSP Lucy Makelemo aliyekuwa OCS Uwanja wa Ndege Mwanza anakuwa Staff Officer I Dar es Salaam.

Alisema mabadiliko hayo pia yamewagusa wakuu wa upelelezi wa mikoa Mara, Kigoma, Shinyanga na Mbeya. Wanaotarajia kustaafu nafasi zao zimechukuliwa na Bw. Msato Marijani aliyekuwa OCD Wilaya ya Biharamulo (Kigoma), Bw. Deusdit Kato (Mara). Kabla ya hapo alikuwa OCD Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
 
Shida yangu ni pale ninapoona kila mtu anatamani kuingia kwenye siasa, ndiyo maana utendaji wa polisi unamwelekeo wa kisiasa siasa kumbe wakuu wao huwa wanatengeneza mazingira ya kukubaliwa kwenye vyama vyao. Baadae tutasikia Mkuu wa majeshi, Mkuu wa PCCB nk wanagombea ubunge.
 
Sipati shida ninaposikia mstaafu fulani katika serikali hata lama ni jeshini akitangaza kwenda kwao kugombea ubunge.

Ila ninausikitikia ubunge unavyodhalilishwa. Hivi kila anayestaafu bila hata ya kukagua historia yake anachoweza kutangaza haraka ni nia yake ya kugombea ubunge?

Kwa upande wa Tiba... sina sababu ya kumwekea mtimanyongo. Ila ninasubiri nione ni kwa kiasi gani anachukia ufisadi na kwamba yuko tayari kupambana nao.

Ama kwa hakika hakuna hata mtu mmoja anayeipenda hii nchi kwa moyo wote ambaye leo hii atajiunga na chama cha mapinduzi eti tu kwa kuwa anataka kuwa mbunge.

Tiba anaweza kabisa kushinda ubunge kwa jina lake mwenyewe kule Muleba. Lakini ninamhakikishia kuwa nitampigia kampeni endapo ama atachukua kadi ya CHADEMA au chama chochote cha upinzani au awe tu mgombea huru. Akifanya hivyo nitampigia kampeni kwa sababu nitakuwa nimejiridhisha kuwa yeye ni shujaa mpambanaji mwenzetu.

Na kama ataenda CCM ajiandae kupingwa na wanaCCM wenyewe na sisi wanamapinduzi kwani wanaCCM hawako tayari kumpokea mtu anayesema wazi wazi. Kusema wazi wazi kuko upinzani tu!!! Mimi Kamende nitampinga kwa sababu siamini hata kidogo kuwa hata Malaika akija leo akajiunga na CCM anaweza kufanya mabadiliko yoyote. Chama kimeoza mno hakifai hata kwa kuungwa na tangawizi na vitunguu swaumu

Karibu Mshaija!!!
 
Haya ni matatizo ya wabongo ,mtu umishafanya kazi miaka kibao na ukifika wakati wa kustafu unatafuta jipya ,hivi ni lini watu hawa wataelimika kwani maana ya kustaafu ni kutumia muda wa uhai wako uliobaki kukaa na kustarehe na familia yako ,ukifuata maisha ya kufanya ziara za hapa na pale yaani unageuka na kuwa katika kundi la utalii kuitazama dunia ,kama huyu ana karadi ka hoteli,kuku,mbuzi ngamia sasa kwenda kujitumbukiza kwenya siasa haoni kama wengine zimewatoa ngeu ,mi namshauri achukue familia yake aende Bang Kok Thailand akapumue na kufanyiwa masaji kiasi ya wiki mbili tu.
 
HAKUNA CHA KUSIFIA HAYA MABADILIKO!,"AMETOA KOPO AMEINGIZA BOX"!.
KUNA MAFISADI,MABINGWA WA RUSHWA,WATAALAM WA NGONO HATA WENGINE WAMEPATIWA JINA "KING MSWATI" BADO WAPO WAMEKUMBATIWA NA MWEMA!.
HAPO MAKAO MAKUU YAO WAMEJAA WAZEE AMBAO HAWAZEEKI KILA MMOJA ANA MIAKA 45!!!!,RAIS ACHUKUE HATUA ZA HARAKA KUIOKOA NCHI HII KWANI KUNA SHUTUMA MBAYA SANA ZINAZOLIKABILI JESHI ZA USHOGA AMBAO KUNA VIGOGO NDIO ZAO KUHARIBU VIJANA KWA KUWAPATIA UPENDELEO KATIKA KAZI!!.

na Juma Masumbwi, bagamoyo, - 24.05.08 @ 11:35 | #13046

Source: Maoni from Tanzania Daima
 
TUNAKUSHUKURU SANA MWEMA KWA KUTUTOLEA HUYU MZINZI HAPA MWANZA ANAJISHAUA TU HATA KAZI KASHINDWA KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU NDIO ZAKE MBEYA NDIO KWENYEWE UKIMWI AKAUZOE MJIANDAE
na MASANJA, nyakato, - 24.05.08 @ 10:23 | #13027
 
Lakini wakubwa hili la watu kufanya biashara tofauti kabisa na taaluma zao mnalionaje? Kuna Profesa wa Botany namfahamu anamiliki club ya pombe na bendi ya mziki wa kizaire. Profesa mwingine wa uhandisi anaendesha genge la kiti moto, ugali na bia! Yuko profesa wa surgery nilikuwa napishana naye kila siku jioni amebeba makombo ya ugali na wali na maganda ya viazi kwenye pick up yake, alikuwa anapita kuyakusanya kwenye majiko ya vyuo Muhimbili, IFM, CBE na DarTech na kwenye mabanda ya chipsi, kwa ajili ya kupeleka nyumbani kwake kulishia nguruwe. Mwingine alikuwa katibu mkuu wa chama kikongwe kwa miaka kumi, sasa analima viazi kijijini kwao kwa jembe la mkono, lilelile alilokuwa anaimba kwenye sera za chama chake kuwa halina tija, na kuwa chama hicho kingewakomboa wakulima waondokane nalo! Yuko mama mmoja alikuwa mkuu wa wilaya na baadae RDD (siku hizi inaitwa RAS), aliwahi kunitia msukosuko nilipokuwa mwalimu kwenye wilaya yake kwa kosa la kumwadhibu mwanae aliyekuwa anavuta bangi, sasa hivi yuko Visiga ana kiunga cha mihogo na anafuga bata kwa kuwalisha ukoko wa wali anaobakisha, na yule mwanae mvuta bangi bado yupo na ni mtu mzima lakini anamwibia mama yake kila siku! Biashara anayofanya huyo ex-DC: kusuka mikeka na nyungo na kuzipanga barabarani kusubiria wateja!

Na leo tumeambiwa RPC analima mananasi na kufuga nguruwe! Halafu akistaafu atakuwa anaendesha hoteli yake na wenzie (sijui atakuwa mkurugenzi au nani!), lakini nawaza hiyo hoteli yake itakavyoweza kutofautiana na Police Mess!

Mshangao wangu: Kwa nini hawa watu wasifanye biashara katika mambo ambayo wana uzoefu nayo, uwezo zaidi, na credibility? Wenzetu wa nchi zilizoendelea wakistaafu madaraka kama hayo wanatumia uzoefu wao katika ngazi za ushauri, na wanalipwa vizuri sana. Mfano ukitembelea ofisi za Security consultants utakuta ni mashushushu na maaskari wastaafu, na wakikufanyia consultancy ni uhakika! Watu wenye uzoefu wa utawala, uongozi, biashara, kilimo, elimu, sheria, usalama n.k. wanaanzisha firms za consultancy ambazo uzoefu wao pekee kabla hata ya elimu ya darasani ni credibility tosha ya kuwauzia ushauri watu wanaouhitaji, na wanakula kiulaini bila kugombana na watu kwenye hizi biashara ndogondogo! Na hata kama ni biashara kubwa, kama si fani yako itakushinda tu, labda ukodishe kwa mjasiriamali uwe unachukua tu mafao mtayokubaliana.

Nashangaa hivi, kwa nini watu wakubwa tu wenye uzoefu wa mambo yao makubwa mazuri, wanarudi kuzunguka palepale kwenye biashara za genge, viazi, kitimoto, kulima nanasi, kuuza juisi na barafu nk, kwa nini? Kwa nini wanarudi kwenye hatua ambazo kimsingi walipaswa wawe wameshazivuka? Nini kinawarudisha huko?
 
Kimsingi silioni tatizo kwa mstaafu kutaka kuingia katika siasa na kuutumia uzoefu wake kuwatumikia jamii kwa mara nyingine tena akitumia, pamoja na huo uzoefu, busara na hekima za utu uzima. "utu uzima dawa."

Kwangu binafsi, tatizo linakuja, ninapoona kumbe mtu huyo, katika wakati wote alipokuwa anautumikia umma, alikuwa mwanachama mkamilifu na mtiifu wa CCM au chama kingine chochote cha siasa.

Mathalan, huyu Ndugu Tibaigana, kwa matamshi ya azma yake, kabla hata hajastaafu, anatudhihishia kuwa yeye ni kada wa CCM. Kwa mtaji huo, ina mana kuwa wakati wote wa utendaji wake, akiwa mtumishi wa umma, maamuzi yake hayakuwa ya haki sawa kwa vyama vya kisiasa vilivyokuwa vikipingana au vikikinzana na CCM.

Mifano kama hii ya Ndugu Tibaigana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa Maalumu wa Dar-ES-Salaam, ni mingi sana. Unafanana na ule wa "Mzee wa Vijisenti" Andrew Chenge, Attorney General na maamuzi yake wakati akiwa katka kiti hicho. Wapi vyama vya upinzani vinaweza kupata uwanja ulio sawa wa ushindani wa kisiasa?

Katiba mpya, wagombea binafsi, tume huru ya uchaguzi, wabunge wasiwe mawaziri, wakuu wa mikoa pamoja na wale wa wilaya na makamanda wa polisi na vyeo vya aina hiyo wachaguliwe na wakazi wahusika kutoka nje ya vyama vya kisiasa na kadhalika.

Kubwa zaidi kuweka mihimili ya Utumishi (Executive) angalia, nimesema Utumishi sio Utawala, Sheria na Bunge kuwa na nguvu sawa zenye uwezo wa kukosoana na kusahihishana.

Hatamu za utawala ni za wananchi wenyewe kwa njia ya kura zao. Ndio maana ya kujitawala wenyewe.
 
Tiba...siasa hujui kaanzishe TIBAIGANA SECURITY GUARD COMPANY hapo hapo DSM,huku ukiendesha hoteli na kufuga nguruwe.
 
inatisha kuona kila anayemaliza post za juu ndani ya serikali kutaka kugombea ubunge!
kwa sababu it means wapo madarakani huku wakijipendekeza kwa chama, na hapo kazi zao lazima tuzitilie wasi wasi kama zitakuwa zipo na haki kwa watu wa vyma vyengine
 
Sasa kama ni kweli watu wa Muleba Kusini wanamtaka na CCM hawataki kumpitisha kugombea na yeye hataki kujiunga na chama kingine kwanini asiruhusiwe kusimama kama mtu huru bila kulazimishwa kuingia upinzani au kuanzisha chama chake? Kama kweli watu wa Muleba wanamtaka si wanaweza kumchagua hata akiwa mtu huru?

..kwahiyo ana hela za kugombea ubunge, sio?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom