Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
Na Maulid Ahmed
Daily News;
Saturday,May 24, 2008
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Alfred Tibaigana anayetarajia kustaafu Julai mwaka huu amesema huenda akagombea ubunge katika Jimbo la Muleba Kusini mwaka 2010.
Mbunge wa sasa wa Muleba Kusini ni Wilson Masilingi wa CCM ambaye wakati wa awamu ya tatu, aliwahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais aliyeshughulikia Utawala Bora. Akizungumza na gazeti hili jana, Tibaigana ambaye anatarajia kustaafu rasmi Julai 5 mwaka huu, alisema amepata ujumbe kutoka kwa wakazi wa Muleba Kusini wakimtaka aende kugombea ubunge katika jimbo hilo.
Kwa sasa bado sijaamua kwa sababu familia yangu imegawanyika, nusu yake wanataka nigombee na nusu wengine hawataki, sasa tunajadiliana na wakikubali basi nitagombea mwaka 2010, alisema Tibaigana ambaye ni mzaliwa wa Wilaya ya Muleba.
Mbali na nia hiyo ya kugombea ubunge, Tibaigana alisema kuwa atakapostaafu atajihusisha na biashara ya kuendesha hoteli ambayo ameshaijenga pamoja na wenzake eneo la Mkuranga mkoani Pwani. Hakuwataja wenzake. Kwa mujibu wake, Mkuranga pia ana shamba la mananasi, mapasheni na anafuga nguruwe, mbuzi, ngombe na kondoo.
Pia kijijini kwao katika Kata ya Buganguzi, wilayani Muleba ana shamba la migomba na anafuga ngombe. Wakati anaondoka katika nafasi hiyo ya ukamanda wa Dar es Salaam, Tibaigana mbali na kuwashukuru wakazi kwa ushirikiano waliompa katika kazi, ametoa mwito waheshimu sheria kupunguza ajali.
Kabla ya mwaka 2006 alipoteuliwa kushika wadhifa alio nao (Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam), Tibaigana alikuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu 2001. Kanda ya Dar es Salaam inajumuisha mikoa ya polisi ya Kinondoni, Ilala na Temeke.
Alitokea mkoani Arusha ambako alishika wadhifa huo wa ukamanda wa mkoa tangu mwaka 2002. Alianza kushika wadhifa wa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Tanga mwaka 1997.http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=9202