Alfred Lucas wa gazeti la Jamhuri awa Afisa Habari wa TFF

Mwanagandila

Senior Member
Oct 9, 2011
182
100
Kwa mujibu wa tovuti ya TFF, Alfred Lucas ameteuliwa kuwa Afisa Habari mpya wa TFF kuanzia leo April 27, 2016.

Alfred anachukua nafasi ya Baraka Kizuguto aliyehamishiwa katika Kurugenzi ya Mashindano kuwa Afisa Mashindano na Meneja wa Mifumo pepe ya Usajili (TMS).

Alfred ana uzoefu kutoka vyombo mbalimbali alivyovitumikia kama mwandishi wa habari na mhariri.

Kadhalika Alfred kitaaluma amesomea uandishi wa habari, uhusiano wa kimataifa na diplomasia pamoja na lugha.

Mawasiliano ya Afisa Habari,

Alfred Lucas:

Namba ya simu: 0769 088111

alfredkadenge@gmail.com,

Swali ni je TFF imeogopa kutumbuliwa hata kufikia kumuajiri Afisa Habari kutoka katija gazeti hilo ambalo mpaka sasa limeshawafukuzisha kazi viongozi mbalimbali serikalini na taasisi za umma?
 
Back
Top Bottom