Alexander Mnyeti akabidhiwa ofisi mkoa wa Manyara, atoa onyo kali kwa wapinzani

John Walter

Member
Aug 14, 2017
59
57
22853334_1381021475359958_7376771153611314281_n.jpg


Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Alexander
Mnyeti amekaribishwa rasmi katika mkoa wa Manyara tayari kwa kuanza kutumiika
kama mkuu wa mkoa wa Manyara.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema viatu alivyopewa ni vikubwa lakini atajitahidi kuvivaa kwa kushirikiana na wananchi wa Manyara na watumishi katika kuuletea mkoa Maendeleo.

Akizungumzia siasa Mnyeti amesema yeye kama mkuu wa mkoa anasimamia ilani ya chama cha mapinduzi na kutoa onyo kwa wapinzani kwa wakati yeye yupo mkoani Manyara kwamba wafiche makucha yao kwani hatkuwa tayari kusikia chama chake kinachafuliwa na yeyote.

Amesema yeye atafanya kama Mnyeti na hawezi kufanya kama Bendera,’Bendera alikuwa mpole sana ila mimi nitakuwa tofauti”.

Jimbo la Babati mjini linakaliwa na upinzani [CHADEMA] kuanzia madiwani na mbunge,katika kata nane CCM ilipata kata 3 pekee.

 
Arumeru imemushinda utaweza Manyala akija kibabe anapelekwa kibabe.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom