Alert: Pokeeni Salamu Toka Kwa JF Member-Lunyungu.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,723
Ndugu wana JF,

Tunasikitika kuwataarifu kuwa mwenzetu Lunyungu ambaye ni JF member, anaugua mno, hawezi kusimama wala kukaa, anaishi kwenye wheelchair.
His lower disc has been compressed ,ana maumivu makali sana na anasubiria operation.

Anasema anawamiss sana JF members na anamiss the forum.
Kwa yoyote anaetaka kuwasiliana nae, namba yake ni 0767 554433.

Uongozi wa Jf na kwa niamba ya members wote wa JF inampa pole sana na inamtakia afya njema na apone haraka.

Mungu mbariki na msaidie Lunyungu
.
Ndugu wanaJF,

Natumai mnaendelea na mapambano!

Rejeeni quotation ya hapo juu, ambapo tulipewa hiyo taarifa na member(JamiiForums).
Kimsingi, nilimpigia Bwn Lunyungu kuwa ningeenda kumtazama jana[14/9/2010], na kweli alinielekeza kwake maeneo ya Njiro, nikafika, na kwa mara ya kwanza tangu dahari tukafahamiana!.
Kwakweli huyu ndugu jamani anaumwa!...amekuwa totally incapacitated, na ni wa kupewa msaada kwa kila movement anayohitaji...sina maneno zaidi ya kusema ANASIKITISHA!

Waswahili walishasema kwamba JASIRI HAACHI ASILI, huyu bingwa wa mabandiko katika mtandao huu, pamoja na kuongea kwa tabu alinieleza kuwa anawamiss sana members wote na jukwaa kwa ujumla, na akaulizia juu ya mada-moto zinazotamba sasa hivi, nami bila kukwepesha sura nikampa full-mazaga!

Aliendelea kunisimulia jinsi ambavyo huwezi kuelezea Historia ya JF bila kumtaja yeye, maana anasema alikuwa ni mtu wa 3(overall) kujiunga na JF, miaka ya 2006!
Bingwa huyu ni mtu mweledi wa juu sana wa siasa za Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla, na pamoja na maumivu ya mwili aliyo nayo hakukosea kitu katika stories zake!
Kwa ufupi alifurahia sana kutembelewa na mimi kama member, na alikiri kuwa wana-JF ni ndugu!

Back to his health. Lunyungu alikumbana na urasimu wa hatari huko Muhimbili, pamoja na kwamba alikuwa kwenye whee-lchair akiwa hoi!...anasema kuwa moyoni mwake anayo mengi sana ya kuandika juu ya watendaji hao wa hospitali kubwa kuliko zote nchini, pindi atakapopona.
Matokeo yake ni kwamba alikata shauri kwenda kutibiwa nje ya nchi, na anasafirshwa kesho(16/9).

Hujafa hujaumbika....Wana JF nawaombeni sana tumkumbuke huyu mpiganaji katika maombi yetu.
Lakini zaidi tuanzishe namna ya kusaidiana katika shida za namna hii...Lunyungu kwa sasa anaishi kwa madawa makali sana ya kutuliza maumivu, ambapo yana bei kali, nadhani kipato chake chote kinapitilizia huko!

Hatimaye muda wa saa2.30 za usiku niliagana na mwana-mabandiko huyu, nikimtakia kila la heri katika safari ndefu, lakini pia Afya NJEMA pindi atakapofanyiwa upasuaji huko ughaibuni.
Nawasilisha, na Mungu awabariki.

UPDATE ON LUNYUNGU's Health!:

Lunyungu amenipigia simu leo(20/09/2010, saa 9.00jioni hii) toka ughaibuni, akinipa maendeleo ya Afya yake!

Kimsingi nimefurahi sana kupata call yake!

Maendeleo ni kama hivi:

(1)Alifika salama huko eneo la (tukio) matibabu!
(2)Madaktari wa huko baada ya kumchunguza walitupilia mbali dawa zote alizopewa na madaktari wa Muhimbili na kumwanzishia dawa mpya.

(3)Waliikataa kabisa diagnosis iliyoandikwa na Muhimbili, na sasa hivi wanaendelea kum'observe, na bado hawajaestablish shida yake(wakati Bongo walimchunguza kwa dakika chache tu na kuamuru afanyiwe operation!)
(4)Wamechukua samples za makohozi na wanazifanyia kazi.
(5)Ijumaa hii anakutana na 'neurosurgeon' ambaye atamchunguza kwa umakini na kutoa majibu!
(6)Anasema kwa dawa anazotumia sasa hivi tu amepata improvement kubwa sana..Anaweza hadi kupiga mswaki na kunawa mwenyewe, huku akipiga hatua mbili-tatu za kutembea!
(Anamshukuru sana MUNGU, na pia anawashukuru sana wanaJF kwa sala zenu )

HESHIMA KWENU,
MUNGU AMPE AFYA NJEMA.
 
Thanks Mkuu PJ, kwa kweli you have done exactly what you were supposed to, na tunashukuru umetuwakilisha huko wapwa na mabinamu wote hapa JF, ni faraja tosha.

Inatia msisitizo kwamba sisi ni ndugu na however much our differences are, bado tunabaki kuwa ndugu na kufarijiana na kusaidiana kwenye matatizo kama haya ni jambo la muhimu sana sana.

Ndio maana najisikia faraja walau kwa nafasi yako huko uliweza kwenda kumwoma na kumfariji.

Big up sana kwa hilo mkuu
 
Namuweka katika maombi yangu siku zote,Mungu ni mwema sana tunaamini atapona na kurudia afya yake hasa tukikumbuka magonjwa yanatupata sisi wanadamu kuingia ni rahisi lakini kutoka ni tatizo.
Tuko pamoja nae
 
Tunashukuru sana PJ kwa kwenda kumuona mwenzetu na kwa taarifa hii muhimu.
Mungu ni mwaminifu sana, tunaamini atamsaidia na atapona.
Afya njema iwe kwako Bwn. Lunyungu.
 
Oh maskini.....

Thou sikuwahi kupata nafasi ya kumfaham mheshimiwa huyu,
lakini hizi taarifa zimenisikitisha mno, na i do hope kwamba kwa uweza wake Mungu basi atapona.
Inasikitisha sana pia utendaji kazi wa hospitali zetu hizi za taifa, maana cases za namna hiyo si mara ya kwanza kusikia,
wengi wameshaathirika na utendaji huu mbovu na wengi wataendelea kuathirika kama hali hii haitashighulikiwa mapema iwezekanavyo.

Nikupongeze pia "Paka Jimmy" kwa kitendo chako cha ubinadamu na kujali kwa hali ya juu na kwenda kumuona member mwenzetu,
Mungu akubariki na moyo huo....na akuzidishie zaidi na zaidi....

And with God's graces....May his operation be successful and him be back to his normal self soon enough.
 
Thanx PJ Mungu akubariki sana kwa Upendo wako!! Namtakia Lunyungu safari njema na Apone haraka!!:amen:
 
Ah pole sana Lunyungu,
Mungu akutangulie uende salama na kurudi ukiwa na afya njema...
Tutaendelea kukuombea.

PJ thanx kwa taarifa, ubarikiwe kwa kuwa na moyo huo
 
Pole sana Mkuu, all will be well........tunashukuru PJ kwa kujali. una moyo wa pekee.

nakuweka kwenye maombi Lunyungu...
 
Mungu akubariki PJ, umewakilisha vema JF, na Mungu amjalie afye njema mgonjwa wetu Lunyungu, ili aje tujumuike naye hapa.
 
Thanks PJ kwa taarifa, endelea na moyo huo huo,kwa kweli once again umeugusa moyo wangu, Wana JF hebu wote tumpongeze kaka PJ kwa huo moyo wake,kaka huyu ni wa tofauti sana,ana moyo ambao kwa kweli sijui nisemeje, nakumbuka alinitia moyo sana wakati wa harusi yangu alinipa company mno mpaka ndugu zangu walishangaa, tuige mfano wake.

Kwa mwenzetu Lunyungu wana JF tuendelee kumwombea naamini Mungu atamponya.
 
thanks kwa taarifa PJ God bless you for that.
will pray for Lunyungu na afya yake itakuwa njema for God sake.:pray2:
 
Mkuu PJ.. Kazi uliyoifanya MUNGU atakulipa mara dufu! Huwezi jua faraja aliyoipata wakati ukiwa nae hapo... Mungu wa neema amponye Kiongozi Lunyunyu!
 
PakaJimmy thanx kwa kutuwakilisha na kutupa taarifa.
Nilimpigia simu na kuongea naye kirefu sana. Naamini anafarijika tunapomjali hata kwa salaam.

Nina maombi kwa MODS na INVISIBLE.
Kama inawezekana tudundulize sh mia mia zetu kwa wazee wa jukwaa kisha zimfikie kwa ajili ya kununulia dawa na matibabu. Just kumsaidia maana leo kwake kesho kwangu.
Kwa kuanza nitatuma jioni la leo shs 10,000/- na text ya kuelekeza mchango ni wa nini. Nitatuma endapo ombi la kumchangia Lunyungu litakubaliwa. Sijali itikadi, imani, ukabila wala rangi. natukuza UTANZANIA na UDUGU.

Nasubiri jibu ktuoka kwa mods au Invisible
 
PJ safi sana mkuu, Hakika huo ndio upendo wa kweli kumjali mtu pale anapokuhitaji zaidi, kuliko wewe unavyomuhitaji. Naamini Mungu wetu atamponya haraka na baada ya kitambo kidogo tutakuwa nae tena.
 
Safi sana PJ and Lunyungu you will get well soon: PJ tujulishe ni nchi gani ya ughaibuni mdau anapelekwa ili kama anakuja huku tulipo sisi nasi tumtafute na tumpatie msaada wetu tuwezavyo:
 
Mungu akubariki PJ kwa hii information muhimu Mungu siku zote amtupi mja wake na natumaini Mungu yuko pamoja na Lunyungu katika kipindi hiki cha matatizo basi na sisi wana JF tuendelee kumuombea ili aweze kupona na kurudi katika hali yake.
 
Mungu atamsaidia na atapona na kujumuika nasi humu,Pj tunashukuru sana kwa kazi nzuri na moyo wa upendo uliokuwa nao,Mungu akuzidishie maradufu na akubariki.
 
Back
Top Bottom